pombe kali
JF-Expert Member
- Jun 28, 2014
- 267
- 525
Tafadhali bandiko hili liwafikie uongozi wa Suma JKT, hawa askari wanashindwa maadili. Wanapata wakati mgumu wa kuishi huku uraiani.
Kwanza hawalipi nauli kwenye daladala wakiulizwa wanasema wao ni JKT. Ninachojua mimi Suma JKT ni kampuni na wala sio kikosi chochote cha ulinzi na usalama.
Nimeshuhudia zaidi ya mara mbili wakigoma kulipa nauli na kuanzisha fujo. Tukawasiliana na kikosi cha usalama barabarani ambapo walitushauri kuwapeleka kituo cha polisi. Leo tena nimeshuhudia dereva wa daladala akiwakwepa walikuwa kituoni wakisubiri gari ambapo walikimbiza gari mpaka kwenye foleni ila abiria tuliweza kuwadhibiti.
Tafadhali uongozi wa Suma JKT ufuatilie hili ikiwezekana wavae majina au namba ambazo zitawatambulisha kuturahisishia kuripoti matukio.
Asante