Swali Fyatu: Yaani mmesahau yote yale mnawalilia vijana hawa?

Unamuunga mkono kwa haya halafu unalaumu ya Nape na wengine waliotumwa na mtu huyo huyo? Na bado wewe hujali taratibu, mradi kaamua lolote analotaka kufanya na linakupendeza wewe unaunga mkono bila kujali taratibu za kuyafanya hayo mambo.

"Kuhamia Dodoma kuliwashinda marais wote, yeye kaweza", hili ndilo liwe kipimo cha ufanisi wa utendaji wake na mengine yote hata yale ya msingi kabisa kama ukiukwaji wa haki za watu tuyasahau?
 
Nadhani tukubaliane kwamba kila mtu ana uhuru
wa kuona anavyoona,ndo maana kila mtu Mungu amempa
macho yake binafsi na si ya pamoja.

Nikuulize yule mwandishiwa habari aliyeuwawa iringa,kwenye kampeni,ilikuwa uongozi huu?
na kama siyo huu je hapo demokrasia ilitumika? Na je kama haikutumika
nipe mfano mmoja wa maendeleo yanayoitikisa Tanzania yaliyofanyika kipindi
hicho ambacho kwa macho yako unaona demokrasia ilitamalaki.
 
Sasa unaniuliza maswali ya kijinga. Ni wapi niliposifu alipouawa mwandishi wa Iringa au kiongozi aliyesababisha mauaji hayo?
Hivi unaelewa tunachozungumzia hapa.

Haijalishi ni kiongozi yupi anafanya mambo hayo mabaya. Kama yapo yatapingwa na kama anafanya mengine kama hayo unayoyasifia wewe, bado hatutaweza kusifu hayo mavitu mazuri anayojenga huku akiendelea kukandamiza anaowajengea mavitu hayo.
.
Hitaji kuu kushinda yote ni haki kwa kila raia kwanza, mengine yanafuata.

Hivi unajua maana ya "maendeleo"?

Unapoondoa haki hiyo, ni upuuzi kumhadaa kwa vitu vitamu huku ukiendelea ukimnyanyasa.
 

Mwanakijiji umezeeka? Umelogwa? Umepuuza akili na ufahamu wako? Umekula maharagwe? Au nini kimekusibu?!!!!

Sikuwahi kukuhisia kuwa siku moja unaweza kufikiri kwa uduni namna hii, udhaifu huu umeutoa wapi, my role model analysit?

Ni kweli unaamini upinzani ni kuunga mkono na kufurahia unyanyaswaji na ukandamizaji wa watu ili mradi tu wale watu wamewahi kuwa kinyume au kukutendea vibaya? Mzee Mwanakijiji, ndivyo ufikiriavyo namna hiyo? Kwamba Nape kushikiwa bastola mchana kweupe, upinzani (Mzee Mbowe) uibuke na kusema ua kabisa huyo? Kweli? Kwamba upinzani ni kuwa wakitukanwa na kudhalilishwa watu useme hata kupiga pigeni tu hao maana sisi ni upinzani hatuwapendi? Kwamba upinzani kwa kuwa ulipigia kelele rushwa, mikataba ya wizi basi mtu akiamka asubuhi akaita gazeti na waandishi na kutangaza Mwanakijiji ni mla rushwa basi ukamatwe na kuwekwa lokapu au leo mtu akisimama akasema nafuta mkataba wa hii kampuni na biashara zake nataifisha bila kufata taratibu na sheria basi upinzani upige makofi na kushangilia?

Mzee Mwanakijiji!! Kwani miaka imeenda umeshazeeka sana? Nini kimekusibu katika fikra zako pevu?

Bado naendelea kuwaza..... bado nawaza tena na napatwa hisia pengine ni Mwanakijiji mwingine sio yule ninayemfahamu.... bado nawaza, kweli ni yuleyule Mwanakijiji?
 

Kama ufikiri huu ndio ufikiri wa wana-CCM, wanasiasa, vyombo vya dola, vyama vya siasa, imani/dini, jamii n.k. basi ni hatari kwa nchi yetu. Kwamba akiumizwa asiyekuwa wa upande wako au aliyekutendea au kukusema vibaya, akikandamizwa akatendewa isivyo haki basi ufurahie na kumuombea shari zaidi.....!!!

Kazi tunayo mzee mwanakijiji.... hakika leo umenipa fursa ya kuwaza!🤔🤔🤔
 
Hujui siasa,Siasa haina adui wala rafiki wa kudumu!Cha msingi unaangalia fursa,mgongano ndani ya ccm ni fursa kwa wapinzani kuchomekea kuni ili moto uwake na wavurugane,hiyo ndiyo siasa!Siasa sio amri kumi za Mungu!!!!
Wabongo sijui tunakwama wapi?Hata kuelewa siasa napo tabu!!!!!

Huyo huyo JPM mwenyewe wakati mwingine anakula maneno yake na kubadilika!!!Angalia hizi-
1.Serikali yangu sitateua wapinzani!!!Je,anefanye hivyo?????
2.Nikitoka chato nitatoa salary slip,miaka imeshakata toka atoe kauli hii akiwa chato!!
3.Nitatoa milioni 50 kila kijiji,sasa tunaambiwa hakusema hivyo bali huduma za elimu na afya ndio zinafidiana humo humo kwenye hiyo 50m.
4.Changia wahanga wa tetemeko,zikachangwa na serikali ikazitaifisha!!!
Kiufupi siasa sio msahafu!!!
 
Mzee unajitoa ufahamu, human nature adui wa adui yangu ni rafiki yangu!
 
Kwani hao ndio wameminya demokrasia na uhuru wa maoni?Tunajua source ni nani na hao ni spika tu kutufikishia!

Hongera kwa kukiri kuwa Tz kuna uminywaji wa demokrasia na uhuru wa maoni!
 
Kwa ufafanuzi huu asipoelewa Bora tuu huyu Mzee Mungu amtwaeee tuu! Ameni
 
Huyu Mzee alishaamua kuunga mkono juhudi na kusahau yaliyopita! ila kuhusu hao vijana namuunga mkono hao vijana wanastahili kupitia hayo wamevuna walichopanda.
 
Hao vijana waliota mapembe wakajiona wamefika angalau wamekumbushwa hawana hati miliki ya vyeo.
Mimi sioni cha ajabu kutoka kwa hao vijana kwa sababu, for what I know, nothing personal! Wapo CCM, na walikuwa wanaipigania CCM, so again, nothing personal, it's all about politics! Kama ambavyo sisi tunavyoita ma-FISICM! It's politics, na ukiona mtu anakuja juu kwa kuitwa ma-FISICM, basi huyo ni mgeni wa siasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…