Swali korofishi: Tanzania ya kujitegemea ni ipi hasa?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Labda kuna Tanzania nyingi,ima hapa duniani au sayari nyinginezo! Kama nchi,tuliponyimwa fedha za Millenium Challenge Corporation (MCC),tuliambiwa na kuaminishwa kuwa Tanzania haikushtuka wala kuathiriwa na kunyimwa huko.

Viongozi wetu walituambia kuwa Tanzania yetu sasa inahitaji kujitegemea. Haihitaji misaada wala mikopo,hasa yenye masharti, kujiendesha. Fedha za MCC zikapondwa bila kupendwa. Zikaonekana si lolote na kunyimwa kwetu kunatuimarisha kama taifa.

Hakika,tuliambiwa Tanzania inataka kujitegemea na kujitenga na misaada pamoja na mikopo. Kuna mtiririko na mfululizo usio na likizo wa mikopo na misaada toka nchi za Ulaya,China,Japan na hata India. Ile Tanzania ya kujitegemea iko wapi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
 
Utajitegemeaje wakati nusu ya makusanyo ni mishahara wanayojilipa watawala na wafanyakazi wao serikalini?
Robo yake inalipa madeni yanayozidi kuongezeka kila uchao

Kwa mikopo hii ya China kuna siku kama hawajataka ndovu wote wangolewe meno yapelekwe kwao basi watadai kumilikishwa kisima cha mafuta au gesi au wapewe mkoa mmoja wahamishie baadhi ya watu wao
 
Mkuu kwani hilo ni suali la kuuliza...? Hali si unaiona?
Nivute sasa umeanza kuvutika. Hivi nani alikwambia dhana ya kujitegemea ni kutoshirikiana na mataifa mengine? Ni katika ushirikiano huo wa kiuchumi, kisiasa (kidiplomasis), kijamii au kiutamaduni nchi hupeana hiki na kile. Unakumbuka kuwa Tanzania iliipa US ruhusa ya kutumia anga letu? Kwa hiyo, haishangazi kuona Tanzania ikitoa hiki kwa yule wakati ikipokea hicho kutoka kwa huyu. Umeelewa? Uchochezi iwe mwisho na mwiko.
 
Back
Top Bottom