Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho

Sumaye: Tubadili utawala wa vitisho

Kutoka kuwa premier mpaka kugombea m/kiti wa mkoa Chadema kumbuka jamaa alikuwa mgombea urais kama mara mbili na amerudi nyuma.

Hiyo siyo sababu kwani hata katika maisha huwa tuna shindwa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo. Je tukate tamaa kwa kuwa tulikuwa na maisha fulani sasa Tumefirisika hivyo tusianze upya???????


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Mkuu mstaafu ushauri wa bure, ama fanya biashara au fuga kuku. achana na siasa kwani lazima uwe mwanasiasa mpaka mwisho?kubali yaishe ukweli ni kwamba umefilisika kisiasa.
wewe umepotoka hizi nondo anazozitoa ndio wakati wake sasa kaa pembeni kama ujui siasa sie tunamkubali nje ndani
 
Akubali kugombea Uenyekiti CHADEMA kanda ya Pwani.

Aomba wajumbe kumpigia kura.

FREDRICK Sumaye, Waziri Mkuu mstaafu amesema anatamani kuona ndoto yake inatimia kwa watanzania kubadili uongozi bila hofu na vitisho vinavyosababishwa na watawala kwa kutumia nguvu ya dola, anaandika Mwandishi Maalum.Sumaye ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Cha cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ameyasema hayo kutoka na historia za baadhi ya viongozi wa Bara la Afrika pindi wanapoingia madarakani kutopenda hata kuwaona wengine wakiinua pua.

Akizungumza na wandishi wa habari Kijijini kwake mara baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mwenyeketi wa Dar es Salam,Kijijini kwake Tondoroni, Kiluvya Pwani, Sumaye, amesema kuwa ni wakati sasa wa kukipeleka chama hicho hadi katika ngazi za vitongiji ambako ndiko wanakoringia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema ni vema watawala wa kiafrika wakawaacha wananchi kutumia demokrasia yao katika kujiamulia kuchagua kiongozi wanayefikiria atatekeleza malengo yao wanayoyatarajia.

“Ndoto niliyo nayo ni ile ile iliyonitoa CCM, katika demokrasia kwa mfano ukienda Marekani huwezi kuona wamarekani wamekiacha chama kimoja kikitawala miaka 30 hadi 40 kwaza hata miaka nane ni bahati sana kwa sababu chama kikitawala miaka nane huwa ni bahati kwasababu wanaju kikishatawala miaka hiyo kitakuwa kimepata fursa ya kutekeleza malengo yake,”amesema Semaye.

Amesema tatizo lilipo Tanzania ni chama kilichopo madarakani kutokubali kuviona vyama vingine vinainua pua ifike pali kwa chama tawala kukubali kushindwa pindi wananchi wanapoamua.

“Kwa kawaida chama chochote kikitawala muda mrefu hakiwezi kufanya vizuri na hiyo ni sawa na anayepiga maji wakati hajui kuogelea hali inayowanyima wananchi fursa ya maendeleo,”alisema Sumaye.

Sumaye, amesema ndoto yake nikuona CHADEMA ina wafikisha watanzania kule wanakotaka na kuamini kwamba sasa demokrasia imechukua mkondo wke.Akizungumzia uchaguzi huo wa Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Sumaye, amesema anawashukuru wanachama hao kwa kuonesha imani kwake na kuahidi kwamba yuko tayari kufanya kazi ya kukiimarisha chama hicho kuanzia ngazi ya chini kabisa.

Amesema, ingawa ili awe mwenyekiti ni lazima achaguliwe lakini aliwaahidi wanachama hao kwamba CHADEMA inahitaji kuongoza dola kwa hiyo kazu kubwa iliyoko ni wanachama wa chama hicho kujipanga kuanzia sasa ikiwemo kujiepusha na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Amesema haata inapotokea ni vema zikatumika busara katika kuipatia ufumbuzi ambayo matokeo yake ni kuwa na chama imara.

“Nawashukuru kwa kunichangia sh. 100000 ya kunichukulua fomu najuamefanya hivi kwa upendo wenu wala siyo kwa ubaya nami nasema nimekubali ombi lenu Bali naomba mnipigie kura msiishie hapa,”amesema Sumaye.

Naye mwanasheria wake Aidan Kitare amesema kwa vile kesho ndiyo siku ya mwisho atajitahidi pamoja na mgombea wake wanakamilisha utaratibu na kurusisha fomu hiyo kabla ya saa 6:00 mchana.

Mwita waitara mwenyekiti wa Dar es Salaam Kuu aliyekuwepo katika kumsindikiza kiongozi huyo, amesema wanachama hao waliyojitokeza kumchukulia fomu Sumaye walifanya hivyo wakiamini kwamba atakisaidia chama kwa vile anauzoefu mkubwa katika masuala ya uongozi katika utumishi wa Umma.
Huyu mzee Sumaye anachekesha sana! Anasema huu ni utawala wa vitisho na lazima aung'oe! Maswali kidogo kwake:
1.Upi utawala unatisha sana kati yake aliyewapiga waislam mwembechai msikitini na huu ambao wao ndio wanauchokoza?!
2.Alishindwaje kuing'oa hiyo ccm wakati alikuwa na mamlaka ya kuing'oa akiwa waziri mkuu kwa miaka 10?
 
Hiyo siyo sababu kwani hata katika maisha huwa tuna shindwa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo. Je tukate tamaa kwa kuwa tulikuwa na maisha fulani sasa Tumefirisika hivyo tusianze upya???????


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!

Babu yako hajashindwa bado ni premier mstaafu na anakula 80% salary ya Mh. Majaliwa sema tamaa tu na kutokubari kazi zinazofanywa na wengine yeye anajikubari yeye tu ndio maana akitoswa anahama chama kwake Chadema ni kitonga toka wakiteke na ni wakukaya. Sema JPM kawapigia na 4WD kabisa mwacheni akahadhirike huko. Yeye ni mzeefu na wala hawezi kuwalingania watu wa Pwani aligombea huko kwao CCM Nagu alimshinda amekimbia mazima.
 
Mhe. Sumaye yupo sahihi kabisa naamini ipo siku ndoto zake zitatimia siku CCM ikiondoka madarakani kwa amani
 
yaani former PM anakuwa mwenyekiti wa kijiji?

Ungebaki mshauri wa chama!

Sasa utakaa ukimuandalia mikutano Mbowe na akija ujipange barabarani kupokea na makuti ya pwani?

Achana na hizo fomu za mkoa wa pwani!

Unaweza kukisaidia chama kwa kutoa ushauri, kulikoni kuingia front ambapo utagombana na watoto! Wapi succession plans kwa nyie executives mliostaafu? Jenga watoto wakurithi sio kugombea nafasi ambazo vijana wangetumia kujenga chama na nchi yao!
Hii ni aibu na wala haina hata chembe ya Faraja kwa wana CHADEMA!
Well said
 
Hiyo siyo sababu kwani hata katika maisha huwa tuna shindwa na kurudi nyuma kabisa kimaendeleo. Je tukate tamaa kwa kuwa tulikuwa na maisha fulani sasa Tumefirisika hivyo tusianze upya???????


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Hapo issue sio kukata tamaa!
Katika maisha kila unavyopanda ndio unazidi kujitambua na kujipambanua!
Kwa wanao mature well,wanaanza kutambua roles zao ni kuongoza wengine kufikia malengo na sio kutenda wao!
I am sure kwa Sumaye mambo mengi ya kifamilia kwa sasa atataka wanae wayatende zaidi kuliko kutenda yeye mwenyewe! Yapo ya umri wake kama ushauri ktk vikao vya kifamilia, lkn biashara zake au vitu vingine angependa wanae ndio watende na yeye atoe support tu! (Note: Sio lazima yeye awe hivyo)!!
Kuna tatizo utakapoona mtu wa 65 au 70 anapanda majukwaani kujifanyia kampeni za ubunge, Uenyekiti wa kitongoji, wilaya au mkoa!
Kuna kazi ambazo ndizo za kuibulia vipawa vya vijana! Kama ana guts Sumaye aende akachukue fomu ya uenyekiti wa chama taifa, ingawa nao ni Umugabe!
Si dalili nzuri kwa chama!
Kwanza kwanini Sumaye aende Pwani? Kwanini hakuwahi kugombea chochote kwa mkoa wa Pwani alipokuwa CCM Ila kwa CHADEMA ameamua kwenda Pwani na sio Manyara kama alivyokuwa akifanya CCM?
Kwanini anabana nafasi za watu wengine, hasa wakazi halali wa mkoa wa Pwani kukiimalisha chama katika maeneo ya mashariki? Nadhani anatia DOA zaidi kuliko kukijenga chama! Please wana CDM pwani msimchague!
 
Babu yako hajashindwa bado ni premier mstaafu na anakula 80% salary ya Mh. Majaliwa sema tamaa tu na kutokubari kazi zinazofanywa na wengine yeye anajikubari yeye tu ndio maana akitoswa anahama chama kwake Chadema ni kitonga toka wakiteke na ni wakukaya. Sema JPM kawapigia na 4WD kabisa mwacheni akahadhirike huko. Yeye ni mzeefu na wala hawezi kuwalingania watu wa Pwani aligombea huko kwao CCM Nagu alimshinda amekimbia mazima.
 
Mtafuteni Sumaye muulizeni kuhusu Rais Magufuli anajibu zuri sana kwa sasa. Nakumbuka wakati wa uchaguzi miongoni mwa watu waliotamba kuwa Rais Magufuli ni mwepesi ni pamoja na mzee Sumaye Waziri Mkuu wa zamani katika Serikali ya awamu ya tatu.

Baada Rais Magufuli kuanza kazi amepiga kazi ambayo haijawahi kutokea mpaka amekuwa gumzo kwa Africa na Dunia nzima, miongoni mwa watanzania waliokiri kuwa Rais Magufuli haijawahi kutokea ni pamoja na aliyekuwa mgombea wa UKAWA mzee Lowassa.

Mtu mwingine aliyekutana na nguvu ya Rais Magufuli ni mzee Sumaye kwa sasa kama yupo mtu aliyekaribu na Sumaye aende amuulize kuwa anaionaje speed ya Rais Magufuli nadhani anaweza kutoa machozi kwa huzuni maana alivyodhani imekuwa tofauti na matakwa yake.

Mambo mengi aliyokuwa anayafanya Sumaye kiujanjaujanja sasa yote yamekwama baada ya mifumo yote ya Serikali kuwa inafanya kazi kwa ufasaha hana tena fulsa ya kufanya uhuni wala ujanja, nirudie tena muulizeni sumaye kuwa huyu Rais Magufuli ndiye aliyemdhani?
 
Hoja yako kubwa ni nini? Yaani tukamuulize sisi wakati wewe ndo unataka kumskia huyo Mr zero wako.. Nenda kamuulize wewe si tuko busy na mambo mengine.
 
Back
Top Bottom