Sura ya Mwl. Nyerere hana macho ya Mwl. Nyerere

tangoMwitu

Member
Feb 23, 2017
74
125
Salamu wanajamvi!

Tangomwitu ni mnyonge wa mawazo na macho yake hayana uwezo wa kuona ninakotoka wala ninakokwenda lakini baada ya kashikashi nyingi za siasa za watu kuama kutoka huku kwenda kule macho yangu leo yamepata kuona.

Amefanana na mwl.Nyerere na ni jembe kwelikweli huwa na mkubari sana hawapo jukwaani akiongea maneno yake ya busara yanayoleta mijadala kwa wanaomuelewa na wasio muelewa.

Mimi mnyonge wa mawazo na macho yasiyoona leo nimeona huyu mwenye sura ya mwl Nyerere hana macho kama ya mwl Nyerere.

Macho yangu yameona jambo moja kubwa kuwa naye ni kipofu kama mimi tunataka mazuri lakini atujui jinsi ya kuyapata, tunaamini kuwa ufalme wa mbinguni utatekwa na wenye nguvu bila kujua tunayepambana naye ni mnyonge.

Ametuletea ajabu katika nchi hii nafikiri yeye ni miongoni mwa wale asilimia 80 waliotaka chama kimoja enzi za mwalimu pamoja na hao ulionao sasa awapendi vyama vingi maana nao furaha yao kuona upinzani wote kuja chama tawala.

Ni wakumbushe mwl aliyekuwa na akili Si kama huyu mnayemfananisha naye hakununua upinzani wala kuwashawishi wapinzani warudi chama tawala ila alicheza na upinzani wakiwa huko huko kwao,uchaguzi wa mwaka 1995 ungekuwa shule kwako kama ungekuwa na macho mwl. aliruhusu watu toka kwa chama chake wawe upinzani kuleta democrasia na kutuonyesha wananchi kuwa kuna upinzani.mfano ni huyu ambaye sasa tunatambua kuwa ni wakwenu lakini bado anahekima aliyoachiwa na mwl. anamuunga mkono mkuu akiwa upinzani ndg Mrema alitikisa kisiasa wananchi tukasema huu ni mwisho wa chama chenu lakini Mkuu wa kipindi hicho akununua watu kurudisha kwenu ila baada ya uchaguzi walichokifanya wakuu wa wakati ule ni kumtumia Mrema mwenyekiti wa chama chenye nguvu kuama ama chama na kuunda vyama vingine hadi NCCR ikafa na upinzani ukawa zaifu,

Kwa upande wa CUF walibaki na Lipumba akitumiwa huko huko na Siraa CDM hadi mlipowatumia kama kalata yenu uchaguzi 2015 na kuleta matokeo makubwa bila kuama vyama vyao.

Mimi nisiyenamacho nimeona nikupe macho kuwa hata mataifa makubwa wanatumia siasa za kimafia za mtindo huu kula pamoja nao wakiwa huko kwao na sisi wananchi tusio na macho tukajua kuna upinzani kamili lakini wewe pamoja na macho uliyonayo unaona watu wakijitangaza kuamia kwako ndiyo sifa kwako je vyama vyote vikiamia CCM wakiwa na akili kama za hao wanaokuunga mkono nchi itakuwa na upinzani acheni kufurahia ujinga.Nikwambie ukweli tu

Kwanza mataifa mengine watasema unataka kuua vyama vingi.

Pili wananchi wataona siasa ni maslahi binafsi si kutetea wananchi

Tatu wananchi wapenda vyama vingi ambao idadi yao uijui watakuchukia
Nakushauri kama umeshindwa kutumia mbinu za wenzako waliopita tumia za rafiki yako wa Ruanda ajanunua upinzani kwenda chama tawala lakini vyama vyote vilinunuliwa vikabaki huko na vikamuunga mkono angalau sisi wenye wenye macho mabovu na fikra dhaifu za kisiasa utatutuliza na kutuaminisha kuwa wewe ni bora lakini kwasasa kwakweli wengi wanakuombea mabaya na kwasababu wanakuogopa kwa vitisho vyako wala ahutafanikiwa kumjua mbaya wako nani.muda utaongea utakapoona ya Mugabe na wale waliokuwa wanampigia makofi.

[HASHTAG]#usiniulize[/HASHTAG] swali sijibu,tapika povu lako upite.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom