Swali: Bunge Kuahirishwa leo?

Swali: Bunge Kuahirishwa leo?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,788
Bunge ni mhimhli mmojawapo kati ya mihimili mitatu ya dola, wenyewe ukiwa wa kumhusisha zaidi Mwananchi kupitia kwa Mbunge wake.

Wote tunajua yaliyotokea Arusha kuwa ni Mauaji makubwa na ya kusikitisha kwa raia wasio na hatia, waliokusanyika kwa mujibu wa katiba yetu, na kwa kutimiza misingi na haki ya kidemokrasia ya kukusanyika kufanya siasa.

Ninachouliza ni kwamba Je Bunge letu leo hii litaendelea, ikiwa ni siku yake ya kwanza kuonana tokea tendo hili la kinyama kufanywa na magaidi?

Je Bunge litaahirishwa kama ilivyokea huko Mtwara mwezi wa tano wakati wa kadhia ya gesi, ambapo pia kama ilivyo Arusha watu kadiri ya watatu waliuawa.

Maoni Yangu:
Kama Spika na wasaidizi wake wametambua kuwa Demokrasia ya Mtanzania na ya Vyama vingi imesiginwa kwa tukio la Arusha, basi wataahirisha Bunge japo kwa leo, bila kujali kama wataunda tume yoyote.
 
mkuu jiulize,hilo bomu lingelipuka kwenye mkutano wa ccm ingekuweje???
wangehisi muhusika ni nani??
 
mkuu jiulize,hilo bomu lingelipuka kwenye mkutano wa ccm ingekuweje???
wangehisi muhusika ni nani??
Mkuu Marire
Serikali yote ingehamia kwenye tukio na kutoa kauli za kila aina, na ofcourse FBI wangeletwa kuchora mchoro wa mhusika.

Msajili pia angeifuta kama si kuisimamisha kwa miaka mitatu cdm.

Machalii wa Arusha huwa wanasema ...Mungu Hanywi Chai! , wakimaanisha Mungu hana upendeleo au yeye siye Athumani, maana aliamua kuwadhalilisha kabla hata ya jua kuzama.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom