Sumaye, Jaji Warioba wazidi kutetewa CCM; Yadaiwa uadilifu wao umewatengenezea maadui | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye, Jaji Warioba wazidi kutetewa CCM; Yadaiwa uadilifu wao umewatengenezea maadui

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  *Yadaiwa uadilifu wao umewatengenezea maadui
  *Hatua ya kujivua gamba yalinganishwa na kioo


  Na Tumaini Makene

  WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiendelea na mkakati wake wa kujivua gamba, kikilenga kujisafisha, mwanasiasa machachari, Mchungaji
  Christopher Mtikila ameibuka akisema huo ni ubabaishaji, huku akiwasifia baadhi ya mawaziri wakuu wastaafu kuwa ni mfano wa viongozi safi ndani ya chama hicho, lakini wanashambuliwa kwa sababu hawashiriki katika 'kukomba na kupora' nchi.

  Amesema kuwa CCM kinaugua maarufu katika kabila la Wapangwa unaojulikana kama 'nambulila' ambao mgonjwa hujiona ni mzima lakini wanaomzunguka humwona amekufa hivyo humtayarishia mazishi na hatimaye kumzika, huku mwenyewe (mgonjwa) akiwa hajiwezi kiasi cha kushindwa hata kufurukuta, kuwakatalia na kuwaambia kuwa yungali mzima, si mfu.

  Mbali na hilo, mwanasiasa huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Democratic Party(DP) ambacho moja ya sera zake maarufu ni 'kudai' uhuru wa Tanganyika, amekifananisha CCM na mtu anayejitazama kwenye kioo, ambapo kila akicheka, taswira nayo hucheka, kisha hujifariji kuwa amepata 'mwenzake' wa kucheka naye.

  Mwanasiasa huyo ambaye hujulikana kwa 'matata' na wakati mwingine ujasiri wake katika masuala kadhaa ya kisheria, amesema kuwa wanasiasa wachache wasafi waliobakia ndani ya CCM hawawezi kupata fursa ya kushauri, kwani kila wakifanya hivyo wanageuzwa kuwa maadui kisha wanashambuliwa.

  Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mchungaji Mtikila alisema kuwa CCM kinapaswa kuelewa kuwa sasa wananchi wanaanza kuamka katika usingizi wa 'nusu kaputi' kutokana na ujinga waliokuwa nao, hivyo lazima wataanza kuhoji masuala mbalimbali yanavyoendeshwa nchini, kisha watadai mabadiliko, ambayo mara nyingi hutokea bila viongozi (watawala) walioko madarakani kutaka.

  Mchungaji Mtikila alisema kuwa anakizungumza CCM kwa sababu ndicho chama kilichoko madarakani kwa sasa, kikiwa kimekabidhiwa dhamana ya kuwaongoza Watanzania kwa miaka mitano, hivyo chochote kinachoendelea katika chama hicho, kinaweza kuathiri kwa namna moja ama nyingine maisha ya kila Mtanzania nchini.

  "Hivi fikirieni mwenyekiti wa chama hicho ndiye anayeteua Kamati Kuu, ndiye anayeteua sekretarieti, tena wakati mwingine kwa kuwapigia simu tu watu anaoona ni rafiki zake, sasa ikimshauri akawa mbishi au ikishindwa kumshauri yeye anaepukaje kuwa sehemu ya gamba la chama hicho.

  "Lakini pia Mwenyekiti wa CCM katusaidia Watanzania kuelewa kumbe chama hicho ni joka ndiyo maana linahitaji kujivua gamba, lakini sisi tunajua kuwa dawa ya joka si kuliacha lijivue gamba, bali ni kuliteketeza na kulipotezea mbali. Namtakia mema Rais Jakaya Kikwete, maana watu wamechoka kweli, lakini naye ajivue gamba.

  "Watu wasafi wachache waliobaki CCM kila wakisema wanashambuliwa na UVCCM, wakisema kitu wanatukanwa, watu kama akina Bw. Fredereck Sumaye na Jaji Joseph Warioba hawana nafasi, hawa sijawaona katika ufisadi mkubwa kama vile uporaji wa madini yetu. Warioba alidhalilishwa kwa sababu si mwizi, hayuko katika kukomba na kupora nchi," alisema.

  Alisema kadhalika Bw. Sumaye amekuwa akikabiliwa na mashambulizi makubwa kisiasa kwa kuhusishwa na kashfa mbalimbali ambazo ukifuatilia kwa makini unabaini kuwa ni fitna zinazotokana na uadilifu ndani ya chama hicho.

  Alisema kuwa mara baada ya tuhuma juu ya Bw. Sumaye wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2005 hususan ile ya kununua shamba la wanaushirika huko Mvomero, Morogoro, walibaini kuwa hakuna taratibu zilizokiukwa kama vile uuzwaji wa nyumba za umma na Benki ya Taifa ya Biashara.

  "Baadae tulifuatilia vizuri, tulipomlipua huyu bwana, aliweka bayana ukweli ulivyo katika vikashfa kashfa vyake vya mashamba, huyu alikuwa mtu wa kilimo . Lakini pia pamoja ya kuwa alikuwa mtendaji mkuu wa serikali wakati ule tuligundua kuwa tuhuma za ufisadi mkubwa kama vile uuzwaji wa Benki ya NBC, nyumba...michezo hii ilikuwa ikichezwa na wengine.

  "Simjui Msuya, lakini namjua Sumaye, juzi naye kashambuliwa, karushiwa makombora na UVCCM ambayo kwenye usukani yupo Ridhiwan Kikwete. Sote tunajua kuwa ni katika awamu ya akina Sumaye ndipo uporaji wa kutisha, uporaji wa kijasiri wa nchi hii, lakini jiulize hivi leo Rais Kikwete akitaka kula mahali, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anaweza kumzuia kweli, hawezi. Anashindwa nini kufanya mabadiliko ya baraza la mawaziri na kumwondoa mara moja.

  Ufafanuzi wa Mchungaji Mtikila ulivutana na kiu ya waandishi wa habari, walimuuliza kuwa kama yuko tayari kumwomba radhi Bw. Sumaye kwa kumpakazi tuhuma, lakini mwanasiasa huyo alizidi kusisitiza kuwa baada ya kufuatilia kwa kina na mazingira ya kisiasa yalivyo ndani ya CCM wamebaini kuwa waziri mkuu huyo aliyekaa madarakani kwa muda mrefu kuliko mwingine yeyote nchini, hahusiki na tuhuma za ufisadi mkubwa kama ambavyo amekuwa akipakaziwa tangu alipotangaza azma ya kuwania urais kupitia CCM katika uchaguzi wa 2005.

  Akizungumza juu ya Jaji Warioba ambaye naye ni waziri mkuu mstaafu akiwa pia amewahi kushika nafasi ya makamu wa pili wa rais, mwanasheria mkuu wa nchi na jaji wa mahakama kuu, Bw. Mtikila alisema kuwa kiongozi huyo naye ni msafi kati ya watu wachache waliosalia ndani ya CCM, akiwataka kama hawawezi kuondoka, basi waendelee kutoa ushirikiano kwa vyama vya upinzani, kuwasaidia Watanzania.

  "Huyu bwana namkubali sana, kwanza ni mtanganyika mwenzagu, ni mtu ambaye amekuwa kidai uhai wa Tanganyika ambao kwa kweli uko ndani ya uhuru wa Desemba, mwaka 1961. Walimzulia kashfa ya Kampuni Mwananchi Gold. Lakini hazikuwa na ukweli wowote ule najua. Juzi kafanyiwa mambo ya ajabu sana. Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza mstaafu analetewa mapolisi na kuzuiliwa kuingia Karimjee kisa atazungumza mambo mazito ya ambayo wakubwa wananchi waelimishwe."
   
Loading...