Ndugu wanabody,
Napenda kuwasalimia pia na kuwapa pole na kazi na mishemishe za kila siku. Mimi ni mkazi wa jijini Mwanza jiji ambalo linakuja kwa kasi katika ukuaji na ongezeko la watu.
Shunghuli zangu ni dereva wa daladala hapa mjini na nimekuwa nikiendesha daladala huu ni mwaka wa tano ila miaka yote hii sijawahi kuajiriwa au kupewa barua ya mkataba na tajiri yangu.
Point: Katika maelekezo ya mwenye gari kabla hajapewa kibali na SUMATRA cha kuweka gari la abiria barabarani ni lazima tajiri awe na mkataba wa dereva atakaendesha hilo gari, cha ajabu huyu tajiri yangu ana daladala 30 na ameajiri madereva 2 tu na kila SUMATRA ya gari ikiisha anapeleka mkataba wa dereva mwajiriwa na kuna kipindi unakuta magari kama 10 yameisha SUMATRA lakini unatumika mkataba 1.
Sasa tulikuwa tunajiuliza sisi madereva vibarua hii inakuaje kama kweli SUMATRA wanafanya hivi, ila katika kupepeleza hapa na pale kumbe boss uwa anawapa rushwa SUMATRA ili kuminya ajira zetu, madereva mengine, ni kwamba kutokana na hili boss amekuwa akitutishia kila ukimuuliza suala la ajira kisa eti wapo wengi wanaotaka kazi pia waajiriwa wamekuwa wakitishiwa kila wakiomba kuongezewa mishahara kuwa vibarua wapo wengi, ebu tusaidiane hili wapendwa, watu wanalipwa 150000 kwa mwezi pia mimi naamini kama SUMATRA wangezingatia haki tusingelipata taabu. Takukuru tusaidieni.
Madereva wenzetu nilijaribu pia kuwauliza madereva wenzetu wa mabasi nao matatizo ni kama hayo ila madereva wa makampuni ya kitalii ndio shida. Mwanza inakuja juu kwa utalii lakini madereva ambao ndio wataalamu wa kazi za utalii ambao wanasidia makampuni hayo kukua na kuvuna utajiri wa kutisha bado hawana thamani mbele ya mabosi zao wa Kihindi.
SUMATRA mikataba ni yale yale kampuni zingine zina magari 20 ila mwajiriwa 1 au 2 likija suala la mikataba kuhonga kuko palepale haiwezekan magari 20 yaendeshwe na dereva 1 kwa mkataba wa dereva 1 ifike hatua SUMATRA muone aibu vijana wenu wazalendo wanapata taabu kwa kukosa ajira, huku tukiwaneemesha wahindi wakwepa kodi.
Niliwahi kuongea na dereva wa tours Mwanza ambae ameajiriwa eti analipwa 250000 na nusu kwa mwezi bila makato huu ni mshahara wa kidharalishaji, ebu fikiri mgeni mmoja anaweza kuingizia kampuni zaidi 5m kwa safari ya siku nne toka Mwanza hadi Arusha lakini mtaalamu huyu dereva unakuta mshahara ndo huu, dereva anapewa posho ya safari kwa siku elfu 20 -25 kwa siku, hiyo ndo chakula, kunywa, kulala na matumizi ya familia yake, hii cio fare.
Inasemekana kampuni ina uwezo wa kupata watalii wa kuweza kuilipa kampuni zaidi 50m kwa mwezi ila dereva mwajiriwa akaambulia 250000 ya mshahara na 25000 kila siku ya posho, bado gari ikipata uharibifu wa tairi kubasti unalipishwa wakati huo vibarua uambulia 25000elfu tu kila ukisafiri kumbuka gharama za maisha zimepanda ambapo gesti mbovumbovu ya chini Arusha 15000 unabaki 10000 hiyo ndo ule unywe, na matumizi ya familia.
Najua nimewachosha wapendwa ila ni kutokana na hasira na pa kusemea hapapo tofauti na hapa.Nawatakia mchana mwema pia nitaona furaha kama wahusika wameona watusaidie pia niwieni radhi kwani sina kipaji cha uandishi.