Miss Natafuta
JF-Expert Member
- Sep 16, 2015
- 26,575
- 48,726
Maza katoka kijijini kaja kunitembelea kaja na maboga ya kutosha namuonea huruma sijui alibebaje anyway am her little daughter hata kama nimezeeka vipi so hapa nimeona nipike soup ya boga.
Kula maboga sio umaskini boga ni chakula kizuri sana kwa wagonjwa ,watoto pia mahoteli makubwa wanatumia kama appetizer so nawashauri hasa watu wa dar nyie ambao chakula chenu ni mzunguko wa wali, ugali, tambi, pilau mjitahidi kuongeza na vyakula kama maboga kwenye meza zenu.
Mapishi ya soup ya boga mahitaji vipande vya boga vilivochemshwa inategemea na mpo wangapi tuseme kama nataka bakuli nne nitachukua nusu boga maziwa robo lita ukipata ile cream ya juu ya maziwa ni safi sana butter kijiko kimoja
vitunguu vile vya majani kama vinne hivi chumvi, pilipili manga.
Mapishi;
Chukua boga blend au pondaponda hadi lisagike kabisa unasweza ukasaga na tui na nazi au maji tu ukipenda weka sufuria jikoni weka mafuta kidogo sana na butter kijiko kimoja weka vitunguu vya majani baada ya kukatakata vidogodogo au hata vitunguu maji ukipenda ila vya majani ndo vizuri zaidi according to me, acha kitunguu kiive kidogo kisiungue kabisa.
Mwaga lile boga uliloliblend kwenye huo mchanganyiko wa vitunguu
koroga kwa nguvu weka chumvi, weka pilipili manga, koroga sana weka maziwa koroga sana ili yasikatike baada ya hapo acha kidogo ila koroga tu kwa muda
hapo supu yako itakuwa tayari.
Karibuni hapa nakunywa supu ya boga
Kesho nitawapikia vegetable soup