SUMATRA kunyonga wanyongeni lakini haki zao wapeni

SUMATRA kunyonga wanyongeni lakini haki zao wapeni

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Imekuwa ni hulka kutembezeana ubabe ubabe hata katika masuala ambayo hayana ulazima wowote. Imekuwa hivyo hivyo tokea kwa:

1. Wauza nyama na serikali za mitaa kama ilivyo ripotiwa tokea Mwanza hapo jana
2. Tume ya uchaguzi na vyama vya siasa
3. Serikali na wapinzani
4. SUMATRA na Taboa
5. Nk nk

Hebu fuatilia clip ninayoambatanisha kuona busara za kawaida tu zinavyoendelea kututupa mkono.

Ni wazi kuwa tunakoelekea si kwema hasa pale ambapo kibinadamu hujinadhania hayatuhusu pale udhalimu unaofanywa unapokuwa hauna athari za moja kwa moja kwa makundi mengine kwa wakati huo.

Unathibitika ukweli ule kuwa “wakimalizana na sisi watakuja kwenu”. Hadi pale udhalimu kwa jina la udhalimu utakapo pigwa vita bila kujali unaelekezwa wapi, tokea wapi na nani udhalimu utatamalaki dhidi ya haki.

Maswahiba tunayoyaona wakifanyiwa wengine ni wazi kuwa ni suala la muda tu.

Leo Sumatra wanasema wanapambana na Taboa kuwafanya wadau wa serikali kwa kuwatoza faini kubwa kubwa. Jamani kuna machozi ya mamba kuliko haya?
 

Attachments

Back
Top Bottom