Swali Fyatu: Yaani mmesahau yote yale mnawalilia vijana hawa?

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
11,825
2,000
Ndo maana mimi ninamuunga mkono
Mh.rais ambaye anafanya kazi inaonekana,kazi kubwa iliyowashinda marais wa awamu zote ya kuhamishia
makao makuu dodoma ameweza yeye na mengine mengi kila mwenye macho anayaona.Na hata kwenye
kampeni zake alisema sitawaangusha,Hakusema hatutawaangusha,Hebu tumuunge mkono.
Unamuunga mkono kwa haya halafu unalaumu ya Nape na wengine waliotumwa na mtu huyo huyo? Na bado wewe hujali taratibu, mradi kaamua lolote analotaka kufanya na linakupendeza wewe unaunga mkono bila kujali taratibu za kuyafanya hayo mambo.

"Kuhamia Dodoma kuliwashinda marais wote, yeye kaweza", hili ndilo liwe kipimo cha ufanisi wa utendaji wake na mengine yote hata yale ya msingi kabisa kama ukiukwaji wa haki za watu tuyasahau?
 
uchumi2018

JF-Expert Member
Mar 4, 2018
906
1,000

Nadhani tukubaliane kwamba kila mtu ana uhuru
wa kuona anavyoona,ndo maana kila mtu Mungu amempa
macho yake binafsi na si ya pamoja.

Nikuulize yule mwandishiwa habari aliyeuwawa iringa,kwenye kampeni,ilikuwa uongozi huu?
na kama siyo huu je hapo demokrasia ilitumika? Na je kama haikutumika
nipe mfano mmoja wa maendeleo yanayoitikisa Tanzania yaliyofanyika kipindi
hicho ambacho kwa macho yako unaona demokrasia ilitamalaki.
 
Sasa unaniuliza maswali ya kijinga. Ni wapi niliposifu alipouawa mwandishi wa Iringa au kiongozi aliyesababisha mauaji hayo?
Hivi unaelewa tunachozungumzia hapa.

Haijalishi ni kiongozi yupi anafanya mambo hayo mabaya. Kama yapo yatapingwa na kama anafanya mengine kama hayo unayoyasifia wewe, bado hatutaweza kusifu hayo mavitu mazuri anayojenga huku akiendelea kukandamiza anaowajengea mavitu hayo.
.
Hitaji kuu kushinda yote ni haki kwa kila raia kwanza, mengine yanafuata.

Hivi unajua maana ya "maendeleo"?

Unapoondoa haki hiyo, ni upuuzi kumhadaa kwa vitu vitamu huku ukiendelea ukimnyanyasa.
 
utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Aug 19, 2017
2,577
2,000
Una pepo la chuki, kaombewe!!
kwetu hivi tu
IMG_20190723_203502.jpg
 
Kweyunga

Member
Dec 28, 2009
17
45
Sielewi kama ni usahaulifu, Kujali kuliko pitiliza au yakeyale. Kweli Kuna mtu yeyote kutoka upinzani au mwenye Kujali demokrasia, Uhuru wa maoni, mawazo na kujieleza anasikitika kwa Vijana watatu hawa kuondolewa serikalini? Au ni ile chuki dhidi ya Magufuli imewatoa kumbukumbu na ufahamu?

Mwanakijiji umezeeka? Umelogwa? Umepuuza akili na ufahamu wako? Umekula maharagwe? Au nini kimekusibu?!!!!

Sikuwahi kukuhisia kuwa siku moja unaweza kufikiri kwa uduni namna hii, udhaifu huu umeutoa wapi, my role model analysit?

Ni kweli unaamini upinzani ni kuunga mkono na kufurahia unyanyaswaji na ukandamizaji wa watu ili mradi tu wale watu wamewahi kuwa kinyume au kukutendea vibaya? Mzee Mwanakijiji, ndivyo ufikiriavyo namna hiyo? Kwamba Nape kushikiwa bastola mchana kweupe, upinzani (Mzee Mbowe) uibuke na kusema ua kabisa huyo? Kweli? Kwamba upinzani ni kuwa wakitukanwa na kudhalilishwa watu useme hata kupiga pigeni tu hao maana sisi ni upinzani hatuwapendi? Kwamba upinzani kwa kuwa ulipigia kelele rushwa, mikataba ya wizi basi mtu akiamka asubuhi akaita gazeti na waandishi na kutangaza Mwanakijiji ni mla rushwa basi ukamatwe na kuwekwa lokapu au leo mtu akisimama akasema nafuta mkataba wa hii kampuni na biashara zake nataifisha bila kufata taratibu na sheria basi upinzani upige makofi na kushangilia?

Mzee Mwanakijiji!! Kwani miaka imeenda umeshazeeka sana? Nini kimekusibu katika fikra zako pevu?

Bado naendelea kuwaza..... bado nawaza tena na napatwa hisia pengine ni Mwanakijiji mwingine sio yule ninayemfahamu.... bado nawaza, kweli ni yuleyule Mwanakijiji?
 
Kama ufikiri huu ndio ufikiri wa wana-CCM, wanasiasa, vyombo vya dola, vyama vya siasa, imani/dini, jamii n.k. basi ni hatari kwa nchi yetu. Kwamba akiumizwa asiyekuwa wa upande wako au aliyekutendea au kukusema vibaya, akikandamizwa akatendewa isivyo haki basi ufurahie na kumuombea shari zaidi.....!!!

Kazi tunayo mzee mwanakijiji.... hakika leo umenipa fursa ya kuwaza!🤔🤔🤔
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,669
2,000
Ndio hapo utajua wafuasi wa vyama vya upinzani Tz ni wa hovyo kupitiliza, yule yule aliezima Bunge live leo anaonewa huruma na wapinzani kwa kukosa uwazili, kisa hapatani na Magu,yule yule aliyeleta sheria ya mitandaoni wapinzani wakalia lia kumbe walikuwa wanafki leo eti wanamtetea yule yule aliyefurushwa awaziri eti kaonewa, pamoja na kumtuhumu ya kwamba ndiye aliyefunga goli la mkono leo wanamhurumia kupoteza uwaziri. Upinzani wa awamu hii ni wahovyo haijawahi kutokea.Ndio maana mm nasema nimfuasi sugu wa Magu na Musiba.
Hujui siasa,Siasa haina adui wala rafiki wa kudumu!Cha msingi unaangalia fursa,mgongano ndani ya ccm ni fursa kwa wapinzani kuchomekea kuni ili moto uwake na wavurugane,hiyo ndiyo siasa!Siasa sio amri kumi za Mungu!!!!
Wabongo sijui tunakwama wapi?Hata kuelewa siasa napo tabu!!!!!

Huyo huyo JPM mwenyewe wakati mwingine anakula maneno yake na kubadilika!!!Angalia hizi-
1.Serikali yangu sitateua wapinzani!!!Je,anefanye hivyo?????
2.Nikitoka chato nitatoa salary slip,miaka imeshakata toka atoe kauli hii akiwa chato!!
3.Nitatoa milioni 50 kila kijiji,sasa tunaambiwa hakusema hivyo bali huduma za elimu na afya ndio zinafidiana humo humo kwenye hiyo 50m.
4.Changia wahanga wa tetemeko,zikachangwa na serikali ikazitaifisha!!!
Kiufupi siasa sio msahafu!!!
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,152
2,000
Sielewi kama ni usahaulifu, Kujali kuliko pitiliza au yakeyale. Kweli Kuna mtu yeyote kutoka upinzani au mwenye Kujali demokrasia, Uhuru wa maoni, mawazo na kujieleza anasikitika kwa Vijana watatu hawa kuondolewa serikalini? Au ni ile chuki dhidi ya Magufuli imewatoa kumbukumbu na ufahamu?
Mzee unajitoa ufahamu, human nature adui wa adui yangu ni rafiki yangu!
 
Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
13,669
2,000
Sielewi kama ni usahaulifu, Kujali kuliko pitiliza au yakeyale. Kweli Kuna mtu yeyote kutoka upinzani au mwenye Kujali demokrasia, Uhuru wa maoni, mawazo na kujieleza anasikitika kwa Vijana watatu hawa kuondolewa serikalini? Au ni ile chuki dhidi ya Magufuli imewatoa kumbukumbu na ufahamu?
Kwani hao ndio wameminya demokrasia na uhuru wa maoni?Tunajua source ni nani na hao ni spika tu kutufikishia!

Hongera kwa kukiri kuwa Tz kuna uminywaji wa demokrasia na uhuru wa maoni!
 
nkuwi

JF-Expert Member
Feb 11, 2013
4,152
2,000
Marehemu Mandela aliwahi kusema, 'kama ubaguzi wa rangi wa mzungu dhidi ya mtu mweusi haukuwa mzuri, na tuliupinga, basi pia ubaguzi wa mtu mweusi dhidi ya mzungu hauwezi kuwa mzuri, nao tutaupinga'.

Kama tuliuchukia ubaguzi, uonevu, wizi wa kura (goli la mkono) na dhuluma iliyokuwa ikifanywa na vijana hao watatu dhidi ya wapinzani, basi pia hatutaunga mkono uovu huo huo ukifanywa dhidi ya hawa waovu wa zamani.

Kama tunavyopinga leo uonevu na uvunjifu wa haki za binadamu unaofanywa na JPM dhidi ya wapinzani, pia tutapinga uonevu wa namna hiyo hiyo dhidi yake kwa siku zajazo atakapokuwa nje ya madaraka.
Kwa ufafanuzi huu asipoelewa Bora tuu huyu Mzee Mungu amtwaeee tuu! Ameni
 
Proved

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,893
2,000
Sie wakongwe wa hapa JF tunakumbuka jinsi ulivyokuwa unahangaika baada ya kuuawa yule mtangazaji wa Channel 10, Daudi Mwangosi! Binafsi bado nakumbuka ulivyokuwa unaleta habari za US Senate kuhusu suala lile! Bado nakumbuka ulivyokuwa kwenye timu ya kubandika magazeti US kuonesha yaliyomkuta Daudi Mwangosi na kuitaka US ichukue hatua!!
Huyu Mzee alishaamua kuunga mkono juhudi na kusahau yaliyopita! ila kuhusu hao vijana namuunga mkono hao vijana wanastahili kupitia hayo wamevuna walichopanda.
 
myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,623
2,000
Hao vijana waliota mapembe wakajiona wamefika angalau wamekumbushwa hawana hati miliki ya vyeo.
Mimi sioni cha ajabu kutoka kwa hao vijana kwa sababu, for what I know, nothing personal! Wapo CCM, na walikuwa wanaipigania CCM, so again, nothing personal, it's all about politics! Kama ambavyo sisi tunavyoita ma-FISICM! It's politics, na ukiona mtu anakuja juu kwa kuitwa ma-FISICM, basi huyo ni mgeni wa siasa!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom