Sura za watu wa arusha..

Sura za watu wa arusha..

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,977
Reaction score
37,879
Makonda wa mabasi yaendayo mikoani ubungo huwa wananifurahisha kitu kimoja, unapokuwa unapita mitaa hiyo hapo ubungo halafu wakakustukia kama ni msafiri vile, basi mtu atakufuata huku akikwambia kuhusu kuwepo kwa usafiri wa mabasi ya kwenda mkoa fulani, jamaa huwa hawakosei, kama wewe umetoka Arusha utaambiwa, kaka Arusha Buku 30, kama umetoka Iringa utaambiwa kuna gari ya Iringa, na kama ni wa Mwanza utaambiwa hii kaka/dada/mama/ babu/bibi gari ya Mwanza hapa n.k..Mimi ni shuhuda wa jambo hili, kwetu ni Arusha, kila ninapopita hapo Ubungo lazima niambiwe kaka gari ya Arusha ipo, sio mimi tu zaidi ya rafiki zangu watatu ambao wanatoka arusha wameshaambiwa kitu kama hicho, achilia mbali wa mwanza, mbeya, dodoma nakadhalika, swali hivi hawa makonda huwa wanajuaje kuwa mtu fulani anatoka sehemu fulani kwa kumuangalia tu?
 
watu wa arusha wana swagga zao bana sio mameen au malady wanavo vaa na appearance lugha na kadhalika
 
watu wa arusha wana swagga zao bana sio mameen au malady wanavo vaa na appearance lugha na kadhalika

wala utumbo wana swagga gani nivea? ulinichekesha siku ile.
 
kila wakazi wa sehemu fulani wana tabai zao ambazo inaweza kuwa rahisi kwa mtu aliewazoea kuwajua, kwa watu wa kaskazini wanajulikana kwa itikadi zao ambazo hata kwenye mavazi, lafuzi etc utawajua tu..
 
wala utumbo wana swagga gani nivea? Ulinichekesha siku ile.

hahahahaah unakumbukumbu kweli hahahahahah hawa wala utumbo wa kuku hapa mjini swaga zao hazisomeki njaa kali.pale ubungo wanacheki mabegi lafudhi na swagga .unafikiri ukifika pale watu wa kigoma utawajua wana ile mifuko ya asante shangazi ya nailoni wameweka mawese na asali na mamizigo meeeengi ,hahahahah
 
kila wakazi wa sehemu fulani wana tabai zao ambazo inaweza kuwa rahisi kwa mtu aliewazoea kuwajua, kwa watu wa kaskazini wanajulikana kwa itikadi zao ambazo hata kwenye kimavazi, lafuzi etc utawajua tu..

heri ya mwakampya lakini
 
Wa Arusha ni easy sana kuwa recognized kwanza meno,pili dress code yenu bana masweta hadi dsm lol
 
Uzoefu kazini unawasaidia kumsoma msafiri kwamba huyu anatoka kule au anakwenda kule
 
Kutambua Watu;
Wa Arusha - hupendelea kusafiri na wake/wapenzi zao
Wa Mwanza - Hubeba mizigo mingi
Wa Iringa - Baba hutangulia mbele mama hufuata nyuma ie single file
Wa Moro - Huwa hawana mzigo wowote zaidi ya mkoba mdogo
Wa Mbeya - Husindikizwa na ndugu wengi wakati wa safari n.k
 
hahahahaah unakumbukumbu kweli hahahahahah hawa wala utumbo wa kuku hapa mjini swaga zao hazisomeki njaa kali.pale ubungo wanacheki mabegi lafudhi na swagga .unafikiri ukifika pale watu wa kigoma utawajua wana ile mifuko ya asante shangazi ya nailoni wameweka mawese na asali na mamizigo meeeengi ,hahahahah

hehehe ngoja wakusikie uone, heri ya mwaka mupya pia
 
Ebwana hiyo kweli, jamaa wabaya wale ... huwa wanakosea mara moja na si zaidi ...
 
Wa Arusha ni easy sana kuwa recognized kwanza meno,pili dress code yenu bana masweta hadi dsm lol

lol, hata nyie vijana wa dar ni rahisi sana kuwajua, unakuta mtoto wa kiume kavaa pedo ya pinki,red.. nywele kaipika inameremeta, tshirt imeishia kwenye mkanda, miwani nyeusi hadi gizani, mfukoni kabakiza shilingi 100 ya maji ya kandoro.. yani ni zaidi ya hatari..
 
Kwa hiyo watu wa Arusha hawaendi Dodoma hata siku moja?
 
hahahahaah unakumbukumbu kweli hahahahahah hawa wala utumbo wa kuku hapa mjini swaga zao hazisomeki njaa kali.pale ubungo wanacheki mabegi lafudhi na swagga .unafikiri ukifika pale watu wa kigoma utawajua wana ile mifuko ya asante shangazi ya nailoni wameweka mawese na asali na mamizigo meeeengi ,hahahahah

Ha haaa,yaan umenichesha jamani!khaa,eti mfuko wa asante shangazi
 
Kutambua Watu;
Wa Arusha - hupendelea kusafiri na wake/wapenzi zao
Wa Mwanza - Hubeba mizigo mingi
Wa Iringa - Baba hutangulia mbele mama hufuata nyuma ie single file
Wa Moro - Huwa hawana mzigo wowote zaidi ya mkoba mdogo
Wa Mbeya - Husindikizwa na ndugu wengi wakati wa safari n.k

Hiyo ya Wa Iringa Kiboko! Sijaona wafuatao:

Tanga
Mtwara
Songea
Dodoma

Utawatambuaje?
 
wa arusha ni easy sana kuwa recognized kwanza meno,pili dress code yenu bana masweta hadi dsm lol

ina maana wanatembea wakicheka na kuongea hata wakiwa peke yao? Muuliza swali aliuliza kwamba ukipita wanajuaje kwa kuangalia tu sura? Halafu ukisema sweta unaongeza chumvi. Dar ndio wanaopenda sweta, hawana pa kuvalia, hivyo hulazimisha huku huku kwenye joto
 
Kutambua Watu;
Wa Arusha - hupendelea kusafiri na wake/wapenzi zao
Wa Mwanza - Hubeba mizigo mingi
Wa Iringa - Baba hutangulia mbele mama hufuata nyuma ie single file
Wa Moro - Huwa hawana mzigo wowote zaidi ya mkoba mdogo
Wa Mbeya - Husindikizwa na ndugu wengi wakati wa safari n.k

u made ma day ila,umejuaje?
 
hawa jamaa ni wazoefu wa kuangalia watu na mikoa husika ,huwa rahisi kwake kujua huyu ni iringa ,tanga ,dodoma ingawaje huwa kuna vitu vidogo huwapa utambulisho haraka kama meno ya rangi anajua huyu ni arusha au mosh,lafudhi ya lugha ,n.k
 
Ni uzoefu wa kazi tu,ni sawa na watu wanaodili na watalii kutoka nje,wakimwangalia mtalii tu,wanajua katoka nchi gani.
wanavitu vingi sana wanavyotofautisha mataifa ya wateja wao.kwamfano kuna siku dada mmoja bila kusalimiwa akaulizwa
kama anatokea Amsterdam,Rotterdam au mji gani,mwenyewe akashangaa wamejuaje kama anatoka Uholanzi.Jibu ni kwamba,viatu alivyovaa ni wadachi tu,ndo wanaovivaa wakiwa wanatembelea nchi kama za Africa.Kwa hiyo,pamoja na mambo mengine,mi naamini watu wa kutoka sehemu moja na nyingine wanatofautina sana kwa mavazi.
 
Back
Top Bottom