SUMATRA na magari ya wanafunzi

SUMATRA na magari ya wanafunzi

funzadume

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2010
Posts
13,650
Reaction score
21,520
Kuhusu hii issue ya magari yote yanayobeba wanafunzi kupakwa rangi ya njano na kutobeba abiria wa kawaida nadhani SUMATRA wamekurupuka bila kuangalia hali halisi ya maisha ya mtanzania

Kwa mfano mimi mtoto wangu anasoma shule ambayo ina mabasi mawili tu na imebidi mimi na wazazi wenzangu tunaokaa maeneo ya karibu tukubaliane kukodi basi la abiria kupeleka watoto shuleni asubuhi na kisha kuwarudisha saa 10 jioni wanapotoka shule na kipindi cha kati wakati watoto wako shule basi hilo uendelea na shughuli zake

Hii inasaidia sana kuwafanya watoto kuwahi kuliko kuzungushwa mji mzima na mabasi machache ya shule na kuingia majumbani late hours na kumfanya mmiliki wa gari lililokodishwa kufidia upungufu kwa kuendelea na biashara pindi wanafunzi wakiwa shuleni

Tatizo linakuja baada ya SUMATRA kusema kuwa magari yote yanayobeba wanafunzi yapakwe rangi ya njano na pindi yakionekana yamepaki stendi kuchukua abiria wa kawaida watatozwa faini ya Tsh 250,000.00 au kama likibeba w/funzi bila rangi ya njano faini ni hiyo hiyo

Hii inaonyesha kuwa kama wazazi watakodi gari itabidi lifanye kazi hiyo tu kitu ambacho kwa wamiliki haiwalipi kabisa na kama wakihamua kukodisha magari yao kwa kupaka rangi inabidi kwa mfano Hiace inayobeba watoto 25 itoze kila mtoto Tshs 65,000.00 kwa mwezi ndio inaweza kumlipa mwenye gari fedha ambayo kama una watoto zaidi ya mmoja ni nyingi kwa mzazi tofauti na tunayokuwa tunalipa zamani Tsh 30,000 kwa mwezi kwa mtoto

Sijapata logic ya SUMATRA kung'ang'ania hiyo issue ambayo haina manufaa yoyote kilojikia zaidi ya kuleta vipingamizi visivyo na msingi wakati tunaelewa kabisa tatizo la usafiri kwa w/funzi lilivyo kubwa ktk nchi yetu hasa miji mikubwa
 
Pole sana ndugu yangu.....kwani hakuna shule jirani na unapoishi?
zipo ila naongelea hizi za kulipia (English Medium) ingawa hata shule za serikali wanakodisha magari mfano ni Forodhani, Mnazi Mmoja, Bunge, Muhimbili na nyingine
 
zipo ila naongelea hizi za kulipia (English Medium) ingawa hata shule za serikali wanakodisha magari mfano ni Forodhani, Mnazi Mmoja, Bunge, Muhimbili na nyingine

Zilipaswa kuhamishwa hizi toka kati ya mji kwenda nje ya mji kupunguza msongamano
 
Magari ya wanafunzi ndo mkombozi wa wanafunzi sasa kama wanafunzi wanasubiri stendi mnasema faini hivi sumatra mna akili kweli?
 
Magari ya wanafunzi ndo mkombozi wa wanafunzi sasa kama wanafunzi wanasubiri stendi mnasema faini hivi sumatra mna akili kweli?
kuna tatizo ktk uongoziwa SUMATRA
 
Back
Top Bottom