SUMATRA fuatilieni utapeli huu AZAM MARINE

Abdallah M. Nassor

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2008
Posts
600
Reaction score
620
Habarini wakuu!

Niende moja kwa moja juu ya utapeli unaofanywa na wakata tiketi wa boti za Azam. Mnamo siku ya Alhamis majira ya saa saba mchana nilifika bandarini nikiwa ni msafiri kwenda Zanzibar. Bajeti ya nauli niliyokuwa nayo ni 25,000 kwenda na kurudu nauli hio hio.

Sasa kufika pale nikaambiwa bei ni 35,000/- nikasema nataka ya 25, mkatishaji akasema labda ukate ya kesho asubuhi. Basi kwa shingo upande nikaongeza 10,000/- nikapewa hio ya elf 35.

Kinachoniuma zaidi ni pale jamaa yangu niliyekuwa nasafiri nae alifika bado robo saa tuanze kuingia melini alikata tiketi ya 25,000/-. Kabla hajafika nilimwambia awahi asijekuta na hizo za 35 zimeisha akaambulia za 50.

Hilo nikalimezea tu nikasema bas labda sio bahati yangu. Kilichoniuma zaidi na zaidi ni huko Zenji, nilifika saa moja kasoro asubuhi kukata tiketi na hapo pia naambiwa hakuna za elfu 25 kwenye boti ya saa tatu zipo za 35, 50 na 60 tu. Kwa shingo upande tena nikakata hio 35.

Jamaa yangu kama kawaida yake kachelewa chelewa badae anakuja bandarini ananipigia simu namwambia nipo humu VIP Lounge, anasema kwani sikupata za 25? Mbona yeye kakata sasa hivi kwa 25!

Kwa kweli nimeumia sana kwani bajeti yangu imeharibiwa na hawa wakata tiketi, hivyo naomba sana SUMATRA komesheni hii hali, yaani wanalazimisha kuuza za bei ya juu kwanza halafu ndio wauze economy. Na wanadanganya kwa kusema zimeisha. Sumatra tusaidieni kwa hili tafadhali.

Nawasilisha wakuu!
 
hawa sumatra sijui wanafanya nini yaani toka Kilimanjaro mpk Dodoma nauli ni 23,000 ila tunakatiwa Kwa 28,000 alafu wao wanasimamisha tumbo zao huko barabara wakipewa ela ya kiwi na makonda wasifike kwenye gari
 
Ni muda muafaka sumatra kuwawajibisha wamiliki wanaolea matapeli mbona kwenye ndege hakuna huu upuuzi
 
Habarini wakuu!

Niende moja kwa moja juu ya utapeli unaofanywa na wakata tiketi wa boti za Azam. Mnamo siku ya Alhamis majira ya saa saba mchana nilifika bandarini nikiwa ni msafiri kwenda Zanzibar. Bajeti ya nauli niliyokuwa nayo ni 25,000 kwenda na kurudu nauli hio hio.

Sasa kufika pale nikaambiwa bei ni 35,000/- nikasema nataka ya 25, mkatishaji akasema labda ukate ya kesho asubuhi. Basi kwa shingo upande nikaongeza 10,000/- nikapewa hio ya elf 35.

Kinachoniuma zaidi ni pale jamaa yangu niliyekuwa nasafiri nae alifika bado robo saa tuanze kuingia melini alikata tiketi ya 25,000/-. Kabla hajafika nilimwambia awahi asijekuta na hizo za 35 zimeisha akaambulia za 50.

Hilo nikalimezea tu nikasema bas labda sio bahati yangu. Kilichoniuma zaidi na zaidi ni huko Zenji, nilifika saa moja kasoro asubuhi kukata tiketi na hapo pia naambiwa hakuna za elfu 25 kwenye boti ya saa tatu zipo za 35, 50 na 60 tu. Kwa shingo upande tena nikakata hio 35.

Jamaa yangu kama kawaida yake kachelewa chelewa badae anakuja bandarini ananipigia simu namwambia nipo humu VIP Lounge, anasema kwani sikupata za 25? Mbona yeye kakata sasa hivi kwa 25!

Kwa kweli nimeumia sana kwani bajeti yangu imeharibiwa na hawa wakata tiketi, hivyo naomba sana SUMATRA komesheni hii hali, yaani wanalazimisha kuuza za bei ya juu kwanza halafu ndio wauze economy. Na wanadanganya kwa kusema zimeisha. Sumatra tusaidieni kwa hili tafadhali.

Jambo la kwanza Sumatra hawana mamlaka huku Zanzibar, huku kuna ZMA ofisi yao ipo hapo hapo bandarini karibu na hizo ofisi za Azam

Jambo la pili jifundishe kufanya booking mapema unapotaka kusafiri. Ingia tu kwenye google andika Azam booking then fuata maelekezo.

Tatu kama wewe ni msafiri wa mara kwa mara fanya mazoea na wale jamaa wa bandarini wakuekee tiketi ili ukifika unawalipa.
 
Habarini wakuu!

Niende moja kwa moja juu ya utapeli unaofanywa na wakata tiketi wa boti za Azam. Mnamo siku ya Alhamis majira ya saa saba mchana nilifika bandarini nikiwa ni msafiri kwenda Zanzibar. Bajeti ya nauli niliyokuwa nayo ni 25,000 kwenda na kurudu nauli hio hio.

Sasa kufika pale nikaambiwa bei ni 35,000/- nikasema nataka ya 25, mkatishaji akasema labda ukate ya kesho asubuhi. Basi kwa shingo upande nikaongeza 10,000/- nikapewa hio ya elf 35.

Kinachoniuma zaidi ni pale jamaa yangu niliyekuwa nasafiri nae alifika bado robo saa tuanze kuingia melini alikata tiketi ya 25,000/-. Kabla hajafika nilimwambia awahi asijekuta na hizo za 35 zimeisha akaambulia za 50.

Hilo nikalimezea tu nikasema bas labda sio bahati yangu. Kilichoniuma zaidi na zaidi ni huko Zenji, nilifika saa moja kasoro asubuhi kukata tiketi na hapo pia naambiwa hakuna za elfu 25 kwenye boti ya saa tatu zipo za 35, 50 na 60 tu. Kwa shingo upande tena nikakata hio 35.

Jamaa yangu kama kawaida yake kachelewa chelewa badae anakuja bandarini ananipigia simu namwambia nipo humu VIP Lounge, anasema kwani sikupata za 25? Mbona yeye kakata sasa hivi kwa 25!

Kwa kweli nimeumia sana kwani bajeti yangu imeharibiwa na hawa wakata tiketi, hivyo naomba sana SUMATRA komesheni hii hali, yaani wanalazimisha kuuza za bei ya juu kwanza halafu ndio wauze economy. Na wanadanganya kwa kusema zimeisha. Sumatra tusaidieni kwa hili tafadhali.

Nawasilisha wakuu!
mkuu kama ticket imeandikwa bei hiyo unayolalamikia i.e 35000 ihifadhi na ikiwezekana hayo malalamiko yako yaweke katika maandishi na uyawasilishe SUMATRA (kama hutojali) unaweza kuwa mkombozi wa tatizo hilo kwa watapeliwaji wengi
 
Pale Zenji ukitokea Ferry ni umbali wa kama Mlandizi tu,
Ilifaa tulipe Buku tu kama tunavyolipa kwenda Mlandizi
Tehteh.... Haya bwana.. basi twende Mlandilizi kwa boti!!! Aina ya usafiri inachangia..Basi na kwenda Mwanza kwa ndege twende kwa 50K. Hahaha. Joking anyway
 
Mwenye contacts za sumatra aweke hapa niwaende hewani
 
Mimi mwenyewe huwa najiuliza kwa nini Sumatra hawapangi nauli za boti kwenda Zanzibar wakati hilo ni jukumu lao kisheria.

Vv
 
Back
Top Bottom