Ndugu wana JF wakati JK anafanya kampeni za urais mwaka 2005 nilivutiwa na mwonekano wake pamoja na kauli mbiu yake ya maisha bora kwa kila mtanzania. Nilikuwa na imani kubwa na ile kauli mbiu japo kisera Mbowe alionekana kumzidi JK namna ya kuzinadi. Ni mtangulizi wake Mkapa ndiye aliyenishawishi kumuunga mkono JK hii ni kutokana na mambo mengi mazuri aliyoyafanya Mkapa ktk uongozi wake.
*wakati mkapa anaingia madarakani nchi ilikuwa na madeni mengi ya nje na ndani, alijitahidi akalipa na mengine akasamehewa hivyo mpaka anaondoka madarakani aliiacha nchi ikiwa na ziada (surplus) hazina.Tofauti na kipindi cha JK ambapo deni limeongezeka takribani 30%.
*Zaidi ya hapo elimu ya juu ilikuwa ni bure kwa yeyote bila ubaguzi kwa tajiri na maskini, equivalent na mature age wote walikuwa na haki sawa na fani zote zilikuwa na fursa sawa ilimladi tu mtu uwe umefauru kuingia chuo.Tofauti na kipindi hiki cha Jk ambapo elimu hiyo imekuwa ya kulipia kwa mfumo wa mikopo ambayo pia inawabagua equivalent na mature age ambao wengi wao ni watoto kutoka familia duni ambao mara nyingi wamekuwa wakitumia njia hizi mbili kutokana na hali zao za maisha kuwalazimu kufanya hivyo. Kwa namna nyingine hii inatoa tafsiri kuwa watoto wa maskini hawana haki ya kupata elimu ya juu.alibuni miradi yenye kufufua uchumi kama bomba la maji la kahama, kudhibiti mfumuko wa bei,aliipandisha thamani pesa yetu 1$=1000tsh tofauti na sasa ambapo Mtego aliowekewa JK ulikuwa mkubwa mno,jiulize kwa nini Sekretariat ya ccm ya NEC YOTE ILIJITENGA KUFANYA KAZI NA JK?