Sumaye atoa kauli nzito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye atoa kauli nzito

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mallaba, Oct 19, 2010.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  [​IMG] Azungumzia masahibu shule za kata
  [​IMG] Asema umoja wa taifa uko hatarini  [​IMG]
  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye  Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema umoja wa taifa unatishiwa na shule za sekondari za kata na kueleza kwamba sababu zinazotolewa juu ya kuendelea kufeli kwa wanafunzi wake ni nyepesi mno, hivyo utafiti wa kina unahitaji kufanywa kujua chanzo cha hali hiyo.
  Sumaye ambaye amekuwa si mwepesi wa kungumza hadharani kwa muda mrefu tangu astaafu mwaka 2005 serikali ya awamu ya tatu ilipomaliza muda wake, alisema pamoja na sababu zilizo wazi za upungufu wa walimu na ukosefu wa maabara katika shule hizo, lakini bado kuna kila sababu kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na wadau wengine kufanya utafiti huo ili kuondoa tofauti kubwa ya elimu kati ya watoto wa masikini na wenye fedha.
  “Najua zipo sababu kadhaa zinazotolewa kwa hali hii kuwepo, kubwa kabisa la upungufu wa vifaa vya kufundishia, lakini mimi naona haya ni majibu rahisi kuna tatizo tata hapo lazima lipatiwe majibu,” alisema Sumaye.
  Sumaye alitoa kauli hiyo mwishoni mwa wiki alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya tano ya Shule ya Sekondari ya Sumaye iliyopo katika Kata ya Bigwa katika Manispaa ya Morogoro.
  Alifafanua kuwa tofauti hiyo ya elimu inatokana na watoto wasio na uwezo kusoma katika shule za kata na wenye uwezo kusomeshwa katika shule za binafsi ambazo zinatoa matokeo mazuri.
  Alisema kuwa hali hiyo ikiachwa iendelee, kuna hatari ya kuvuruga umoja wa kitaifa. “Hali hii isiporekebishwa itajenga tabaka la wenye elimu nzuri na wenye elimu duni, shule za binafsi zitasomesha watoto wachache wenye uwezo na hao ndio watakaopata elimu nzuri na wataingia katika ajira nzuri na nafasi mbalimbali katika taifa,” alisema Sumaye ambaye alishikilia nafasi ya uwaziri mkuu kwa miaka kumi mfululizo kuanzia mwaka 1995 hadi 2005.
  Kutokana na hatari hiyo, Sumaye aliitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya utafiti wa kina kubaini matatizo yanayosababisha wahitimu wa shule za sekondari za kata kufanya vibaya katika matokeo ya kidato cha pili na nne.
  Alisema kuwa matokeo ya kidato cha pili katika kushindwa mitihani kilishuka kutoka asilimia 24 mwaka 2004 hadi asilimia moja mwaka 2007, lakini kiwango hicho kilipanda tena hadi asilimia 21 mwaka 2008 na kupanda zaidi hadi asilimia 47 mwaka 2009, ikimaanisha kuwa karibu nusu ya darasa walishindwa mitihani. Akizungumza katika mahafali hayo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Evarist Ndikilo, alisema pamoja na mapungufu ya shule za sekondari za kata, Serikali itaendelea kuzienzi na kuzilea kutokana na mchango wake mkubwa wa kielimu kwa taifa. Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Sumaye, Prosister Kavishe, alisema shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa walimu, maabara na kumbi za mikutano na vyumba vya madarasa.
  Mpango wa kila kata kuwa na shule ya sekondari ulianzishwa na serikali ya awamu ya nne baada ya kuingia madarakani kwa lengo la kuwawezesha watoto wengi kupata elimu ya sekondari.
  Hata hivyo, shule hizo zimekuwa zikitoa matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha pili na cha nne kutokana na kukabiliwa na matatizo mengi.
  Miongoni mwa matatizo yanayozikabili shule hizo ni ukosefu wa walimu, vitabu, maabara, miundombinu, madarasa na mabweni.
  Hali hiyo mara kwa mara imekuwa kisababisha baadhi ya makundi ya jamii kuikosoa Serikali kwa kushindwa kuwa na mipango endelevu kwa shule hizo.
  Licha ya kukosolewa, Serikali imekuwa ikijivunia mpango huo kwa maelezo kuwa watoto wengi wamepata elimu ya sekondari kupitia shule hizo na kwamba zinafahaulisha watoto wengi.
  Aidha, Serikali imekuwa ikitoa ahadi kuwa inakusudia kuziboresha shule hizo kwa kuzijengea maabara na kuvipatia vifaa vya kisasa.
  Kwa muda mrefu sasa serikali imeruhusu mifumo miwili ya kutoa elimu nchini, ukiwamo ule wa Kiingereza kama lugha ya kufundishia na mwingine Kiswahili.
  Katika shule zinazotumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia nyingi ni za binafsi na ada zake ziko juu kiasi kwamba familia zenye kipato kidogo haziwezi kumudu, hizo ndizo zenye walimu, vifaa vya kufundishia na mazingira mazuri huku zikifaulisha zaidi.
  Kwa upande mwingine, zile za lugha ya Kiswahili hazina walimu, zina msongamano mkubwa wa wanafunzi, mazingira duni, ukosefu wa vifaa muhimu hata madawati, na ndiko wanakosoma wanafunzi wengi zikiwa zinamilikiwa na serikali.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Some truth!
  Lakini haoni kwamba na yeye ni part na parcel ya maamuz mabovu?
   
Loading...