Suruali mpya.

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,608
1,743
Siku zile za zamani zilipoanza kungia suruali huko kwetu, alitokea jamaa mmoja wa shamba akaenda kushonesha suruali mbili. Siku aliyokwenda kuzichukua, bahati akaikuta moja na moja ilikuwa bado haijashonwa na hivyo akalazimika kuchukua hio ili nyengine aje aichukue siku nyengine atakayo kuja mjini.

Akatoka kuelekea zake nyumbani lakini hamu yake ilikuwa apate sehemu yenye kichaka hivi ili aivae kabisa ili akifika kwao awe tayari anayo. Basi akafika sehemu kichakani akajitia na kuivaa ile suruali huku lungi lake akidhani analiweka mabegani. Mara ikatokea gari iendayo kwao na akatoka kichakani kwa haraka sana ili awahi kuisimamisha na kuikimbilia. Mara alipoingia garini, watu wakaanza kucheka. Akifikiri wale watu wanafurahia kwamba kavaa suruali, yeye ikamtoka tu " hata bado, moja iko kwa fundi haijamaliza"

Kumbe wale jamaa wakimcheka kwani ile suruali aliivaa mguu mmoja tu na mmoja alikuwa kaupachika begani badala ya lungi.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom