Suzuki kei

Ellie

Senior Member
Sep 2, 2011
123
15
Habari wanajamvi,wakuu naomba kuuliza kuhusu ubora wa haka ka gari kwa matumizi ya hapa town Dar..?
 
Weka picha uongeze uwigo wa kuchangia.
01w.jpg
 
Hiki kitakuwa poa. Bila shaka kina 4wheel, milango minne na injini ndogo. Lakini usije kuingia kishawishi kwenda safari ndefu ukipishana na lori utapeperushwa.
 
Hiki kitakuwa poa. Bila shaka kina 4wheel, milango minne na injini ndogo. Lakini usije kuingia kishawishi kwenda safari ndefu ukipishana na lori utapeperushwa.

Mkuu hiki ni mjini hapa ndio kina raha, kwanza kwenye foleni za hapa town mzee mafuta wala huwazi, na pia sio kwa ajili ya safari ndefu wala offroad, so ni safi sana coz kiko economical
 
Hii si baby walker?Kwanza unafahamu sipea zinapouzwa??waulize wenye suzuki wakwambie!
 
mimi ugonjwa wangu uko hapa tu, labda mniambie kama nimeigia chaka na model hizi mbili jimny na samurai zote 660CC engine capacity na zina 4wd.

suzuki-jimny-jlx-1999.jpg

Suzuki_Samurai_front_20071025.jpg
 
mimi ugonjwa wangu uko hapa tu, labda mniambie kama nimeigia chaka na model hizi mbili jimny na samurai zote 660CC engine capacity na zina 4wd.

View attachment 68935

View attachment 68936

Naamini hizo zitakuwa poa sana, maana nina Mitsubishi Pajero Mini, cc660, 4WD, 5Manual transmission, ina turbo, inaweza kwenda safari yoyote ile kwa Tanzania maana ina nguvu sana, mf Dar-Bukoba, kwenye mafuta ni very economical hadi raha, suala la mafuta wala haileti hata homa, spea zake zinapatikana sana japo ni ghari mno ila ni genuine na si za kugushi kama zilivyo zilizo nyingi za Toyota. Jimmy na Pajero mini mimi binafsi nazikubali sana.
 
raum zile za zamani au hizi model mpya zenye vvti ingine?

zote nzuri sema mi nina experience na ya zamani 1999/2000, cc 1496/1500, mimi nina miaka 2 nayo inanisaidia sana, naitumia mbeya, ila nasafiri nayo masafa; mbeya -dar-mby zaidi ya mara 15, hapa mby nasafiri sana maeneo mbalimbali, Aisee sijaona kama RAUM hii! haijawahi kuguswa na fundi kwenye injini, haijawahi kuchemka, coz miaka 2 sasa rejeta inatumia maji yaleyale ya dawa. Consuption ya mafuta ime maintain; safari ndefu 1 ltr/14-16 km, safari za mjini tu 1ltr/10-13 inategemea aina ya barabara.
 
Naamini hizo zitakuwa poa sana, maana nina Mitsubishi Pajero Mini, cc660, 4WD, 5Manual transmission, ina turbo, inaweza kwenda safari yoyote ile kwa Tanzania maana ina nguvu sana, mf Dar-Bukoba, kwenye mafuta ni very economical hadi raha, suala la mafuta wala haileti hata homa, spea zake zinapatikana sana japo ni ghari mno ila ni genuine na si za kugushi kama zilivyo zilizo nyingi za Toyota. Jimmy na Pajero mini mimi binafsi nazikubali sana.

asante kwa ushauri kuhus pajero mini
 
mimi ugonjwa wangu uko hapa tu, labda mniambie kama nimeigia chaka na model hizi mbili jimny na samurai zote 660CC engine capacity na zina 4wd.

View attachment 68935

View attachment 68936

Hizi gari makini sana kwa misele ya town. Wese huna hata haja ya kwenda petrol station. Hata ikinusa tu harufuu ya petrol unakanyaga unasepa. Jimny naona ziko makini zaidi ingawa bei zake ziko ghorofani.
Hiyo Suzuki mdau ni gari poa sana nayo. Suzuki Kei najua ina tatizo la apetite mbovu inapokuja suala la wese. Haili kabisa wese. Ukiipata chukua aisee.
Acha uoga wa spare parts. Kariakoo zimejaa za kumwaga. Maisha ya sasa asikuogopeshe mtu kabisa suala la spares. Zinaweza zikawa na bei juu kidoooogo sana lakini sio kukosekana.
Gari ni matunzo tu. Uendeshaji wako unaweza usiwe sawa na wangu lakini utunzaji wa gari ndio utakaotofautisha gari zetu hata kama tumenunua siku moja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom