Nina wasiwasi na uelewa wako , hukusoma lipo hapa, si o lazima kila jambo liwe clearly expresed, impliedly pia inaruhusiwa, uwavyotaka wewe iwe, katiba itakua na pages zaidi ya 600, haya soma hapa , ibara ya 31.
31.
-(1) Kila mtu anao uhuru wa mawazo, imani na uchaguzikatika mambo ya imani ya dini na anao uhuru pia wa kubadilisha dini,imani yake au kutokuwa na imani na dini.(2) Kazi ya kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini itakuwani huru na jambo la hiari kwa mtu binafsi ili mradi asivunje sheria za nchi.(3) Shughuli ya uendeshaji wa jumuiya za dini itakuwa nje yashughuli za mamlaka ya Serikali.(4) Hifadhi ya haki zilizotajwa katika Ibara hii itakuwa chini yataratibu zilizowekwa na sheria ambazo ni muhimu katika jamii yakidemokrasia kwa ajili ya usalama, amani, maadili na umoja wa jamii nawa kitaifa na vitasimamiwa kwa utaratibu ulioainishwa kwenye sheria zanchi.(5) Ni marufuku kwa mtu, kikundi au taasisi ya dini kutumia uhuruwa kutangaza dini kwa kukashifu imani na dini nyingine, kujenga chuki aukuchochea vurugu na ghasia kwa madai ya kutetea imani au dini.(6) Dini na imani ya dini haitatumika kwa namna yoyoteitakayowagawa wananchi, kuleta uhasama au kuharibu amani miongonimwa wananchi.(7) Neno "dini" kama lilivyotumika katika Ibara hii litatafsiriwakwamba maana yake ni pamoja na madhehebu ya dini, na manenomengine yanayofanana au kuambatana na neno hilo nayo yatatafsiriwa
kwa maana hiyo.
haya sasa kazi kwako kuelewa