SUMATRA: Zipi ni Nauli Sahihi na ZIpi si Sahihi na Je Mmechukua Hatua Gani?

Nami nasema vijijini bado kuna changamoto ya usafiri ..barabara mbovu na usimamizi kufikia hadi vijijini inakuwa ngumu ndio price zake haziko listed

Just imagine uko kijiji gari ya kwenda wilayani inatoka moja saa 11 asubuhi unafikiri price itakuwa rafiki kama zingekuwepo mingimingi


Kwa mifano niliyotoa ni njia za lami
 
  1. Juzi nilitoka Dodoma kwenda Iringa kwa bus umbali wa Km 260.8 nauli ilikuwa Tsh. 10,000
  2. Jana nilisafiri kutoka Iringa mpaka Morogoro umbali wa Km 303 na nauli kwa bus ni Tsh 15,000
  3. Nikapanda bus Kutoka Morogoro hadi Dumila umbali ni Km 69.4 na nauli ni Tshs 3000
  4. Nikapanda bus toka Dumila mpaka Kilosa Km 69.3 nauli ni Tsh 5000
  5. Leo nilipanda bus toka Dumila mapa Turiani Umbali wa Km 46 nauli ni Tsh 5000
  6. Jioni hii nimepanda bus toka Morogoro kurudi Dodoma umbali wa Km 262.5 nauli ni Tsh 15,000
Naomba kujibiwa maswali haya:
  • Inakuwaje nauli ya Kutoka Morogoro mpaka Dodoma Km 262 inafanana na Iringa hadi Morogoro Km 300 - Tsh 15,000 badala ya nauli ya Morogoro hadi Dodoma kufanana na ile ya Dodoma hadi Iringa ambapo umbali wake unakaribinana kabisa?
  • Inakuwaje nauli ya kutoka Dumila kwenda Kilosa ni sawa na Dumila kwenda Turiani wakati umbali wake unatofautiana kwa kuasi kikubwa sana? (Km 69 nauli 5000, Km 46 nauli Tsh 5000
  • Inakuwaje nauli ya kutoka Morogoro kwenda Dumila Km 69 ni Tsh 3000 ambayo ni ndogo kuliko kutoka Dumila hadi Kilosa na Dumila mpaka Turiani ambako ni Tsh 5000?
Nilijaribu kutumia huduma ya simu kama mlivyoelekeza kwenye website yenu website yenu lakini nayo nimeona haifanyi kazi ni usanii mtupu!! kwanini msiweke mabango makubwa kwenye stand za mabasi mkionyesha nauli za kila njia? na kama mabango yamepitwa na wakati basi tangazeni kwenye screen zilizopo stand kama ile ya Msamvu Morogoro ili kila abiria ajue?

Tangazo lenu linasomeka hivi:
Kujua viwango vya nauli ya mabasi kutoka kituo moja kwenda kingine:
Tuma ujumbe mfupi wa maandishi kama ifuatavyo:
Andika neno: Nauli, acha nafasi, Mahali unapoanzia safari, acha nafasi, Mahali unapoishia, kisha tuma ujumbe huu kwenda namba 15276Mfano: Nauli Tanga Mwanza

Kwanini mnaacha wananchi wanaibiwa nanyi mpo maofisini badala ya kutega mitego kuwakamata wanaotoza nauli isivyo halali?
Usiombe kujua nauli halali ya SUMATRA,mara nyingi nauli halali ya SUMATRA ni kubwa kuliko nauli ya SOKO,
 
Mabasi yanashusha bei kutokana na competition au status ya bus na idadi ya abiria kwenda route husika. Wanataka kupata wateja.

Unaweza ukawa umepanda bus 'economy' toka dom kwenda iringa ila toka moro kwenda dom ukapanda 'semi luxury' au 'luxury'.

Kwenda Arusha/Moshi toka Dar kuna wanaopanda kwa 36,000/33000 na wengine wanaenda na hata 20,000/18,000. Na hakuna anaelalamika wala kuuliza.

Haijalishi unashukia wapi, gari za moshi/arusha toka Dar hawakupunguzii nauli hata iweje tofauti na gari za Mbeya/Tunduma.
Uko sahihi,ila kwa Arusha Moshi Dar nauli ya SUMATRA iko juu kuliko nauli ya soko,ndio maana chrsmass sumatra wako bus stand,mfano moshi/dar bei ya sumatra ni 22000 kawaida,28000 semi luxuary,hadi 36000 full luxuary,lkn bei ya soko ni 15000/18000 kawaida,20000 semi lux,30000 full lux,,
 
@bavaria acha ujinga wewe aujaelewa Mada bora ukae kimya unajichoresha tu hapa tangu lini umbali wa dar to arusha ukawa Sawa na Dar to moshi..... Watu kutokulalamika ni kutokuelewa kwao.dar to mosh ni Zaid ya km500 wakati arusha ni Zaid ya 600km
SIKU sumatra wakifuata ushauri wako,walalahoi mtaumia,,narudia bei elekezi ya sumatra ni kubwa kuliko bei ya soko,DAR/MOSHI ni 22000 lkn sasa hivi watu wanasafiri mpaka 15000/,acha ubishi
 
SIKU sumatra wakifuata ushauri wako,walalahoi mtaumia,,narudia bei elekezi ya sumatra ni kubwa kuliko bei ya soko,DAR/MOSHI ni 22000 lkn sasa hivi watu wanasafiri mpaka 15000/,acha ubishi


Kwa bei ya SUMATRA
Dar - Kibaha ni Km 26 nauli ni Sh 1000
Ina maana kwamba mtu akisafiri Km 52 anatakiwa kulipa Sh 2000 (Nilitarajia watu wa Dumila - Turiani Km 46 walipe Sh 2000)
Ina maana mtu akisafiri Km 78 atalipa sh 3000
Akisafiri Km 104 atalipa Sh 4000
Akisafiri Km 130 atalipa Sh 5000
Akisafiri Km 156 atalipa Sh 6000
Akisafiri Km 182 atalipa Sh 7000
Akisafiri Km 208 atalipa Sh 8000 (Nauli ya Moro - Dar inahusika hapa ni Km 193)
Akisafiri Km 274 atalipa Sh 9000 (hapa wasafiri wa Moro - Dodoma Km 260+ wanaangukia kwenye fungu hili)
Akisafiri Km 300 atalipa Sh 10000 nk
 
Yaani idara nyingi za serikali hazihangaikii changamoto za wananchi wanajihanhaikia wao wenyewe ili kupata kipato sasa hebu ona huo mfano wako hapo na SUMATRA wapo wamejifungia ofisini wanasubiri siku mh. Rais aseme ndio waanze kufuatilia

Yaani hakuna uwiano wa nauli na umbali kwa maeneo mengi ya nchi wananchi wana ibiwa sana SUMATRA wapi tu ofisini hawaendi field kufuatilia na wanalipwa mishahara

Wapo busy na kuissue sticker za sumatra tu kwenye magari lkn wao kutoa service kwa wananchi ndo tatzo
 
Utetezi wa kijinga sana huu umeelewa content ya mtoa mada? Swala sio hadhi ya basi swala ni kwamba distance za safari zinatofaitiana na gharama. Umeona mfano hapo mtu anatoka mbeya kwenda morogoro lakini analipalishwa nauli ya Dar swala la msingi ndio lipo hapo na sio hadhi ya basi muwe mnaelewa mada ndio maaana mnafeli na mitihani.
Nauli elekezi ni ukomo wa kiwango cha juu kabisa ambacho msafirishaji anaruhusiwa kutoza
Hata hivyo kwenye maeneo yenye wingi wa mabasi na ushindani mkubwa wa kibiashara si ajabu kukuta nauli zipo chini sana kuliko zile zinazoelekezwa na Mamlaka
 
Hawa jamaa ni wapuuzi sana, yani unaweza kuta bus limeandikwa Luxury sasa ingia ndani ya bus hilo ni hivyo kabisa.

Alaf unaweza kuta mathalan kampuni kama Saratoga ana mabasi mawili kwenda Kigoma moja ni Luxury lingine ni ordinary tu lkn kila anyeenda kukata ticket anaoneshwa lile luxury baada ya kukata njoo kesho yani unapandishwa basi la hovyo. Mi mpaka huwa najiuliza sawa labda huku vijijini kwetu hawawez kufika jamani mpaka Daslam jijini?
 
Back
Top Bottom