SUMA JKT na sababu ya kuanzishwa kwake

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,642
698,000
SUMA JKT Ni kifupi Cha neno;- "Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa " kifupi ndio SUMA JKT,

Shirika hilo limesajiliwa Kama Shirika la la Ulinzi ndio maana inaitwa SUMA JKT Guard Limited,

Kiuhalisia hawaitwi askari wanaitwa walinzi wa SUMA JKT,

Kuanzishwa kwa JKT, kulitokana na mawazo ya Umoja wa Vijana wa Chama cha TANU (TANU Youth League),

Katika Mkutano wao Mkuu uliofanyika mjini Tabora tarehe 25 Aug 62, chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo, hayati Joseph Nyerere.

Tarehe 19 Apr 63, Baraza la Mawaziri la Tanganyika chini ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,

Lilipitisha Azimio la umoja wa vijana wa TANU na kuamua kwa kauli moja kuazishwa JKT mnamo tarehe 10 Jul 1963. Kundi la kwanza lilipata mafunzo katika kambi ya Mgulani Dar es salaam likiwa na jumla ya vijana 11 toka wilaya 11 tofauti.

Vijana hao wa mwanzo walikuwa makatibu wa umoja wa vijana ambao walikwishapelekwa na TANU huko Yugoslavia mwaka 1962, kuchukua mafunzo ya uongozi wa vijana.

Baadhi ya vijana hao watangulizi ni Bi. Z. Kiango, Bw. S. Chale, Bw. P. Lwegarulira, Bw. R. Kamba, Bw. H. Ngalason, Bw, J.Ndimugwango, Bi. M. Mhando (Senior Guide), Bw. D. S. Msilu (Master), Mr ES Mwakyambiki, (Senior Master) na Mr AI Msonge (Master), Mr LM Mitande.

Ulipofika mwezi Agosti, 1963 kikundi kingine cha watu watano kikiwa na Bw. S. Desai, Bw. E. Simkone, Bw. J.

Mwanimlele (Asst Master) na Bw. A. A Moyo (Asst Master) kilijiunga na kupata pia mafunzo ya uongozi.

Kwenye uzinduzi wa JKT, Mwalimu Nyerere alisema Umuhimu wa JKT unatokana na Taifa kuhitaji huduma ya vijana na vijana kuitikia wito huo wa kulitumikia Taifa lao kwa jukumu lolote lihitajiwalo.

SHERIA YA KUANZISHWA KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA MAREKEBISHO YAKE

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (Nationa Service Act) ambayo ni sheria No 16 ya mwaka 1964.

Sheria hii inatoa uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kuandikisha vijana wa kulitumikia Jeshi hilo.

Aidha, sheria hii imeendelea kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitajio na baadhi ya marekebisho hayo ni:-

1. Marekebisho ya mwaka 1966

Tangu lilipoasisiwa JKT lilikuwa linaandikisha vijana wa kujitolea wenye elimu ya darasa la saba tu.

Ilipofika mwaka 1966, ilionekana kuwa, kuna umuhimu wa vijana wasomi wenye elimu zaidi ya kidato cha nne kulitumikia JKT.

Hivyo, sheria ilirekebishwa ili kulipa JKT nguvu za kisheria ili liweze kuandikisha vijana wenye taaluma zaidi ya kidato cha nne kwa mujibu wa sheria (Compulsory).

Marekebisho mengine ni ya mwaka 1975 ambapo, ili kuimarisha ulinzi wa Taifa, JKT liliungana rasmi na JWTZ mwaka 1975 hivyo kulifanya JKT kuwa moja ya Kamandi zilizochini ya JWTZ.

Sambamba na marekebisho hayo, shughuli za JKT ziliwekwa bayana kuwa ni:-

a).Kuwafundisha vijana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulitumikia Taifa katika nyanja za kijamii, maendeleo ya uchumi na ulinzi wa Taifa.

b). Kutoa mafunzo ya msingi ya Jeshi kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufikia sifa ya kujiunga katika vyombo vya Ulinzi na Usalama Kama vile;- JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Magereza.

Japokuwa JKT katika shughuli za malezi ya vijana lilijihusisha na uzalishaji mali pia,

Shughuli hii ilipata nguvu zaidi mwaka 1981 pale ambapo Shirika la Uzalishaji Mali au kwa kifupi SUMA JKT lilianzishwa kisheria kupitia “The Corporation Sole Establishment Act”.of 1974,

Awali, nia ya kuanzishwa SUMA JKT ilikuwa ni kusaidia miradi ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji ili iweze kuzalisha zaidi na kwa faida na hivyo kuisaidia serikali katika kupunguza matumizi katika kuendesha shughuli za JKT.

Baadae ndio ikaanzishwa kampuni ya ulinzi ili wale wayakao baki baada ya wengine luchaguliwa kuwa Polisi, Askari magereza, Usalama wa Taifa, na JWTZ wasiende tu nyumbani bali waajiliwe na kuwa walinzi kwenye mashirika mbalimbali,

Kinachofanyika wewe Kama una ofisi yako na unahitaji walinzi wa SUMA JKT unakwenda ofisi za JKT ndani yake ndio Kuna ofisi zinazo husika na SUMA JKT kwasababu Suma JKT ipo Chini ya JKT ukifika unaomba walinzi unao wataka unaambiwa bei munakubaliana na ofisi halafu wanakuja kukulinda,

Wewe unalilipa Shirika la SUMA JKT halafu Shirika ndio linawalipa walinzi wake Asilimia kadhaa ya kile ulicho lipa na kiasi kingine kinaenda kwa Shirika la SUMA JKT.

Screenshot_20220206-101057.jpg
 
SUMA JKT Ni kifupi Cha neno;- "Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa " kifupi ndio SUMA JKT,
Shirika hilo limesajiliwa Kama Shirika la la Ulinzi ndio maana inaitwa SUMA JKT Guard Limited,
Kiuhalisia hawaitwi askari wanaitwa walinzi wa SUMA JKT,
Kuanzishwa kwa JKT, kulitokana na mawazo ya Umoja wa Vijana wa Chama cha TANU (TANU Youth League),
Katika Mkutano wao Mkuu uliofanyika mjini Tabora tarehe 25 Aug 62, chini ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo, hayati Joseph Nyerere.
Tarehe 19 Apr 63, Baraza la Mawaziri la Tanganyika chini ya Rais wa Jamhuri ya Tanganyika na Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere,
Lilipitisha Azimio la umoja wa vijana wa TANU na kuamua kwa kauli moja kuazishwa JKT mnamo tarehe 10 Jul 1963. Kundi la kwanza lilipata mafunzo katika kambi ya Mgulani Dar es salaam likiwa na jumla ya vijana 11 toka wilaya 11 tofauti.
Vijana hao wa mwanzo walikuwa makatibu wa umoja wa vijana ambao walikwishapelekwa na TANU huko Yugoslavia mwaka 1962, kuchukua mafunzo ya uongozi wa vijana.
Baadhi ya vijana hao watangulizi ni Bi. Z. Kiango, Bw. S. Chale, Bw. P. Lwegarulira, Bw. R. Kamba, Bw. H. Ngalason, Bw, J.Ndimugwango, Bi. M. Mhando (Senior Guide), Bw. D. S. Msilu (Master), Mr ES Mwakyambiki, (Senior Master) na Mr AI Msonge (Master), Mr LM Mitande.
Ulipofika mwezi Agosti, 1963 kikundi kingine cha watu watano kikiwa na Bw. S. Desai, Bw. E. Simkone, Bw. J. Mwanimlele (Asst Master) na Bw. A. A Moyo (Asst Master) kilijiunga na kupata pia mafunzo ya uongozi.
Kwenye uzinduzi wa JKT, Mwalimu Nyerere alisema Umuhimu wa JKT unatokana na Taifa kuhitaji huduma ya vijana na vijana kuitikia wito huo wa kulitumikia Taifa lao kwa jukumu lolote lihitajiwalo.

SHERIA YA KUANZISHWA KWA JESHI LA KUJENGA TAIFA NA MAREKEBISHO YAKE

Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa kwa sheria ya Jeshi la Kujenga Taifa (Nationa Service Act) ambayo ni sheria No 16 ya mwaka 1964.
Sheria hii inatoa uwezo wa Jeshi la Kujenga Taifa kuandikisha vijana wa kulitumikia Jeshi hilo.
Aidha, sheria hii imeendelea kufanyiwa marekebisho kutokana na mahitajio na baadhi ya marekebisho hayo ni:-

1. Marekebisho ya mwaka 1966

Tangu lilipoasisiwa JKT lilikuwa linaandikisha vijana wa kujitolea wenye elimu ya darasa la saba tu.
Ilipofika mwaka 1966, ilionekana kuwa, kuna umuhimu wa vijana wasomi wenye elimu zaidi ya kidato cha nne kulitumikia JKT.
Hivyo, sheria ilirekebishwa ili kulipa JKT nguvu za kisheria ili liweze kuandikisha vijana wenye taaluma zaidi ya kidato cha nne kwa mujibu wa sheria (Compulsory).
Marekebisho mengine ni ya mwaka 1975 ambapo, ili kuimarisha ulinzi wa Taifa, JKT liliungana rasmi na JWTZ mwaka 1975 hivyo kulifanya JKT kuwa moja ya Kamandi zilizochini ya JWTZ.
Sambamba na marekebisho hayo, shughuli za JKT ziliwekwa bayana kuwa ni:-
a).Kuwafundisha vijana wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kulitumikia Taifa katika nyanja za kijamii, maendeleo ya uchumi na ulinzi wa Taifa.
b). Kutoa mafunzo ya msingi ya Jeshi kwa vijana kwa lengo la kuwawezesha vijana hao kufikia sifa ya kujiunga katika vyombo vya Ulinzi na Usalama Kama vile;- JWTZ, Polisi, Usalama wa Taifa na Magereza.
Japokuwa JKT katika shughuli za malezi ya vijana lilijihusisha na uzalishaji mali pia,
Shughuli hii ilipata nguvu zaidi mwaka 1981 pale ambapo Shirika la Uzalishaji Mali au kwa kifupi SUMA JKT lilianzishwa kisheria kupitia “The Corporation Sole Establishment Act”.of 1974,
Awali, nia ya kuanzishwa SUMA JKT ilikuwa ni kusaidia miradi ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji ili iweze kuzalisha zaidi na kwa faida na hivyo kuisaidia serikali katika kupunguza matumizi katika kuendesha shughuli za JKT.
Baadae ndio ikaanzishwa kampuni ya ulinzi ili wale wayakao baki baada ya wengine luchaguliwa kuwa Polisi, Askari magereza, Usalama wa Taifa, na JWTZ wasiende tu nyumbani bali waajiliwe na kuwa walinzi kwenye mashirika mbalimbali,
Kinachofanyika wewe Kama una ofisi yako na unahitaji walinzi wa SUMA JKT unakwenda ofisi za JKT ndani yake ndio Kuna ofisi zinazo husika na SUMA JKT kwasababu Suma JKT ipo Chini ya JKT ukifika unaomba walinzi unao wataka unaambiwa bei munakubaliana na ofisi halafu wanakuja kukulinda,
Wewe unalilipa Shirika la SUMA JKT halafu Shirika ndio linawalipa walinzi wake Asilimia kadhaa ya kile ulicho lipa na kiasi kingine kinaenda kwa Shirika la SUMA JKT.

View attachment 2109794
Unapenda kuzungumzia KILA KITU hata ambacho hukijui vizuri just for the sake of SIFA na LIKES.

Suma JKT haijawahi kuanzishwa kama kampuni ya Ulinzi mwanzoni.

Hata jina lenyewe Ni SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI- JKT.

Mission ya Kwanza ya JKT Ni kuzalisha Mali na ndio maana wanajihusisha na KILIMO, UJENZI, FURNITURE, UUZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO n.k.

Ila miaka ya 2009 wakati sekta ya Ulinzi inaanza kukua, makampuni mengi yakawa yanawatumia Wamasai.

Baadaye, makampuni yakaanza kutaka walinzi waliopita JKT Happ ndio ikaanzishwa SUMA JKT Guard kama kampuni chini ya SUMA JKT Group.

Suma JKT kama kampuni ya Ulinzi wakawa wana-recruit vijana wale waliokuwa wanaenda JKT kwa kujitolea halafu hawapati nafasi kwenye vyombo vya ulinzi kutokana na sababu kadhaa has Elimu.

I'll baada ya Magufuli kuingia madarakani, akaanza kujifanya anabana matumizi na hivyo kwakuwa SUMA JKT mishahara midogo maana yake hata wateja wao hutoa pesa kidogo, Magufuli akasema wapewe malindo yote ya serikali walinde.

Happ SUMA JKT wakaanza kupungukiwa sana manpower maana walipewa malindo mengi mno.

Walichofanya SUMA JKT Ni kuanza kuchukua watu mtaani na kuwapigisha tizi huko kimbiji halafu wanawaajiri.

Vile vile, SUMA JKT wamekuwa.wakichukua sana vijana huko vijijini waliopiga mgambo na.kuwaajiri hasa Dar es Salaam.

Kwahiyo SUMA JKT Ni Group of companies yenyewe makampuni mengi tu Wala siyo Ulinzi peke yake.

Tena siku hizi wanna kampuni mpaka ya usafi.

Kuhusu kazi zao: SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JKT
 
Hapo Kuna wahasibu , wahandisi etc .Bora umenyoosha maelezo brother ili watu wafahamu kwenye SUMA JKT sio wrote waganga njaa kama mlivyozoea kwa hao walinzi wasio na nidhamu
 
Unapenda kuzungumzia KILA KITU hata ambacho hukijui vizuri just for the sake of SIFA na LIKES.

Suma JKT haijawahi kuanzishwa kama kampuni ya Ulinzi mwanzoni.

Hata jina lenyewe Ni SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI- JKT.

Mission ya Kwanza ya JKT Ni kuzalisha Mali na ndio maana wanajihusisha na KILIMO, UJENZI, FURNITURE, UUZAJI WA PEMBEJEO ZA KILIMO n.k.

Ila miaka ya 2009 wakati sekta ya Ulinzi inaanza kukua, makampuni mengi yakawa yanawatumia Wamasai.

Baadaye, makampuni yakaanza kutaka walinzi waliopita JKT Happ ndio ikaanzishwa SUMA JKT Guard kama kampuni chini ya SUMA JKT Group.

Suma JKT kama kampuni ya Ulinzi wakawa wana-recruit vijana wale waliokuwa wanaenda JKT kwa kujitolea halafu hawapati nafasi kwenye vyombo vya ulinzi kutokana na sababu kadhaa has Elimu.

I'll baada ya Magufuli kuingia madarakani, akaanza kujifanya anabana matumizi na hivyo kwakuwa SUMA JKT mishahara midogo maana yake hata wateja wao hutoa pesa kidogo, Magufuli akasema wapewe malindo yote ya serikali walinde.

Happ SUMA JKT wakaanza kupungukiwa sana manpower maana walipewa malindo mengi mno.

Walichofanya SUMA JKT Ni kuanza kuchukua watu mtaani na kuwapigisha tizi huko kimbiji halafu wanawaajiri.

Vile vile, SUMA JKT wamekuwa.wakichukua sana vijana huko vijijini waliopiga mgambo na.kuwaajiri hasa Dar es Salaam.

Kwahiyo SUMA JKT Ni Group of companies yenyewe makampuni mengi tu Wala siyo Ulinzi peke yake.

Tena siku hizi wanna kampuni mpaka ya usafi.

Kuhusu kazi zao: SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JKT
Upo sahihi , kabisa
 
Unakurupuka sna.
 
Magereza pia wanao kampuni Kama hiyo,kwa polisi maafisa wa staafu wengi ndio mwamefungua makampuni yao binafsi,ningependa na polisi wawe na shilika lao laulinzi Kama hili japo Kuna auxiliary polisi,yaani polisi wasaidizi.
 
Auxiliary police zipo nyingi tu lakini ziko kiserikali zaidi ni ngumu kuwakuta kwenye mzunguko nje ya serikali
 
mwanzilishi wa suma jkt alikuwa mkuu wa majeshi Mwamnyange inshortly haina muda mrefu toka imeanzishwa na haidili na ulinzi pekee mpaka kilimo na uuzaji wa matrekta,usafi,ujenzi nk
 
vipi mishahara yao kiasi gani,wasijekuwa wanalipwa kama makampuni mengine ya ulinzi
 
mwanzilishi wa suma jkt alikuwa mkuu wa majeshi Mwamnyange inshortly haina muda mrefu toka imeanzishwa na haidili na ulinzi pekee mpaka kilimo na uuzaji wa matrekta,usafi,ujenzi nk
Mengine yalifuata baadae baada ya kampuni kukua na kushamiri
 
Back
Top Bottom