Sumaye kasema kweli;ccm wajibu hoja za kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye kasema kweli;ccm wajibu hoja za kisiasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwana Mnyonge, Mar 10, 2011.

 1. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 346
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Waziri mkuu mstaafu ,Fredrick sumaye amekirejesha darasani chama chake CCM .sumaye anaamini ccm hakijahitimu au kimepotea njia.anataka kisome upya ili hatimaye kiweze kutunikiwa cheti cha ushindani katika mfumo wa vyama vingi.Akizungumza na gazeti la kila siku la mwananchi sumaye ameitaka ccm kujifunza hoja za CHADEMA kisiasa,badala ya kuiachia serikali kupambana na chama hicho.
  amesema chadema wanafanya kazi za siasa lakini ccm imekaa kimya,wanataka serikali ndio ijibu hoja za chadema.hili si jambo zuri kwa kuwa chama kinatakiwa kijibu kila hoja inayoelekezwa kwake .kama hakina majibu kinatakiwa kuuliza au kuomba majibu serikalini .Hiyo ndio kazi ya chama cha siasa kilichopa madarakani.

  kauli hiyo imekuja siku moja baada ya katibu wa halmashauri kuu ya taifa (NEC) ya ccm wa habari na uenezi ,John chiligati kuomba vyombo vya dola viwe imara kuwachukulia hatua viongozi wa chadema kwa kile alichoita ......"kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu"

  source mmwanaHALISI jumatano march 9-15 ,2011
   
 2. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hawa ccm mi naona kwanza hawawezi kusoma nyakati, hawawezi kutofautisha kati ya utawala wa chama kimoja na vingi, wakae watafakari mara mia kwann wamefikia hapa walipo leo, watanzania wamechoka kudanganywa kama watoto wadogo. Huu moto wa Chadema ni mwanzo tu na wasipojirekebisha watatukuta watanzania tuko njian tunadai hhaki zetu, sio chadema tu, cku hizi tunaangalia mtu na c chama, chadema kkwa sasa ndo chama cha siasa chenye muelekeo chanya ambao ndo watanzania wanauhitaji.. Mzee Chiligat mambo yamebadilika kwa sasa
   
Loading...