Sumaye ahamasisha wabunge kuendelea kuibua hoja

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Na Hemed Kivuyo, Arusha
10/17/2009


BAADA ya kimya cha muda mrefu, Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ameibuka kuunga mkono mijadalaNa inayotokea bungeni na kuwataka wabunge waendelee kuibua hoja zaidi kwa manufaa ya taifa.

Kauli hiyo ya Sumaye imetolewa wakati tayari kuna mgawanyiko miongoni mwa wabunge, huku baadhi wakionekana kuwa mashujaa na wapambanaji wa ufisadi, wengine wakipinga na kutaka wachukuliwe hatua.

Hali hiyo imesababisha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kuunda kamati ndogo ya watu watatu wenye hekima chini ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, kufuatilia mwenendo wa wabunge na wanachama wake wanaoonekana kwenda kinyume na matakwa ya CCM.

Kabla ya kuundwa kwa kamati hiyo katika mkutano wake wa hivi karibuni mjini Dodoma, NEC ilimhoji Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki, Samuel Sitta kwa maelezo kuwa amekuwa akiruhusu mijadala inayoikosoa serikali na CCM.

Spika Sitta amekuwa akitajwa kama kiongozi wa kambi ya wabunge wa CCM bungeni, ambao wamekuwa wakijipambanua kama makamanda wa vita ya ufisadi baada ya matokeo ya Ripoti ya Uchunguzi ya Bunge kuhusu mkataba wa Richmond, ambayo ilimfanya Edward Lowassa, kujiuzulu mwezi Februari mwaka jana.

Wabunge wengine waliopo katika kundi hilo ni Mbunge wa Same Anne Killango, Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe na Lucas Selelii wa Nzega. Wengine ni Christopher Ole Sendeka wa Simanjiro na James Lembeli wa Kahama.

Hata hivyo, CCM ilieleza kugundua kuwepo kwa chuki miongoni mwa wabunge wake ndani ya bunge na Rais Kikwete akizungumzia hilo kwenye mazungumzo yake ya moja kwa moja na wananchi Septemba, mwaka huu.

CCM imeipa kamati ya Mwinyi ambayo wajumbe wake ni pamoja na Abdulrahman Kinana na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa kuchunguza kiini cha chuki miongoni mwa wabunge hao.

Akizungunza na Mwananchi Jumapili hivi karibuni, Sumaye alisema mijadala hiyo iendelee na kuwataka wabunge kutoogopa kuibua bungeni mijadala yenye masilahi ya taifa kwa sababu kufanya hivyo ni kukuza demokrasia nchini.

Sumaye alisema kuwa kutokea kwa mgongano wa mawazo baina ya wabunge ni hali ya kawaida na kwamba, hata lingekuwa bunge la chama kimoja, hali hiyo ingeweza kutokea kwa kuwa kila mmoja ana mawazo tofauti na mwingine.

"Mijadala na migongano ya mawazo bungeni ni jambo la kawaida, hata kama lingekuwa bunge la chama kimoja ingeweza kutokea.

Hali ya namna hiyo ni kukua kwa demokrasia hivyo sioni mantiki ya wabunge kuacha kufanya hivyo, nawashauri waendelee," alisema Sumaye.

Mwanasiasa huyo ambaye alishikilia nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa kipindi kirefu zaidi ya wote enzi za utawala wa awamu ya tatu wa Rais Benjamin Mkapa, alibainisha kuwa anapoliangalia bunge la Tanzania anaona kuna dalili ya kugawanyika.

"Ninapoliangalia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, naona kuna kila dalili ya baadhi ya wabunge kugawanyika," alisema Sumaye.

Alipoulizwa kama anafahamu kuwepo kwa baadhi ya wabunge ndani ya CCM wanaolalamikiwa kwa vitendo vya ufisadi na wananchi wa majimbo yao alisema: "Sifahamu kama kuna wabunge mafisadi walio ndani ya CCM".

Kuhusu kuwepo baadhi ya wabunge wa chama tawala kulalamikiwa kwa kushindwa kuwaletea maendeleo kama walivyoahidi, pia Sumaye alisema haamini kuwepo kwa jambo kama hilo.

Hata hivyo alisema iwapo kuna wabunge wameshindwa kuwaletea maendeleo wananchi, CCM isihusishwe na kushindwa kazi kwa wabunge hao.

Alisema kuwa wabunge wasiotimiza wajibu wao watahukumiwa na wananchi wenyewe kwa njia ya kura na kwamba, CCM bado ni imara katika kila nyanja.

Kama kuna mbunge hajatimiza ahadi zake basi hilo litakuwa tatizo lake na siyo la chama. Chama hakihusiki," alisema Sumaye.

Akizungumzia mustakabali wake kisiasa, Sumaye ambaye alikuwa Mbunge wa Hanang mkoani Manyara alisema tofauti na mawazo ya wengi kuwa yeye anataka kurejea katika siasa, lakini ukweli ni kuwa hatarajii kufanya hivyo.

"Pamoja na uwepo wa minong'ono kuwa nataka kurejea katika siasa na kugombea tena ubunge Jimbo la Hanang, habari hizo siyo za kweli. Sitarajii kuingia tena katika siasa zaidi ya kuwa mshauri endapo nitahitajika kufanya hivyo kwenye CCM," alisema Sumaye.

Alifafanua kuwa yeye alistaafu wakati bado anahitajika na wananchi wa Hanang pamoja na Watanzania kwa ujumla, pia bado ana afya njema itakayomwezesha kuendelea kuwatumikia wananchi na kusisitiza kwamba, hajawahi kufikiria kurejea katika siasa zaidi ya kujikita katika kilimo nyumbani kwake.

Hata hivyo Sumaye aliyekuwa mmoja wa wagombea kumi na moja wa nafasi ya urais mwaka 2005 ndani ya CCM na kuangushwa na Rais wa sasa Jakaya Kikwete alisema: "Si dhambi kwa kiongozi yeyote aliyestaafu kutamani na kurejea tena katika siasa kwani hajavunja sheria za nchi na pia kila mtu ana mtazamo wake katika muktadha wa kisiasa".

"Mimi nimestaafu siasa wakati bado nahitajika na wananchi wa Hanang na Watanzania kwa ujumla, lakini sitarajii kurejea tena katika siasa. Kama nitahitajika kutoa mchango wangu wa mawazo nipo tayari ili kuijenga nchi yetu," alisema Sumaye.


NB:
Kwa maoni haya Sumaye naamini bado ni mtu kuliko mwanzo akiwa waziri mkuu
 
sumaye could make a better presidency far far than poor jakaya,at last he has been cleared ....kuwa maneno mengi ya aliyozushiwa na wanamtandawo yalikuwa uwongo.....bado tunaikumbika kauli yake kuwa ..."mtu anayetumia kalamu [kuchafua wenzake] ili aingie madarakani .....atatumia bunduki kusalia madarakani""

siku hizi jakaya kupopolewa mawe na msafara kuzuiwa na wananchi na yeye kujibu kwa mabomu ya machozi ..imekuwa kawaida..

pia..juyu sumaye ndiye aliyeibua hoja ya afya ya mmoja wa wagombea...."watu wengine wanawachafua wenzao ili wawaongoze watanzania..wakati afya zao ni mbovu..""

sihitaji kusema neno hapo!!

sumaye and others contestants must feel very sorry for us now!!!..sijuwi tulilogwa!!..we chosed the least candidate..of allll!!
 
Hana lolote huyu anajaribu kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa anataka urais tu huyu
 
Wakuu mimi nadhani ni heri kwao CCM wenyewe na hata watanzania kwa ujumla alivyompitisha Kikwete 2005 vinginevyo asingepitishwa labda sasa hivi tungekuwa tunazungumzia mengine kabisa katika siasa za Tanzania.
Kumbuka Kikwete alikuwa anapendwa na watanzania wengi siku zile na wengi waliamini kuwa 1995 ni mizengwe ya Nyerere ndiyo iliyofanya aukose uraisi.Kikwete alishakuwa na imani kuwa kama hatawekewa mizengwe basi hakuna wakumshinda kati ya wale wagombea wenzake na ndiyo maana alipotangaza nia yake ya kugombea alikuwa mtu wa kujiamini sana na tena aliweka mkwara mzito kuwatisha viongozi wake wa chama watakaofanya mchujo.
Sidhani kama Sumaye angepitishwa angekuwa Rais bora au hata angeshinda huo urais kama kwa mfano Kikwete angeamua kujitoa na kundi lake kwenda chadema au kuanzisha chama chao halafu akagombea na Sumaye.CCM wangekuwa na kazi kubwa sana ya kumuuza Sumaye mbele ya Kikwete vinginevyo wangeiba kura na ndipo chokochoko ingeanzia hapo.Kipindi kile nakumbuka kulishakuwa na minongo'ono kuwa Sumaye ni chaguo la Mkapa.Na wengi walikuwa hawataki Sumaye awe Rais wa Tanzania.Nakumbuka kuna taasisi za dini zilitangaza wazi kuwa hazimtaki Sumaye sababu hakuwa mchumi japo kiuhalisia sababu haikuwa hiyo.
Kwahiyo tushukuru watanzania tuliokuwa hatuujui utendaji wa Kikwete sasa tunamjua vizuri na kutenda kosa si kosa kosa kurudia kosa.
 
Sumaye pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa Mkapa ni mtu wa karibu sana na Mkapa hata kabla hawajaingia madarakani. Wakati wa utawala wao kulikuwa na malalamiko mengi ya ufisadi dhidi ya Sumaye. Wakati huo Mkapa alikuwa bado ameficha makucha yake au tulikuwa hatujagundua kinachoendelea nyuma ya pazia. Sumaye baada ya kuachia madaraka alifanikiwa kujikosha na tuhuma kwa kuikimbia nchi kwa muda akaenda Marekani (masomoni?) na baadaye kuwatishia kuwapeleka mahakamani waandishi na wengine "watakomkashifu". Inaonekana vitisho vyake vilifanikiwa kwa sababu hakuna mtu anayemsema tena siku hizi. Lakini, je, ni msafi kustahili kurudi kwenye uongozi? Sidhani.
 
Sumaye ni mmoja wa viongozi wa Nchi hii aliyenufaika na ule UFISADI usiopigiwa kelele sana wa KUZITAFUNA taasisi za UMMA zilizokuwa chini ya ofisi yake. Moja ya taasisi zilizomnufaisha sana ni ile TUME YA JIJI alioiunda na kisha kumkabidhi ndugu yake Keenja.
 
Ngoja niwasiliane na Mbunge wangu "aibue"hoja ya Kibaigwa na ranchi za NARCO alizo jigawia.
 
Back
Top Bottom