Supermarket hii inauza unga uliooza

Supermarket hii inauza unga uliooza

tuwe makini ktk hili sio unga tu vitu vingi sana ikiwepo vinywaji
 
Ndugu zangu hizo Expire Date hazina maana. Watu wanajitengenezea mapochopocho yao, wanachonga mihuri yao na kubandika kwamba bidhaa zinamalizika muda mwaka 2015. nani amezithibitisha? Ninachoweza kusema ni kwamba hii post ina ukweli mtupu. Supermarket hii ipo pale Vetenary katika Kituo cha mafuta cha Oilcom. Mimi niliwahi kununua maziwa yanaitwa DAIMA nadhani yanatoka Uganda. Hayana ubora wala ladha yoyote ya maziwa. naomba sana watu wa TFDA waitupie macho. Haya madai kuwa wanafumbia macho kwasababu ya rushwa yanawavua nguo!
 
YangekUWA YA TZ NINGEKUJIBU YA UGANDA LOH ENDELEA KUHARISHA MPAKA UTAKAPOONJA YETu
 
tatizo watoto watasoma shule gani? si unajua jinsi hizi Mamlaka aka AUTHORITIES zinavyojua jukulipa vzr, watoto watahama FEDHA kwenda Kayumba................. zoezi gumu hilo

wanatumia kodi za watanzania waamie tu kayumba kwa sababu wapo tayari kuharibu afya za watanzania walipa kodi ambao ndio wanaowalisha kupitia kodi zao tukiwa wagonjwa huko kulipana vizuri watakupata wapi,?.... akili za baadhi ya watanzania upeo wao wa kufikiri ni mdogo sana any way..., wanatakiwa wafanye kazi,.... na kuna hii nyingine inaitwa OSHA nahisi hawa TFDA wameshawazika siku nyingi...
 
Watu wengi wanaamini kuwa katika Supermarkets kunauzwa vyakula vyenye ubora. Hata hivyo wanakosea sana.
Katika baadhi ya maduka hayo makubwa kuna vyakula vibovu na vingine vinahatarisha maisha ya walaji.
Majuzi mimi mwenyewe nilinunua unga unaoitwa Bora wa Lishe katika supermarket moja iliyoko Vertenary katika kituo cha Mafuta cha Oilcom na nilipofika nyumbani niligundua kuwa unga huo una wadudu weusi.
Niliwapa unga huo unaozalishwa na kampuni ya Fortune Foods Products ili wachukue hatua. Niliambiwa kuwa kampuni hiyo haina kibali kwavile ilikosa sifa. Lakini imeruhusiwa kinyemela iuze bidhaa zake. Swali hapa ni kwamba hivi tuna sheria inayoruhusu mtu asiye na vibali vya TFDA au TBS kuuza bidhaa zake kwenye Supermarkets?
Kama jibu ni hapana, hao wanaoitwa wakaguzi wa idara hizo mbili za kulinda maisha ya mlaji, wanafanyia ukaguzi wao wapi?
Watu wamekua hawaangali ubora bali wanadhamini fedha na kutaharisha afya za watu. TFDA na wauzaji wa vyakula hivi wanatakiwa kuwa makini na bidhaa wanazoziuza na kutoweka stock kwa wingi na pia waangalie muda wa vyakula hivi maana ni hatari.
 
we nawe kila kitu ni chadema, hata ukiachwa na mkeo /mmeo utasubiri chadema ishike dola ndo ikurudishie....
..afu DORA si ni jina la msichana au ulitaka kumaanisha DORA ipi au yupi ambaye atashikwa na chadema??

Hapo sasa!
DORA=DOLA
 
Hiyo supermarket inauza vitu vingi tu visivyofaa. Kuna siku nilinunua keki ile kutaka kuila tu wakati nimefika home nikagundua imeoza...!
 
Lakini pia ndani ya Supermarket hiyo kuna sukari inauzwa inaitwa MO Sugar. Imefungwa kwenye mifuko ya nusu kilo na kampuni ya Mohammed Enterprises Limited. Kampuni hii inachanganya sukari aina ya White Sugar kutoka Brazil na Brown Sugar kutoka India ambazo ni maalum kwa ajili ya kutengenezea pombe tu.
Wataalam wanasema sukari hizi ni hatari kwa akina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano. Mohammed Enterprises hawana kiwanda cha sukari, lakini wameruhusiwa kufungasha sukari hii hatari kwa walaji na kuisambaza katika maduka makubwa likiwemo Oilcom Veternary.
Ndani ya supermarket hii kuna mikate inatengenezwa kienyeji na haina baraka zozote kutoka mamlaka husika ikiwemo TBS.
Hapa unaona jinsi rushwa inavyoangamiza maisha ya watanzania wengi. Maofisa wa TFDA na TBS wanakula rushwa hadi inatia aibu na
kushindwa kuchukua hatua. Hali hii mpaka lini?
 
Naomba directio vizuri wakuu,ni ya pale oilcom ubungo au ni eneo gani,tuijue vizuri
 
Ni Oilcom ya pale Vertenary Temeke karibu na Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi. Kazi kwenu!
 
Kumbe Supermarket yenyewe iko Temeke. Kama ni Temeke basi hiyo sio supermarket bali ni genge maana Temeke hakuwezi kuwa na Supermarket.
 
[Majuzi mimi mwenyewe nilinunua unga unaoitwa Bora wa Lishe katika supermarket moja iliyoko Vertenary katika kituo cha Mafuta cha Oilcom]

Hiyo hakuna majungu wala chenga, mimi pia nilinunua unga pale ulikuwa mbovu. TFDA wanakomaa na rushwa za vipodozi (Cosmetics) hawataki kukagua vyakula (Food). Vet supermarket Oil Com tunawaomba mjirekebishe la sivyo ni kuwatangaza kwenye vyombo vyote vya habari watu waache kuja kununua kwenu.[/QUOTE]

Ni kweli hiyo supermarket inauza vitu vilivyooza mimi nilinunua hapo unga ulikuwa na wadudu, mkate nao niliyonunua hapo ulikuwa umeshaweka fungus. Pia mikate yao ya brauni huwa wanaweka rangi na siyo unga halisi wa mkate.TFD mko wapi?
 
Temeke kweli hakuna Supermarket? Uchumi pale Quality Centre iko wilaya gani? Nadhani tatizo sio mahali ilipo Supermarket bali watendaji waliopo. Kuna mambo mengine mabaya yako wilaya nyingine tofauti na Temeke. Muhimu hapa tuwaombe wahusika wachukue hatua bila kujali mahali husika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom