Naomba nishee ka story kangu, ila wanawake 🙌, bana nakumbuka nimemaliza chuo , sasa nilikuwa na pisi iko mwaka wa mwisho, sasa home ilikuwa ni karibu na chuo nilikomaliz kusoma n yeye ndio alikuwa anasoma hapo, kuna siku bwana nilimwambia tukutane mara moja nimuone kwasababu nilikuwa nimemmisi sana ila kwa haraka, basi tuka set saa moja na nusu usiku na eneo lilikuwa lenye ka giza flani ivi mana nae alikuaa anaelekea kuswali , basi nimetoka zangu na jamaa yangu haraka tukafika eneo pisi ikaja tukasalimiana nayo , jamaa yangu akatupa space, mara kidogo difenda hio imebeba askar magereza, ikawa inapita maeneo yale, tukashituliwa na sauti nyie mnafanya nini hapo, manzi alikuwa ashapiga hatua anataka kukimbia mimi nikatulia tu ,wale jamaa walikuwa kwenye doria, basi wakaja kutubeba mkuku mkuku. Ee si wakaanza kutuzingua mlikuwa mnafanya nin gizani, au nyie vibaka , mimi kimya , manzi hapo ni analia vibaya, kulikuwa na askari wakike 2, na kama sikosei wakiume 4 au 5 iv, sasa bana wanaume si unajua hatukandiani, wale askari 2 wakike wakaanza kunioshea mbele ya manz yangu huku gari inaelekea kituoni kwenda kutulaza, 1 Unatumia simu gani kucheki mimi nina simu ya batani ,manzi ana iphone6, wakamuuliza manz nani kakununulia hii simu akasema baba yake, maneno yakanz kutoka mwanaums gani unashindwa kumnunulia demu wako hata simu alafu wew unatumia batan , ivi hata pedi unaweza kweli?, unafanya kaz gani na unakaa na nani, miki jobless, nakaa na mzee, je anafanya kaz gan nikasem jw, wakauliza cheo nika mute , wakaanza kwahiyo mishahara imetoka ndio ukaona uje umdanganyie huyu binti , mimi kimya, leo itabidi ukalale ndani kesho baba yako aje akutoe, wakaanza tena sikia binti sikuiz hakuna mapenzi bila pesa, hakua ndoa bila pesa, manzi alikuaa analia tu, mjuba nimetulia, kiukweli wale askri wakike walitema shombo mbaya sana juu yangu, kwa akili yangu niliwaza hawa ni form 4 felia ndio mana wameingia huku wanaropoka uchafu niliumia mbaya , aisee gari ikaenda mbali sana wakaenda kutushushia mbali sana njiani , na walitaka tu kutuhangaisha tu, sasa ile nashuka tu alikuja askr mmoj wakiume aliniramba KIBAO CHA MGONGO nikagugumia tu,wakasepa zao, huku tukiwa pembezoni mwa barabara manzi analia nambembeleza huku tunatembea na ni saa 2 kwend 3, basi akaniambia nataka nirudi chuo , nikasema sawa, nikamwitia boda, nikamwambia sina nauli😅 , akasema sawa anayo, huyo akapanda na kusepa, mjuba hapa sina hela nikaanza KUTOTI, nilipash mpka home kufika saa3, pale nje kbla sijaingia ndani nakuta mshikaji wangu kumbe yeye alikimbia baada ya kuona ile difenda, akaniuliz vipi huku akicheka na kulikuwa na mwana mwingine pale, nikawaelezea wakacheka then nikasema huyu manzi kwa sumu aliyojazwa mda c mrefu naachwa, wakanipa hope oh hamna bana, badae saa 4 nikamtafuta manz nikamp pols yakaisha, ila moyoni najua soon nakula kamba, kweli bana siku ya 1,freshi 2, freshi na ya 3 nikaona kabadilika hata majibu yake nikasema hapa ndo bye, siku ya nne ilikuwa tu meet nika lambwa block mpaka leo hii sijuagi yuko wapi yule manzi, nilicheka sana na kuwaambia wana na nilipata funzo flani juu ya hawa she, ila ile sumu na zile kejeli 🙌, NIKIZIPATA nitawadharau sana hawa ubavu wa pili😏.DUMU