Sumaye aimwagia upupu serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumaye aimwagia upupu serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Dec 22, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  SUMAYE AONYA NCHI INAELEKEA KUBAYA
  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, ameonya kwamba nchi inaelekea kubaya kwa kuwa watu wanatumia fedha nyingi kwa kasi kuusaka uongozi na baadaye kuishia kuwanyanyasa….. Pia amewaasa wanasiasa kuacha kuwatumia wanafunzi wa vyuo vikuu kuusaka uongozi kwa maslahi yao binafsi kwa kuwa njia hiyo ni hatari kwa mustakabali wa taifa.

  Akizungumza katika mkutano wa viongozi wa Shirikisho la Wanafunzi wa Elimu ya Juu (Tahliso), Sumaye alisema nchi inaelekea kubaya kwa kuwa watu wanatumia fedha nyingi kupata uongozi na kwamba wakiingia madarakani wanakuwa wababe kwa wananchi waliomchagua.


  “Hivi sasa kuna kila dalili, ukitaka uongozi katika nafasi yoyote mpaka za chini, lazima utumie fedha sana, wapiga kura wananunuliwa na mwisho wa yote, wananchi wanaongozwa na kiongozi mbabe na asiyetaka kushauriwa na watu,” alisema Sumaye.


  Alisema utaratibu wa kununua uongozi ni hatari kwa sababu nchi inaweza kuingia kwenye matatizo makubwa kuwa kuwa kiongozi huyo anakuwa amepata madaraka kwa njia ya mkato, vijana wanapaswa kulisaidia taifa kwa kutokubali kutumika kuwaingia baadhi ya viongozi madarakani.Aliwataka vijana kuwa makini kwa kuwa wamekuwa wakitumiwa na viongozi wa vyama vya siasa kupata madaraka kwa ahadi kwamba vijana hao watapewa fedha au cheo baada ya kumaliza chuo.

  Alisema wanasiasa wanakuwa wastarabu na kuonyesha upole wakati wa kuomba kura, lakini wakipata madaraka wanakuwa wakali na kutumia ubabe katika kufanya uamuzi wa kitaifa. “Watu wakitaka uongozi wanakuwa wa pole sana katika kipindi cha kuomba kura, lakini wakipata madaraka wanakuwa wakali kama simba, hawataki kushauriwa na matokeo yake wanafanya maamuzi ya kibabe ambayo yanasababisha madhara makubwa kwa jamii na taifa kwa ujumla,”alisema Sumaye.


  Alisema hivi sasa viongozi wamekuwa katika mijadala mingi kuhusu tatizo la ajira bila kutoa ufumbuzi wa tatizo hilo.“Jambo hili limekuwa likizungumziwa kwa urahisi sana, kuzungumzia ajira bila kuzungumzia kiwanda ni sawa na kuhangaika na joto la mgonjwa badala ya kushughulikia ugonjwa unaosababisha joto hilo kupanda,”alisema Sumaye. Alisema tatizo la ajira linatatuliwa na kiwanda cha kuzalisha ajira ambacho ni uchumi utakaosambaa na kunufaisha watu wote na siyo kuwanufaisha watu wachache.

  Sumaye aliwataka wanavyuo na wasomi wa masuala ya uchumi kujadili tatizo la ajira kwa kuitisha makongamano ili kuwarekebisha wataalamu na wachambuzi wa mambo kwa lengo la kulisaidia taifa.Alisema endapo vijana watatumika vizuri na nchi kuongozwa na viongozi wenye uwezo kutakuwa na maendeleo makubwa na kuondoa tatizo linaloinyemelea taifa la kununua uongozi.

  Naye Mwenyekiti wa Tahliso, Paul Mkonda alisema hivi sasa kumekuwa na muamko mkubwa wa kisiasa baada ya nchi za Kaskazini mwa Afrika na kuleta hamasa kubwa katika vyuo vikuu nchini.

  “Wanasiasa wanawafanya wanafunzi kuweka mkazo zaidi katika siasa kwa maslahi yao binafsi, na kusababisha wanafunzi wengi kuaathirika kimasomo. Sisi tunaomba wanasiasa wawaache wanavyuo kwa kuwa siasa za chuo na za wanasiasa ni tofauti sana,” alisema Mkonda. Alisema suala la wanafunzi kushiriki katika siasa, inatishia ubora wa elimu katika vyuo vikuu na utulivu.

  Alisema wanapaswa kuweka mikakati thabiti kwa vyama vyote vya siasa ili kuhakikisha waanadhibiti na kukemea wanasiasa ambao wanawashirikisha wanafunzi katika siasa malengo yao. Tahliso inaandaa mikakati ya kuwa na programu ya kuandaa viongozi wa nchi kwa kutoa mafunzo mbalimbali ya uongozi.
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Sumaye amenikumbusha kampeni za mwaka jana Kikwete alivyolala mavumbini na kuwakumbatia viwete, miezi miwili baadaye polisi walipotupa maiti barabarani yaliyouawa na hao hao watumwa na serikali hakudiriki kufunua kinywa chake wala kutamka lolote, na huwezi kuamini kama ni yule aliyekuwa anagaagaa mavumbini na kuwakumbatia disable people. Ni hakika tunakoelekea kila dalili zinaonekana wazi, uvumilivu utafikia kikomo soon.

  Msafara wa Viongozi wa Chadema kwenda Ikulu ikiwa ni kutoka chama kikuu cha upinzani nchini ni pima joto tosha kwa Kikwete, kama kuna busara ambayo ilitakiwa kutumika ni kusikiliza ushauri wa hao kwani wanauwakilishi mkubwa nchini. Hata walao moja ya mapendekezo yao angefanyia kazi. Lakini kutia kapuni ushauri wao na kuruhusu sheria hiyo iliyopitishwa na upande mmoja tu wa wawakilishi bungeni, historia itamwumbua Kikwete.

  Nimeongea jambo hilo kwa maono ndani ya moyo wangu, na walio kinyume cha kauli yangu ni haki yao, lakini kama watakumbuka ninayoongea leo ipo siku wataona yametimia.

  "KIKWETE AMECHANGIA SANA CHADEMA KUPATA UMAARUFU"
   
 3. The Hunter

  The Hunter JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 1,049
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wakati riz na kina malisa wanawahonga wanavyuo hamkusema,mnaona ubaya wenu umefikia mwisho ndo mnakuja na matamko.
  Ole wenu
   
 4. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Hizi zote ni mbio za 2015. lazima wajikwae safari hii. Na atakaye jikwaa lazima apate donda ndugu.
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Wakinyamaa tunawaambia wanalindana, sasa huyu anajitahidi kuikosoa serikali sasa tunamgeuzia kibao eti anataka urais, dalili kuwa hatuna msimamo wa tunachojadili.
   
 6. d

  dannny Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wa vyuo vikuu ni watu wazima ambao more than 90% wana umri zaidi ya miaka 18. Wana haki kama raia wengine kushiriki katika masuala ya kisiasa tena tunawategemea wao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii. Ukiniambia kwamba wanafunzi wa vyuo vikuu wakae kimya na kufumbia macho kile ambacho kwa maoni na utashi wao wanaona kwamba ni uonevu na sio haki hili haliingii akilini kabisa. Shida moja ilioko hapa ni kuwa na viongozi wa vyuo vikuu walio mashabiki wa kisiasa wa chama tawala. Hapa ndio huwa tunaona hukumu isio ya haki ikitolewa na viongozi hawa eti kwamba wanafunzi hawa wakidai haki zao huambiwa kwamba wanatumwa na vyama vya upinzani.
  Ni makosa makubwa sana kuwa na dhana hii potofu kwamba vijana hawa wa vyuo vikuu ambao wengi wao kama nilivyokwisha kusema hapo juu kwamba wamefikisha umri wa zaidi ya miaka 18 hawawezi kuwa na mawazo yao binafsi na kwamba kila wanachokidai au kukisema basi lazima wawe wametumwa na vyama vya upinzani.
  Kwa mawazo yangu ninaamini kwamba mtu yeyote yule awe mwanafunzi, mkulima, mfanyakazi, kiongozi wa dini, au mfanyabiashara ana haki ya kutoa maoni yake, kudai haki yake na kukemema mambo yeyote yale yasio ya haki yanayotendeka katika jamii zetu ili mradi tu mtu huyu havunji sheria na anzingatia kanuni na taratibu zilizopo
  Tunachotakiwa na kujenga mifumo ambayo itatusaidia kuheshima uhuru wa kutoa maoni na kuheshimu haki za binadamu. Tuanzie hapo. na tunaweza.
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,054
  Likes Received: 7,259
  Trophy Points: 280
  Huyo Mahonda nae kilaza tu!!
  Eti wanafunzi wasishiriki siasa,
  Hapohapo eti Tahliso inawaandaa wanafunzi kuja kuwa viongozi (=wanasiasa) bora wa baadae!!
  Hajui kwamba wapo baadhi ya wanasiasa walionzia harakati zao vyuoni wakaja wakawa viongozi wazuri tu!!
   
 8. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hakuna jipya; maaskofu wameshasema hayo yote. Arudishe ardhi aliyowanyang'anya wanachi wa Mvomero hadi makao makuu yakajengwa kule porini
   
 9. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Kama ni upupu kweli si tu kwamba umemwagwa hapa bali ni kwamba umemiminwa kimoja; bwaaaaa!!!

  Shida tu ni kwamba hajaeleza wazi bila unafiki wowote kwamba anapendelea KATIBA-MPYA-PROJECT-MEMBE au KATIBA-MPYA YA WANANCHI. Yeyote anayefikiria kuja kugombea urais nchi hii ni sharti akatujibu hili swali kwanza tena bila unfiki ili nasi tumsikie.
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mi naona alichoongea ni upupu tu yaani hamna pointi hata moja hapo.
   
 11. WCM

  WCM Senior Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 153
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama kauli ya mheshimiwa inamashiko hivi sasa. Matatizo yanayoikabili nchi hivi sasa yameenza kipindi cha uongozi wake. nakumbuka alivyokuwa anatetea rushwa ya uchaguzi kuitwa takrima, wakati suala la mgombea binafsi lilipokejeliwa, wakati alipowaambia wafanya biashara ili wafanikiwe ni lazima wawe ni wanachama wa chama chake, na mengine mengi. Sasa jeuri hii ya kuisema serikali iliyorithi na kuendeleza alichokiacha inatoka wapi? Anaweza kuwa na nia njema, lakini waelewa wa mambo watamkumbusha ya nyuma. ili kauli hizi ziwe na u maana nadhani angetubu kwanza, au la akae kimya kwa sasa. Atumie nafasi aliyo nayo ndani ya chama kushauriana na wala siyo kwenye showcases.

  Nawasalimia
   
 12. n

  nchasi JF-Expert Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Fisadi mkubwa tena papa atatueleza nini watanzania tena wa vyuo vikuu. Usikute hata yeye anapenyeza rupia kwa wanafunzi ili apate umaarufu. Hata siku moja huwezi kuingia ndani ya gari halafu ukatumia energy kulisukumiza, kamwe huwezi hata kidogo. Hakuna aliye clean nda ya the Magambas'.
   
 13. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,650
  Likes Received: 3,299
  Trophy Points: 280
  Safi kabisa mkuu hapo umenena. Madai ya kuwa wanachuo ambao wengi wao ni watu wazima tena wenye kujitambua na kuyatambua dhahiri mazingira yanayowazunguka na zaidi ya hapo wenye elimu japo ya kuweza kutofautisha kati ya black and white eti wana shawishiwa na au kuburuzwa na wana siasa[ hizi uchwara]
  hakika ni kuwafedhehesha na kujaribu kuua ile spirit iliyo ndani yao kama wasomi kama tegemeo la taifa zaidi sana kama watu[raia kamili]wenye haki na uwezo wa kuchangia katika mustakabali wa taifa lao.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Jambo moja angebainisha kutoa ushauri na wahusika kutoufanyia kazi, maana uttezi wake ni wa kimantiki badala ya kutuletea ushahidi wenye kujenga hoja yake.
   
Loading...