Sumaye awa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Kubenea Makamu wake

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Matokeo Baraza la Uongozi CHADEMA Kanda ya Pwani

Mwenyekiti
Kidera : 15 = 17%
Sumaye : 74 = 83%
Makamu Mwenyekiti
Hassanali :18 = 20.2%
Kubenea (MB): 60 =67.41%
Mkono: 11 =12.35%

M/Hazina
Kasilima : 19= 21%
Ruth (MB) : 50 =56%
Lucy (MB) : 20 =22%
Idadi ya wapiga Kura: 112
Kura zilizopigwa : 89

Hongera kwa Washindi.

My Take
Hawa wabunge sijapendezwa na Kugombea vyeo hivi kwani kuna watu wasio na cheo chochote kwenye chama Waligombea. Hapa haki haijatendeka kwa kweli japo ni Demokrasia. Imefika wakati na CHADEMA wabadilishe Katiba, Mtu mmoja, cheo Kimoja.

Haya ni Maoni yangu, nawatakia Kazi njema Washindi.
 
Mbona cdm mumezoeleka kuchukua makombo na kuiga ya ccm...
Chukueni tu hiyo cheo kimoja mtu mmoja si tunajenga kiota kimoja bhana!!
 
Chadema hongereni ila sijaona kama walio chaguliwa wame reflect wakazi wa Pwani, pia watu kama kina Kubenea na Ruth ni wabunge tayari ,chama si kikubwa kias hiko kusema mtu awe na vyeo mbili mbili, so mjirekebishe kiaina.
 
CHADEMA Pwani Wamechaguana kanda ya Kaskazini tupu.Kwani huyu Sumaye kwao si Manyara?
 
Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Fredrick Sumaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani baada ya kumshinda mpinzani wake Mh Kidera, Sumaye alipata kura 74 na Kidera kura 15.

Wakati huohuo Mh Saed Kubenea alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti baada ya kuwashinda wagombea wengine wawili, akiwemo Mbunge ajaye wa Jimbo la Ilala Muslim Hassanali aliyepata kura 18 na Adolf Mkono kura 11.

Kila la heri CHADEMA.
 
Sumaye anahangaika ku-bounce back.Ukifikia level ya juu kama uwaziri mkuu kurudi tuvyeo tudogo kama huto twa mwenyekiti wa CHAMA mkoa ni kudhalilisha taasisi ya uwaziri mkuu.Kuna level ukifikia kubali tu kustaafu uishi kama mstaafu,mshauri nk sio kujishusha hivyo.
 
Ndio uana-harakati huo
 
Matokeo Baraza la Uongozi CHADEMA Kanda ya Pwani

Mwenyekiti
Kidera : 15 = 17%
Sumaye : 74 = 83%
Makamu Mwenyekiti
Hassanali :18 = 20.2%
Kubenea (MB): 60 =67.41%
Mkono: 11 =12.35%

M/Hazina
Kasilima : 19= 21%
Ruth (MB) : 50 =56%
Lucy (MB) : 20 =22%
Idadi ya wapiga Kura: 112
Kura zilizopigwa : 89

Hongera kwa Washindi.

My Take
Hawa wabunge sijapendezwa na Kugombea vyeo hivi kwani kuna watu wasio na cheo chochote kwenye chama Waligombea. Hapa haki haijatendeka kwa kweli japo ni Demokrasia. Imefika wakati na CHADEMA wabadilishe Katiba, Mtu mmoja, cheo Kimoja.

Haya ni Maoni yangu, nawatakia Kazi njema Washindi.
Duh. Kitoka uwaziri mkuu mpaka uwenyekiti wa chama. Kwani hajamaliza kuiba?
 
Back
Top Bottom