Swali:Biashara ya Mahindi Kiteto

haa mym

JF-Expert Member
Jul 7, 2014
4,829
4,612
Habarini wana jamvi?
Natumai mu wazima wa afya. Wadau wa jukwaa hili ninahitaji ushauri wenu kidogo kuhusu biashara ya Mahindi huko kiteto,kuna bwana mdogo wangu mmoja kaniomba shilingi 4 million ili afanye hiyo biashara huko Kiteto kupeleka Tanga anasema faida yake kwa kila safari ni 1million sasa.
Sasa mimi wadau haya mambo ya biashara yamenipitia mbali kidogo sasa kuna ka ukweli wowote hapa kuhusu hii biashara maana mashaka yangu isije kuwa sivyo ikawa tabu kwa mimi mtoaji.

Ushauri wenu tafadhari au kama kuna fursa ingine sio mbaya ili niweze kumkwamua huyu bwana mdogo.
 
Kuna kaukweli kidogo ila sio kwa kipindi hiki, labda anunue sasa hivi kwa wingi halafu asubirie kianzia mwezi wa 10 mpka january auze hukohuko au apeleke huko Tanga, kwasasa gunia linaweza uzwa 50 huko shambani japokuwa kipindi hiki mahindi hayajapatikana sana kwasababu za mvua kidogo.
Jana nilijaribu kwenda huko kupitia turiani nikaishia njian baada ya kuona siwezi pata mzigo niliohitaji kwasasa.
 
Back
Top Bottom