Goodluck Mshana
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 1,271
- 1,119
Leo ndani ya UDSM nikakutana na idadi kubwa ya wanafunzi. Idadi hii ilinipa mshawasha wakuuliza kulikoni! Kwani siku na tarehe yakufungua chuo bado. Kwa bahati nzuri nikakutana na baadhi ya wasomi hawa nakupata mwanya wakuuliza kinachojiri chuoni hapo. Vijana wakiwa na nyuso za kawaida sana wakanijibu walikuwa chuoni hapa kwaajili ya "kusapua". Nilipojaribu kufanya mawasiliano kwenye vyuo vingine (kikiwemo AMUCTA cha Tabora-Tawi la SAUT) nikaambiwa hali ilikuwa nizaidi ya huku Mlimani! Shida ni nini haswa wanajamvi? Je tatizo linaanzia kwa Lecturers na Professors ambao baadhi ni incompitent? Na ambao wengi kwa ugumu wa maisha wamezidi kujihusisha na shughuli nje ya vyuo? Au vijana wetu wa bongo wanaona maisha ni kama kumsukuma mlevi hivyo kupoteza umakini masomoni?