Bodi ya mikopo ya wanafunzi kwa kushirikiana na viongozi wa vyuo vikuu ilikuwa ikiiba pesa za wanafunzi hewa, walioacha masomo na hata waliofariki. Bahati mbaya hakuna hatua ya maana iliyochukuliwa.
Kuna mtindo mpya wa wizi. Vijana wetu wanapomaliza masomo na kufuatilia vyeti, huambiwa ulipokuwa mwaka wa kwanza hukulipa ada hii au gharama ile. Mtindo huu umekomaa vyuo vyote, binafsi nimeshawalipia vijana wawili Chuo Kikuu cha Kilimo, SUA na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM baada ya kudaiwa na ofisi ya uhasibu, ada za miaka mitatu iliyopita. Niliamini enzi hizi za kompyuta vyuo vinatunza kumbukumbu zake. Naiona hii ni makusudi. Kwa nini wadaiwe wote ada ya miaka mitatu iliyopita? Wengi wanalipishwa kwa mara ya pili kwa makusudi kabisa kwa madai kwamba chuo hakioni kumbukumbu.
Waziri wa Elimu bahati mbaya wewe umetokea chuoni. Yaonekana una urafiki binafsi na hawa maprofesa wenzako. Tunaomba uviangalie upya vyuo vikuu hivi. Siyo wasafi kama unavyoonesha. Bado wanaangaika kuwaibia wanafunzi na sisi wazazi tunaolipa ada hizo.