SUMATRA kitengo cha mabaharia ni jipu

Seaman88

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
417
156
Nawasilisha malalamiko yangu kwa uchungu mkubwa, kwa heshma na taadhima naziomba mamlaka za juu zinazojihisisha na SUMATRA kitenga cha mabaharia wamulike kwa jicho la pili kitengo hiki kwani ni kero kwa waohitaji huduma katika ofisi hizi.

Wafanyakazi hasa wale wa ngazi za chini kwenye eneo hili ni waliojaa viburi vilivyokithiri, panapokuja suala la kupata hiduma kwenye eneo hili wahuduma hawana lugha nzuri kwa wateja ni wenye viburi na hawasikilizi wateja wao.

Kitengo cha utoaji wa vyeti ni kitengo kilichojaa kero na usumbufu wa hali ya juu, kwa mazingira hayo ni dhahiri kwamba kuna mazingira ya rushwa na ukiukwaji wa taratibu ziliziwekwa na mamlaka, huduma zinatolewa kiupendelea na kwa kufahamina.

Mamlaka za juu ziliangalie hili kwani mabaharia Tanzania tunapata usumbufu mkumbwa, inakuchukua hadi miezi 3 kupata vyeti tulivosotea darasani kwa muda mrefu, wahudumu hawana uelekeo kusaidia wanaohitaji huduma.

Mh. RC Makonda fanya ziara maeneo haya ujionee watendaji wako wanavojifanyia kazi kiholela. Tunapata taabu wananchi wako. Mh waziri Njoo uone utaratibu uliopo hapa.
 
Back
Top Bottom