Kwel kabisa aiseeBaada ya mabasi, BIASHARA ZOTE ziruhusiwe masaa 24 (24/7). Na tuanzie DSM.
Itakuwepo "Bus Tracking System". Hiyo haina ubishi.Usiku tochi zitakuwepo?
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA), imepanga kuruhusu mabasi ya mikoani kufanya safari zake muda wote (mchana na usiku), ikiwa ni hatua za kuongeza tija katika sekta ya usafiri.
View attachment 670836
Sababu zilizosababisha kufutwa safari za usiku hazipo tena? Mabasi Kusafiri usiku ni kuongeza uwezekano wa ajali na vifo vinavyoweza kuzuilika.
Mimi sitasafiri kwa mabasi yatayokuwa yakisafiri usiku labda niwe na dharura.
Vv
Hiyo initiative ni nzuri mno.Lakini wahakikisheni abiria usalama muda wote WA kusafiri usiku maana usiku hubeba mengi wakiwepo waharifu.Nawapongeza kwa mpango huo mzuri.Kasi hii iendane NA daladala za DSM maana MTU kama anafika DSM usiku anafanyaje tofauti NA kulala jambo linaloweza kumuongezea maumivu abaria.
Hapana Mkuu, suala la ajali ni uzembe wa dereva, mwendokasi na ubovu wa gari. Hivi vitu vikidhibitiwa basi nna hakika hakutakuwa na ajali. Nenda Kampala saa saba usiku stendi iko bize watu wanasafiri kwenda mikoa mbalimbali, yaani 24hrs terminal iko bize. Ni wakati kuafaka nasi kubadilika, ukitaka kwenda Mwanza sio lazima uamke saa 10 alfajiri kuwahi basi Ubungo, ifike wakati unaamua unaondoka saa ngapi sio unapangiwa kuondoka.Wanataka kuongeza idadi ya Watanzania watakaochinjwa barabarani. Uamuzi hovyo kabisa. Tutegemee ongezeko la ajali za kutisha barabarani.