Sumatra yaweka ukomo umri wa madereva | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sumatra yaweka ukomo umri wa madereva

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gumzo, Aug 29, 2012.

 1. G

  Gumzo JF-Expert Member

  #1
  Aug 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=3][/h]
  MAMLAKA ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), imesema umri wa madereva wa Usafiri wa Umma unapaswa kuanzia miaka 30 hadi 60 ili kuepusha ajali za mara kwa mara.

  Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na matukio mengi ya ajali ambazo zinahusishwa na uzembe wa madereva na kutozingatia sheria za barabarani.

  Hayo yalibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Udhibiti Usafiri wa barabarani, Aron Kisaka wakati akiwasilisha Kanuni za leseni ya usafirishaji kwa magari yanayotoa huduma ya usafiri wa umma ya mwaka 2012 kwa wadau wa usafiri.

  Vipengele vingine vilivyo wasilishwa katika Kanuni hizo ni pamoja na dereva kutoruhusiwa kuendesha gari zaidi ya saa nane mfululizo, kuendesha gari huku akiongea na simu pamoja na kuendesha gari huku akiwa ametumia kilevi cha aina yoyote.

  Akizungumza katika mkutano huyo, Mkurugenzi huyo alisema katika vipengele vya Kanuni hizo kimoja wapo ni utoaji wa leseni kwa madereva wa usafiri wa umma kuzingatia umri ambapo wao kama Sumatra watatoa leseni hizo kuanzia miaka 30 hadi 60 kwa madereva.

  “Umri wa madereva wa usafiri wa umma unapaswa kuanzia miaka 30 hadi 60 kwani tunaamini kwamba umri huu ni mzuri kwa madereva wengi kuwa makini,” alisema Kisaka na kuongeza:

  “Kanuni mbalimbali ambazo tumeziwasilisha hapa ili kuzijadili kwa mafufaa ya sekta ya usafiri lakini ifahamike wazi kanuni hizi haziwezi kupitishwa moja kwa moja hadi tupate maoni ya wadau wa usafiri,” alisema.

  Kisaka alifafanua kwamba baada ya Kanuni hizo kuwasilishwa kwa wadau wa usafiri zitapelekwa Wizara ya Uchukuzi na badaye kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kabla hazijaanza kutumika rasmi.

  Akizungumzia adhabu ambazo watapewa madereva watakaokiuka kanuni hizo, alisema kuwa ni pamoja na kufungwa jela na kutozwa faini mbalimbali kulingana na kosa atakalolifanya.

  “Madereva ambao watabainika kutumia vilevi wakiwa wanaendesha gari watatozwa faini ya Sh100,000 na kifungo jela mwaka mmoja,” alisema na kuongeza:

  “Upande wa wamiliki wao watatozwa faini ya Sh500,000 na kufungwa jela miaka mitano kama magari yao yatakamatwa yakifanya kazi ya kusafilisha abiria bila kuwa na leseni ya usafirishaji,” alisema.

  Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kama mmiliki wa daladala au usafiri wowote wa umma hatakubaliana na uamuzi utakaochukuliwa na Mamlaka hiyo anaweza kukata rufaa au kupinga kupitia sheria ya Sumatra ya mwaka 2008.
  Katika hatua nyingine wadau mbalimbali wa usafiri vikiwemo vyama vya usafilishaji vilipinga baadhi ya vipengele vya kanuni hizo na kuitaka Sumtra kufanya marekebisho.

  Vyama ambavyo vilishiriki katika mkutano huo wa kujadili Kanuni hizo za leseni ya usafirishaji ni pamoja na Chama cha Wamiliki wa Daladala Dar es Salaam (Darkoboa), Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafirishaji Majini na Nchi Kavu (Sumtra CCC).

  CHANZO: GUMZO LA JIJI
   
 2. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  wamekurupuka hawa sumatra
   
 3. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,840
  Likes Received: 456
  Trophy Points: 180
  I give them a support!! Umri Mwingine Uwe ni Kupata experience!! Ndio maana huwa kazi Nyingi zinatolewa na Experience ya Mhusika say 10 years!! Mbona tulio na 4 years experience Hatulalamiki?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Wamelazimisha mitaala ya ufundishwaji wa madereva iwe moja?
   
 5. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Umri ni muhimu sana kwenye leseni.Kwenye daladala,makonda wetu hawa wasio na maadili ,baada tu ya muda wanakua madeleva ,unategemea nini?Umri na pia kupitia kile chuo cha usafirishaji itasaidia kupunguza ajali.
   
 6. K

  Kyoombe JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 23, 2011
  Messages: 649
  Likes Received: 59
  Trophy Points: 45
  this is another way of reaping where they never sowed a seed!
   
Loading...