Mambo ndio mambo summer party watu kibao,mi mwenyewe ndio mchomanyama hakuna wali wal mchuuzi hiyo party.kwenye pamba kila mtu kajipigigilia za kufa mtu.mimi mwenyewe nimekula simpo tu kitalii zaidi tshirt na shortcombat kama kawaida yetu
watu wanazidi kuongezeka wazungu,wachina,waarabu,wahindi,waafrikayani full rojo mixer,sasa katika walioingia kuna mtoto moja wa kilatin na mashosti zake wakutoka latino wakazama,mziki ulikua unapigwa ghafla ukawa hausikiki kila mtu ndani ya garden amegeuza shingo kumwangalia huyo malaika,anayetembea kama hakanyagi,reception 5star, kaenda hewani kitwiga,kifuakipana kidogo kilichopokewa na kiuno chembamba kama nyigu halaf kimekuja kimebebwa na hips na makalio ya haja, huku chini yakisindikizwa na miguu isiyochosha kuiangalia.watu wakamsindikiza na macho mpaka walipoketi na mashosti zake
mioyo ya midume ishawawaka, ghafla kawa midomoni mwa midume karibu yote mle ndani. loh centre of attraction ishajulikana ndani ya garden,kila kidume akaanza kujitutumua mara salam, wengine wanajifanya kutoa maagizo utafikiri wadosi ili mradi awe noticed
wale waliojiona wana hadhi sawa wakajisogeza karibu na watoto wakaanza soga mara hiv mara vile ,party inaendelea wachuchu wengine wamefichwa kijohn cena u cant c me na mtoto wa kilatino
haya tumekubaliana leo ni nyamachoma na vinywaji tu! ghafla naona mdau kajitolea kuagiza pizza kwa kila group.mara mwingine akaita mcdonald kila kichwa kingsize burgers,mnawatia hasira vibosile nyie! wenye pesa zao wakaingia moja akaagiza kila meza johny mtembez na tequila,hatujakaa sawa mdau mwingine kaja na jack daniels kila kichwa loh! watu tunacheki picha tu mana si wenye msuli mdogo inabid ukae pemben tule kwa macho sasa, maana vita ndio vyapamba moto.mi na nyama zangu naona sasa zitanidodea sasa kama mambo ndio yanaenda hivi
ukaja wakati wa muziki kila mtu yupo juu anacheza, mtoto wa kilatini yupo kati nae anayarudi kwenye dancefloor ,wenye mauwezo hapo nao wanayaonyesha mambinu yao, nashtuka kumbe mtoto hayupo mbali na mimi anapocheza na mashosti zake,nikaamua kujitoa mhanga kuomba dance na mtoto walau nijisif nilicheza na mtoto wa kilatini queen of the night
kumsogelea akanipa nafasi tukaanza kushake maringo adonoadono mtu mzima nikampa mambo ya psquare yenyewe,katikati ya mziki nikamshika kiuno kisicho na mfupa ,nikaona hii namna gani nikampiga kibao cha bambataa likavibrate.akanicheki machoni sikumkawiza nikamkonyeza huku nikimalizia na killer smile,mtoto akaangalia chini,nataka nianze kurusha ndoano mziki ukaisha
nikarudi zangu kuchoma nyama nikisikitika sijamalizia gemu,mara sijakaa sawa si mtoto anakuja kutaka nyamachoma kwa mara ya kwanza,nikampatia naona haondoki,haishii kuisifia nyama yangu,mara akaanza kuuliza maswali ya kipolisi
kumbe mtoto ashamaindi namba,watu wote hawaamini imekuaje huyu ndio ampate demu
mpaka leo najiuliza huyu demu alimaindi nini kwangu,wadau naomba mnisaidie