Kwema humu?
Twende kwenye mada,
Daladala zinazotoka Posta kuja Mwananyamala hupita Barabara ya Mwinyjuma moja kwa moja vituo Vijana, Komakoma, Gereji, Mwananyamala "A", Shule, Kwa Manjunju, Ujiji, Mama Zakaria ndo zinakunja kulia mpaka pale Royal zinakata kushoto lami mpya kuelekea Makumbusho.
Zikiwa zinarudi sasa kuelekea Posta hurudi na lami mpya lakini pale Royal hazirudi na njia ya Mama Zakaria, Ujiji, kama zilivokuja awali, bali hukata kushoto kuelekea vituo Keep left, Mwananyamala Sokoni, Mwananyamala Hospital kisha Mwananyamala "A" ndio hukutana na njia ya awali iliyokuja nayo.
Kwa hiyo wakazi wa Vituo Shule, Manjunju, Ujiji, Mama Zakaria wenyewe huziona hizi daladala zikiwa zinaenda tu Makumbusho, zikirudi hawazioni kutokana na sababu nilizotaja hapo juu. Wakazi hawa wakitaka kwenda Posta hulipa kwanza nauli ya vituo vyao mpaka Makumbusho kisha ndio hulipa nauli za Posta.
Kwa kawaida kwenye vituo vingi abiria wengi hupenda kupanda mabasi ya kwenda kugeuka ili wapate siti abiria wakishuka, hivyo huamua kwa hiyari yao kulipia mara mbili lakini kwa Wakazi wa Mwananyamala ni lazima, hakuna hiyari hapo.
Mkazi anaetokea Mwananyamala maeneo tajwa kwenda Posta just hardly 5km analipa zaidi ya yule anaetokea Mbezi about 17km kwenda same place, Posta.
Sielewi either @SUMATRA hawajui huu wizi kama upo, au hawajui kama ni wizi hivyo wameubariki. Wangerudisha gari hizi zirudie na njia yake ya Mama Zakaria au wawakataze kulipisha mara mbili.