Suzuki Grand Vitara ya 2001(2000cc 16v) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Suzuki Grand Vitara ya 2001(2000cc 16v)

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Hebrew, Jul 18, 2012.

 1. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Make:Suzuki
  Model: Grand Vitara or ESCUDO
  Year: 2001
  Engine size: 1998cc, 16v
  Fuel: Petrol
  Transmission: Manual
  Door: 5
  Mileage: 83,000 Miles
  Bei: 18M

  Hii gari imetoka UK na nipo kwenye njia za kuitoa.

  Kila kitu kinafanya kazi kama kinavyotakiwa. Nimeongeza rear metal bumper nyuma, bull bar ya mbele na spotlights.
  Nimendesha RAV4 (Manual na Auto) na kwa mtazamo wangu Grand Vitara ni nzuri sana kwenye barabara mbaya - 4WD yake ina nguvu kuishinda Rav4 na ni ngumu zaidi ila kwenye barabara nzuri Rav4 inaongoza. Kwa wale wa mikoani hii inafaa sana.

  Kutokana na kodi kuwa kubwa - TRA etc, naanza na bei hiYo hapo juu. Ni PM kama upo serious -

  SPECS:

  ABS, Adjustable seats, Adjustable steering column/wheel, Air conditioning, Alloy wheels, Anti theft system, Body kit, CD, Child locks, Cloth upholstery, Colour coding - Body, Colour coding - Interior, Driver airbag, Electric mirrors, Electric windows, Head restraints, Folding rear seats, Limited slip differential, Locking wheel nuts, Lumbar support, Immobiliser, Metallic paintwork, Part Service History, Passenger airbag, Power assisted steering, Radio, Roof rails, Radio/CD, Rear headrests, Sunblind, Audio remote control, Body coloured bumpers, Front electric windows, Front head restraints, Height adjustable drivers seat, Rear wiper, Remote central locking, Alarm, Rear electric windows.
   

  Attached Files:

 2. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  Gari imetoka.
  Wakuu hii bei ipo juu au?
   
 3. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #3
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  peleka show room
   
 4. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Bei haiko Juu mkuu, Nimecheki kodi ya hiyo gari tu ni 10,998,223.... Tuseme aliinunua #1,000 (pounds) akasafirisha mpaka port kwa 200 (pounds), akaipandisha melini kwa 850 (1000+200+850=2050)
  Sasa 2050*2540=5,207,000....
  5,207,000+10,998,223=16,205,223 Hiyo ni gharama ya CIF na Kodi.... Haya amelipa shipping line na port charges... Say laki 3 tu...inakuja 16.5, kamlipa clearing agent laki2 16.7m.... So roughly anategemea profit kidogo... kwahiyo kwa 18m na ukizingatia katumia muda zaidi ya mwezi kuitafuta (kuna mtu amepiga simu, na kaenda kuiangalia-hapo lazima phone top up na usafiri ulitumika...) na mpaka kuifikisha hapa... lazima hiyo bei iwe very reasonable...
  NB: My Assumptions are based on FOB price of 1000 remember... anaweza kuwa amenunua zaidi ya hapo...

  Ningekuwa mimi ningekomaa na 19... 18 naona ndogo sana... Investment ya almost 17m ikileta 1m kwa mwezi ni hasara tupu...
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,169
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Hem na miimi nishushie bei ya TOYOTA VISTA ya acha ile family size no no ile sedan!
   
 6. COURTESY

  COURTESY JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 2,018
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  gari nzuri,bei iko poa,mi nina 15m cash on hand,naweza pata?
   
 7. Hebrew

  Hebrew JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 3, 2008
  Messages: 509
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45

  Mkuu nashukuru kwa hili. Kwa kweli ushuru ulikuwa mkubwa sana ni nearly 90% ya bei yao/customs value + CIF not FOB. Tunalipa Insurance 1.5% ya bei yao + Freight - hivyo 15M hailipili kabisa COURTESY - itakuwa kama nimekupa zawadi na pesa juu!!

  19 - 20M naona ndio bei zake
   
 8. Doltyne

  Doltyne JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 443
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Dah Mkuu sasa Kila mtu nikianza kumshushia bei za kodi hapa.... si kila mtu atanipm nimpe bei atakazo lipa... Halaf nikikosea akaenda TRA wakamwambia bei nyingine, Ntakuwa nabeba mzigo wa lawama za bure...
  Ngoja tu nikueleze ni jinsi gani unaweza kuzipata na kukokotoa mwenyewe, ili kila asiyefahamu ajue...
  Unatakiwa kuingia kwenye website ya TRA, kisha kwenye homepage katikati ya hiyo page kuna links mbili
  Ziimeandikwa

  *Download Retail Selling Price(RSP) List
  *Download Valuation Calculator For Used Motor Vehicles

  Download hizo mbili kwenye computer yako, kisha fungua hiyo ya Retail Selling Price.... Tafuta Aina ya gari unayotaka... Copy Bei yake (Retail Selling Price) kulingana na mwaka iliyotengenezwa...(hapa kuna tofauti kidogo, sio kila gari imekuwa listed na mwaka wake wa kutengenezwa)
  Ukishacopy au kuandika pembeni bei ya mauzo, then fungua hiyo link ya pili ya Valuation Calculator For used Motor vehicles, Juu kabisa kuna Exchange rate mf: 1580, Ibadili iwe ya siku hiyo kama unaijua... kama huijui weka tu 1600.... Kisha angalia jedwali la kwanza kushoto limeandikwa depreciation for direct imports, then ukishajua gari unayoagiza ina depreciate asilimia ngapi.. Nenda chini kwenye majendwali mengine (yanajieleza vizuri tu na mifano wameweka) halafu ingiza ile bei uliyocopy kutoka kwenye lile file la kwanza ulilodownload na kujua retail selling price, kisha ingiza depreciation percentage (mf 50%), halafu bonyeza enter, Kikokotoo kitafanya kazi na kukwambia total Taxes in Tsh... Hapo utakuwa umejua ni kiasi gani utatakiwa kulipa, hata kama kitazidi au kupungua haitokuwa kwa tofauti kubwa sana....
  Then kuna gharama ya clearing agent.... roughly ni Laki Mbili, sijui kama kuna cheaper than that...Pia kuna gharama ya shipping line na port charges hizi sio kubwa sana kwa magari madogo hazifiki dola 300 kwa usoefu wangu...(NB: Kama Halina Storage Bill)
  Hapo nadhani umeelewa... Kama hujaelewa... Kwenye ile website ya TRA kuna maelezo mazuri sana ya jinsi ya kucalculate bei ya kodi na tozo mbali mbali za kuingizia vitu nchini... Ukipitia hapo utaelewa...

  Nadhani nimejaribu kutoa maelezo ya kutosha kidogo...
   
Loading...