Supermarket hii inauza unga uliooza

Supermarket hii inauza unga uliooza

mabereng'ombe

Member
Joined
Nov 22, 2013
Posts
70
Reaction score
18
Watu wengi wanaamini kuwa katika Supermarkets kunauzwa vyakula vyenye ubora. Hata hivyo wanakosea sana.
Katika baadhi ya maduka hayo makubwa kuna vyakula vibovu na vingine vinahatarisha maisha ya walaji.
Majuzi mimi mwenyewe nilinunua unga unaoitwa Bora wa Lishe katika supermarket moja iliyoko Vertenary katika kituo cha Mafuta cha Oilcom na nilipofika nyumbani niligundua kuwa unga huo una wadudu weusi.
Niliwapa unga huo unaozalishwa na kampuni ya Fortune Foods Products ili wachukue hatua. Niliambiwa kuwa kampuni hiyo haina kibali kwavile ilikosa sifa. Lakini imeruhusiwa kinyemela iuze bidhaa zake. Swali hapa ni kwamba hivi tuna sheria inayoruhusu mtu asiye na vibali vya TFDA au TBS kuuza bidhaa zake kwenye Supermarkets?
Kama jibu ni hapana, hao wanaoitwa wakaguzi wa idara hizo mbili za kulinda maisha ya mlaji, wanafanyia ukaguzi wao wapi?
 
Afya zetu ndio kitu cha thamani sana, wahusika walijue hilo. Wawe wakali kwa bidhaa za vyakula, sio kila mtu anjiuzia tu chakula na dawa kadiri aonavyo yeye. Labda sheria zenye kubana maeneo hayo ziboreshwe la sivyo maisha ya M-tz yako hatarini.
 
Hujatusaidia bado mkuu,taja jina la hiyo supermarket tuifahamu.unaogopa nini sasa?.
 
mambo yatanyooka chadema ikishika dora 2015,
 
[Majuzi mimi mwenyewe nilinunua unga unaoitwa Bora wa Lishe katika supermarket moja iliyoko Vertenary katika kituo cha Mafuta cha Oilcom] [/QUOTE]

Hiyo hakuna majungu wala chenga, mimi pia nilinunua unga pale ulikuwa mbovu. TFDA wanakomaa na rushwa za vipodozi (Cosmetics) hawataki kukagua vyakula (Food). Vet supermarket Oil Com tunawaomba mjirekebishe la sivyo ni kuwatangaza kwenye vyombo vyote vya habari watu waache kuja kununua kwenu.
 
ukiona magari magen yanakuja mtaan kwako jua kishaanza kufuka moshi.
 
mambo yatanyooka chadema ikishika dora 2015,

we nawe kila kitu ni chadema, hata ukiachwa na mkeo /mmeo utasubiri chadema ishike dola ndo ikurudishie....
..afu DORA si ni jina la msichana au ulitaka kumaanisha DORA ipi au yupi ambaye atashikwa na chadema??
 
Ametaja hiyo inaitwa Vet supermarket Oil Com

tungejuaje kama super market hiyo inaitwa vet? kwa jinsi alivyoandika andika kasema tu supermarket moja maeneo ya vertinaly...aisee bongo kubwa jaman hatuifaham yote
 
Nachoweza kusema ni kuwa tuwe macho saana tunaponunua vyakula haswa vilivyofungwa kwa uzito mkubwa yaani kuanzia 2 kgs. Walala hoi wengi tunaishia kwenye 1 kg. Bei inapoongezeka wanaochukua ni wale wenye uwezo. Hivyo, vinabakia kwenye mashelfu muda mrefu na kuharibika.
Nimewahi kununua unga wa ngano umefungwa vizuri 5kgs. nilikuwa na hamu kweli ya chapati. Mama ameanza kusonga chapati nikasikia kelele jikoni kwenda, unga umejaa mabuu nayo yanatokezea kwa sababu ya yale maji.
Nikaenda supermarkiti ingine, nikanunua Bizari chapa simba mbili. Kopo kubwa ili likae muda kidogo. Kufika home, nikakutana na wadudu wa ajabu. Ilikuwa karibu na home hivyo fasta nikarudisha pale. Nikawaona uongozi, nadhani walifikiri kuwa nasema uongo hivyo wakaenda kuleta makopo 2 kwenye ile shelfu. Mungu ni mwema yote 2 yalikuwa na wale wadudu. Wakaumbuka. Wakanibembeleza kuchukua kitu kingine mbadala. Tuwe macho, expire date isikutishe. Chunguza kabla hujaweka kingi jikoni. Rushwa hupofusha macho, na wengi huku kwetu ni vipofu sasa.
 
Kwa ujumla ukienda kunua vitu vya viwandani kuwa makini sana KWA KUSOMA EXPIRY DATE,kuna siku vimeletwa vitu nyumbani mi kuviona vna vumbi kidogo nkaamua kusafisha na taulo kwanza,nna kawaida ya kusoma hzo tarehe,LOHH!! Almost vyote vmeexpire,ama bado mwezi tu,ndo hadi kurudisha na kupewa vipya,wauzaji wanajua wanafanya makusudi KUWENI MAKINI SANA,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom