Sumaye alaani kauli ya Paul Makonda.

Sumaye alaani kauli ya Paul Makonda.

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,514
Reaction score
23,696
Siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumuahidi Rais John Magufuli kuwa mwaka 2020 atamkabidhi mkoa ukiwa na viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi, Chadema imelaani kauli hiyo.View attachment 976537

IN SUMMARY

Ahadi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Rais Magufuli kuwa atamkabidhi mkoa huo ukiwa na viongozi wote wa CCM mwaka 2020 imelaaniwa na Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye ambaye amedai ina dhamira ya kufuta upinzani.

Dar es Salaam. Siku chache baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumuahidi Rais John Magufuli kuwa mwaka 2020 atamkabidhi mkoa ukiwa na viongozi wote wa Chama cha Mapinduzi, Chadema imelaani kauli hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Desemba 24, 2018 jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani, Frederick Sumaye amesema kauli hiyo ya Makonda inalenga kufuta vyama vya upinzani na kuiacha nchi ya chama kimoja.

“Ahadi yake kwa Rais inamaanisha ataendelea kuvunja Katiba kwa kukandamiza upinzani ikiwemo kutumia vyombo vya dola ili kutimiza malengo yake,” amesema.

Sumaye ambaye pia ni waziri mkuu mstaafu amesema kwa mamlaka aliyonayo mkuu huyo wa mkoa hakupaswa kutoa kauli hiyo inayoonyesha wazi uvunjaji wa Katiba.

“Makonda amekuwa akifanya mambo mengi ya kuidhalilisha Serikali, kinachoonekana huenda kazi aliyopewa ni kubwa kuliko uwezo wake, aliyempa ambadilishie au yatakayofuata yatashangaza zaidi,” amesema Sumaye.

-Mwananchi
 
Acheni matamko kama serikali au makonda mwenyewe.. Chukueni hatua twambieni wananchi tuingie rod

kuni ubaya gani akisema hivo?mh waitara ndio alikuwa mvumilivo kashindwa itskuwa sumaye?! sumaye siyo mvumilivu hata sasa nikaogopa tu kumangamanga yeye kama ni kula alikula ccm akasomea akasomesh akShiba
 
Hahaha hizi laana ndio maana siku hizi hazinafanyi kazi, kila mtu analaani. Zamani kulikuwa nawatu wenye uwezo wa kulaani.
 
kuni ubaya gani akisema hivo?mh waitara ndio alikuwa mvumilivo kashindwa itskuwa sumaye?! sumaye siyo mvumilivu hata sasa nikaogopa tu kumangamanga yeye kama ni kula alikula ccm akasomea akasomesh akShiba
Hata kuandika hujui halafu unamkosoa Sumaye.
 
Back
Top Bottom