SUV vs Double Cabin

KndNo1

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
627
2,025
Ulikuwa kwenye gari ndogo sedan.. Sasa unataka uhamie gari kubwa.. Kuna hizo options.

SUV na Dual Cab..
Fortuner vs HiLux..!
Yote ni magari ya juu kwahiyo hakuna kuhofia ground clearance..

Bei na Size
SUV bei inakuwa juu zaidi.. Hii ni kuanzia kiwandani hadi kwenye kodi TRA. Fortuner ya mwaka sawa na HiLux.. Engine moja na HiLux.. Utalipa kodi 15M zaidi.

Double cabin inakuwa na size kubwa kuliko counterpart SUV.. HiLux ni ndefu kwa nusu mita kuliko Fortuner.. Inasababisha usumbufu kwenye parking mjini..! Hata handling kwenye tight space inakuwa sio nzuri.

Comfortablity
SUV ni comfortable zaidi ya Double cabin.. Hii ni kutokana na setup ya rear suspension.. Double Cabin suspension zimekuwa designed kubeba mzigo.. Gari ikiwa tupu ride itakuwa bumpy bumpy.. Rahisi kukwama.. Pia HiLux inatumia Leaf suspension nyuma wakati Fortuner ina Coil. Pia siti za katikati kwenye Double Cabin hazina nafasi kubwa kama kwenye SUV.. Miguu itajikunja zaidi..!

Nafasi ya Watu na Mizigo
Hapa kila moja ina faida yake.. SUV seat mpaka watu 7..Dual Cab watu 5. Kwenye mizigo dual cab anabeba zaidi kuliko SUV..! Pia mizigo inakuwa separated na cabin hivyo kuongeza usalama kwa abiria.

Mengineyo
Dual Cab inakuja na options nyingi zaidi za engines kuliko SUV. Maana kuna wanunuzi watazitumia kama gari za mizigo na wengine kama gari za kupigia misele town.

Ukiendesha Dual Cab unanafasi kubwa ya kuonekana Handsome kuliko ukiendesha SUV.

Ford Ranger vs Ford Everest.
 
Hizo Kwa hapa bongo ziko chache Sana mkuu sio kwamba fortuner ni gari ya lakishamba hapana

Binafsi nazikubali mno, my dream car.

IMG_2330.jpg

Unyama mwingi sana


IMG_2331.jpg


Kuna watu wanaishi Bwana.
 
Ila double cabin kama Volkswagen amarok au ford ranger na nissan Navara ni vyuma vya maana Sana kuliko akina Prado au fortuner
Inategemea una prefer nini. Kama ni mtu wa kazi kama mm hapa na prefer Hilux D4D ama Toyota Fortuner kuliko hizo gari nyingine.
Ukipata Hilux 3.0 1kd Manual diesel ni gari ya uhakika kabisa.
Haina mambo mengi
 
Back
Top Bottom