Sumaye, Nagu katika vita kali: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye, Nagu katika vita kali:

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by sulphadoxine, Jul 20, 2012.

 1. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  .Nguvu ya Chadema yazidisha kiwewe Hanang
  .Pikipiki zaandaliwa kugawiwa katika kata zote
  .Vita ya urais 2015 nayo yahusishwa

  WAZIRI Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye, ameanza kupata vikwazo kuelekea uchaguzi mkuu 2015 baada ya kuwapo na taarifa kwamba Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) Dk. Mary Nagu anawania nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) wilayani Hanang nafasi ambayo mstaafu huyo anaiwania, Chanzo kutoka jikoni kimeeleza .  Taarifa za uhakika kutoka Hanang zimeeleza kwamba, Sumaye ambaye amekuwa akitajwa sana kuwa mmoja wa watu wanaotaka kuwania Urais kupitia CCM mwaka 2015, aliahidiwa na wana CCM wilayani Hanang kuipata nafasi ya ujumbe wa NEC bila kupingwa wilayani humo, sasa atapambana na Dk. Nagu.

  "Kumbe wana CCM kule Hanang walitaka wampe mzee Sumaye heshima ya kugombea NEC ya wilaya na apite bila kupingwa wakidai kwamba CCM wilayani humo imepoteza umaarufu kiasi cha kupoteza kata 13 kwenda Chadema huku CCM ikiambulia kata 12 tu," anaeleza mwana CCM mmoja kutoka Hananga, ambaye anakiri kuwa ni mfuasi wa Sumaye.

  Hata hivyo, nguvu ya Chadema wilayani Hanang imeelezwa kusababishwa na wimbi kubwa la chama hicho cha upinzani kuendesha kampeni zake mara kwa mara katika eneo hilo na mahusiano yake na jimbo la Karatu anakotoka Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa.

  Mwana CCM huyo ambaye kwa sasa yuko mjini Arusha, ameeleza kwamba pamoja na kanuni mpya kuhusu wabunge kugombea NEC kwa kibali maalumu, Dk. Nagu anatarajiwa kupewa kibali na Kamati Kuu kuwania nafasi hiyo.


  Habari kutoka Hananga zimeeleza kwamba huu utakuwa mchuano wa kwanza wa wazi kati ya Dk.Nagu na Sumaye, ambaye awali walielezwa kuwa watu walio karibu sana kabla na wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.

  Sumaye ambaye alikuwa Mbunge wa Hanang, ndiye aliyempisha Dk. Nagu katika nafasi hiyo na ilielezwa kwamba alimpa ushirikiano mkubwa katika kampeni zake za kuingia katika siasa za jimbo.


  "Dk. Nagu alikuwa mmoja wa watu muhimu katika timu ya Sumaye katika kuwania urais mwaka 2005 na alipoona mambo hayaendi sawa kwa mgombea wake, alihamishia kambi kwa mgombea mwingine, lakini alielezwa kuendelea kuwa mtiifu kwa ndugu yake wa Hanang, lakini sasa wanaingia vitani," anasema mchumi mmoja aliye karibu na wanasiasa hao.

  Sumaye hajatamka hadharani kuwania Urais ndani ya CCM ama chama chochote, lakini habari zinaeleza kwamba ni mmoja wanasiasa ambaye anaonekana bado kuwa na kiu ya kurudi katika siasa rasmi, lakini anatarajiwa kukumbana na visiki kadhaa vya kisiasa kutoka kwa wanasiasa na wanamkakati wengine ndani na nje ya CCM.

  Waziri Mkuu huyo Mstaafu aliyetumikia nafasi yake kwa miaka kumi chini ya Benjamin Mkapa, amekwisha kuingia katika malumbano na CCM na hata serikali yake kutokana na ****** ambayo amekuwa akiyatoa hadharani ikiwa ni pamoja na kuukosoa uongozi wa chama chake.

  Wakati sekretarieti ya CCM ikiwa chini ya Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, Sumaye alikaririwa akikosoa utendaji wa sekretari hiyo, na alipata upinzani mkali kutoka kwa viongozi wa chama chake na baadhi ya vyombo vya habari.

  Sumaye aliwataka viongozi hao kutokaa kimya badala yake wajibu hoja mbalimbali zinazoelekezwa kwao na wapinzani ili kutovipa umaarufu vyama hivyo kwa umma.

  Kauli hiyo ya Sumaye ilikosolewa na baadhi ya viongozi walioguswa, wengine kumwona kama mpinzani na kumtaka ajiunge na vyama pinzani.

  Inadaiwa kuwa, Sumaye ameamua kwenda wilayani Hanang kugombea nafasi hiyo ili kujihakikishia ushindi na kujiwekea mazingira mazuri ya kuingia katika kinyang'anyiro cha urais.

  Marekebisho makubwa yaliyofanywa na CCM hivi karibuni ni pamoja na kupitisha utaratibu wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kuchaguliwa katika ngazi ya Wilaya ili kukijenga zaidi chama kwa wananchi.

  Tayari mgombea mmoja wilayani Hanang ameelezwa kununua pikipiki atakazozigawa kwa viongozi wa kata zote za wilaya hiyo, jambo ambalo limeelezwa kuwa ni maandalizi ya uchaguzi huo.
   
Loading...