Swali: Jimbo la Mbalali, Hakuna CHADEMA?

QUALITY

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
853
115
Wana JF, Salamu.

Ni jana tu nilipata fursa ya kuongea na vijana wawili kutoka Mbalali, mkoani Mbeya na kunielezaa kuwa huko kuna CCM tu na hakuna chama kingine chenye nguvu. Mimi nikataka ushahidi lakini hawakuwa nao.

hata hivyo niliichukua kama point nikataka kujua kwa wana JF mnaoifahamu mbalali, kweli mbalali hakuna CHADEMA?

Naomba nisaidieni mwenye taarifa kamili

Quality Chality
Quality First
 
chadema ipo mpaka nje ya Tanzania.
Labda ufunguke vizuri unamaanisha nini
 
Mleta mada mbona hueleweki..sampuli chache hiyo ikufanye ufikie hitimisho kuwa Mbarali hakuna CDM, Kwa taarifa mgombea ubunge jimbo la Mbarali alipata kura zaid ya 16000 na alishika nafasi ya pili nyuma ya CCM.
 
Mbarali gani gani unayoizungumzia? Kule Chadema ina nguvu sn kwani katika miji mikubwa kama Ubaruku na Chimala madiwani walioshinda ni wa Chadema, lakini vilevile ukitoa wale Wabaluchi ndugu na Rostam waliopewa shamba la Mbarali, ambao ni chukizo moja wapo la wananchi, watu wengi wana support Chadema. Kumbukeni vurugu kubwa iliyotokea mwaka 2011 magari na filling station ya mbaluchi kuchomwa, serikali ilisema ni siasa za Chadema Ubaruku. Kwa kuwahakikishieni tu, Chadema wana nguvu kubwa sana Mbarali, na yale mashamba yaliyobinafishwa ni mtaji mkubwa sana kwani yanawatesa sana wananchi

Inatakiwa kuongeza nguvu kidogo tu, kukumbusha wananchu kuwwa tupo pamoja. Mimi ni mzaliwa na mkazi wa Mbarali
 
Ni kweli kanda zimezinduliwa na juzi tumezindua ya kwetu hapo Kibaha. Pia nakubali kuwa CDM ipo nchi nzima (Generally) Je katika Mbalali tunao makamanda ambao wanatarajia kugombea 2015? kama wapo, ningeomba tuwasiliane ili kuona namna. email yangu ni... quality.chality0@gmail.com. Mungi, niko serious juu ya Mbalali. Nataka tufanye kazi

Quality
 
Halafu kule Mbarali mara kwa mara huwa kuna vita vya panzi (CCM), ndio maana utasikia mbunge amehukumiwa kufungwa, mkuu wa wilaya amezomewa, mara sijui katibu wa CCM ametolewa nduki, mara wameshikiana bastola etc
 
Wana JF, Salamu.

Ni jana tu nilipata fursa ya kuongea na vijana wawili kutoka Mbalali, mkoani Mbeya na kunielezaa kuwa huko kuna CCM tu na hakuna chama kingine chenye nguvu. Mimi nikataka ushahidi lakini hawakuwa nao.

hata hivyo niliichukua kama point nikataka kujua kwa wana JF mnaoifahamu mbalali, kweli mbalali hakuna CHADEMA?

Naomba nisaidieni mwenye taarifa kamili

Quality Chality
Quality First
chadema bado wana kazi ya kufanya, wasikae ofisini wazunguke sehemu mbalimbali katika taifa letu!
 
Mimi ni mzaliwa na mkazi wa Wilaya ya Mbarali. Kuhusu uwepo wa Chadema mbarali ni kwamba ipo lakini nguvu yake sio kubwa na hii inatokana na uzembe wa viongozi,wanaharakati wa chama na wanachama wenyewe kutokuwa commited na kazi ya kukieneza chama maeneo mbalimbali ya wilaya hivyo wananchi kukosa mwamko mkubwa kwa Chadema na ndio maana katika kata ishirini za wilaya Chadema ina kata mbili tu.Lakini nichukue nafasi kuwaomba viongozi na wanachama wa Chadema kuanza kuchangamka na kujitoa kwa moyo ili kuharakisha ukombozi wa Wilaya yetu ili tuweze kukomboka na kupata Elimu,Maji,Afya,Miundombinu mbalimbali,Kilimo bora.Kwasasa nipo nje kwa muda lakini kuanzia mwezi wa saba Nitakuwa Mbarali kuhakikisha harakati zinasonga mbele.Peoples power.
 
Nadhani dawa yake imefika kupitia kuanzishwa kwa kanda. Mimi sina wasiwasi ikwa sasa. viongozi wakiendekeza uzembe mwisho wao ni mwaka huu wakati wa uchaguzi wetu wa ndani.
 
Back
Top Bottom