Swala la kuchinja katika katiba!!!!

Swala la kuchinja katika katiba!!!!

Status
Not open for further replies.
...-KIPENGELE CHA 3 KINASEMA ".(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje yashughuli za mamlaka ya Serikali". KWA HIVI SASA SERIKALI IMEINGIA MIKATABA NA JUMUIYA ZA KIDINI KUHUSU UENDESHAJI WA HUDUMA ZA ELIMU NA AFYA. KWA MFANO KUNA MKATABA WA MWAKA 1994 MAARUFU KAMA M.O.U. KATI YA SERIKALI NA MAKANISA. SERIKALI INATUMIA KODI ZA WANANCHI HADI WA MADHEHEBU MENGINE KUYAPA MAKANISA. kwa kipengele hiki cha 3, ina maana mikataba hii haitokuepo tena!? waislamu wamekua wakilalamikaa kwa muda mrefu kuhusu serikali kuwasahau na kuingia mikataba na makanisa. labda kipengele hiki kitaleta unafuu kwa waislamu!

Umesema vyema kuwa ruzuku inatolewa kwa ajili ya Elimu na Afya. Sasa usicho elewa nini, ingekuwa inatolewa kuwalipa viongozi wa dini hapo ungekuwa na hoja. Lakini pesa hizi zinatumika kununulia madawa, vifaa tiba na kulipa madaktari wa serikali walioko kwenye hospitali za hizo, kwa sababu Serikali haijajenga hospitali katika maeneo hayo, ni lazima itoe ruzuku ili watu wake waendelee kupata huduma za matibabu. Mfano; hospitali za Bugando na KCMC inatibu wagonjwa bila kujali wala kuuliza dini ya mtu!

Kwa upande wa elimu ni za kununulia vifaa mbalimbali vya kufundishia na kuwalipa walimu wa vyuo hivyo, Mfano; SAUT inachukua wanafunzi wa dini zote, wanaosomea udaktari na unesi Bugando wanasoma wa dini zote, bado vyuo mbali mbali vya utabibu vinavyoendeshwa na madhehebu ya kikristo, wanasoma wanafunzi wa madhehebu yote. Kama mtu akiwa amevaa miwani ya mbao ndiyo anaweza kuhoji ruzuku inayotolewa kwa taasisi zinazo nufaisha wote bila kujali imani ya mtu.
 
Kuchinja nini hasaaa.. maana tukisema kuchinje kuna sehemu itapindishwa kwa sababu ua uharamu upande mwingine.....
Jitwalieni wanyama mkajifanyie kitoweo mle.....
Achinje nani? hakuna maelezo yeyote zaidi
 
Sasa likiwa la serikali, hiyo serikali ina machinjio wapi? na yenyewe haina hata kiwanda cha kusindika nyama.
hao watakao kuwa wanafanya kazi ya kuchinja watatoka kundi gani?

Watakuwa ni watumishi wa Serikali ambao kila wanachokifanya wanafanya kwa niaba ya Serikali isiyo na dini, kila kinachofanyika na serikali hakina mlengo wa kidini.
 
Nimekupata ndugu yangu, ndiyo maana wakati wa kutoa maoni nilishauri Serikali ichukue jukumu la kuchinja liwe lake ili kuondoa mgongano.
Mkuu serikali inapaswa iwe na majukumu makubwa ya kutuletea maendeleo na siyo kutuchinjia kitoweo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom