Suluhisho la foleni katika jiji la Dar

Suluhisho la foleni katika jiji la Dar

K.Msese

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
2,388
Reaction score
3,049
Ili kupunguza foleni katika jiji la Dar es Salaam, nashauri Serikali itawanye makao makuu za Wizara katika mikoa mbalimbali nchi nzima! Mkoa wa Dar es Salaam kipekee kabisa umekaliwa na wizara zote, hivyo wafanyakazi na taasisi zake wapo Dar es Salaam! Mabenki, na makampuni mengine mengi yanaona ni rahisi na faida yakifunguliwa Dar es Salaam kulikoni yangefunguliwa mikoani ambapo purchasing power ya wananchi wa huko ipo chini!

Endapo Wizara zitatawanywa nchi nzima, at least wizara tatu kila mwaka itaondoa watumishi wengi Dar es Slaam na familia zao, hence kupunguza idadi ya magari barabarani! Pia itafanya mabenki na taasisi zingine kufungua matawi kwenye hiyo mikoa kama siyo kuhamia kabisa! Zoezi hili likifanikiwa, Dar es Salaam kutabakiwa na wizara na taasisi za umma chache zenye umuhimu wa kubakia Dar!

Dar es Salaam ina foleni kwakuwa, idadi ya wakaazi wake inazidi kuongezeka siku hata siku lakini miundo mbinu ni ileile, haiongezeki! Umiliki wa magari limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa karibu kila mtu anayejishughulisha anamiliki gari kama siyo magari! Juu ya hilo ni kuwa, karibu wote tukiamka asbuhi tunaelekea uelekeo mmoja wa mjini, na woote tunatawanyika kutoka mjini ikifika jioni! Ijapo kumekuwa na jitihada nyingi kutengeneza barabara za michepuko, lakini taratibu kadri muda unavyoenda na zenyewe zinazidiwa! Kutoka Mbezi hadi mjini au mjini to mbezi ya Kimara inaweza ikuchukue hadi masaa matatu?. Muda wa Abood kutoka Dar hadi Morogoro!

Mtu wa mikoa mingine, akitaka jambo lake wizarani itamlazimu aende Dar, lakini mkaazi wa Dar ni daladala tu ya kumfikisha mjini, na ana uwezo wa kutembea wizara karibu zote kwa mguu na akazimaliza! Kwa hali hii, wakaazi wa mikoa mingine hawatendewi haki licha mzunguko wao mdogo wa hela wa mikoani itabidi achukue basi, treni au ndege na akodishe hoteli akiwa Dar hadi amalize mambo yake. Kuna wakaazi wengi wa Dar hawajawahi kufika Kigoma, Rukwa, Kagera, Ruvuma nk kwakuwa hamna jambo linalomfanya aende mikoa hiyo? Endapo mikoa hiyo ingepelekewa Wizara zikahamia huko, basi kama hajaenda kusalimia basi kuna jambo atalifuata katika wizara ilio katika hiyo mikoa!

Ushauri ni kuwa, katika kuhamisha huku kwa Wizara, zilenge ile mikoa yenye mwamko mdogo wa kimaendeleo ya kijamii na uchumi! Wizara ya Elimu, ihamie Kigoma , Mambo ya Ndani ihamie Dodoma, Maji Nishati ihamie Singida nk nk? Kwa hali hiii hata wakazi wa huko wataneemeka na mzunguko wa fedha kutoka kwa wahamiaji wapya!

Kuna umuhimu gani wa wizara zoote kuwa jijini Dar es Salaam?
Ofisi za Balozi mbalimbali, kuna ulazima wa wao wote kukaa hapa Dar?
 
Na maeneo ya biashara pamoja na makazi kuwa nje ya mji, kwa mfano kariakoo ime over load, kwa nini eneo la kariakoo na posta kusiwe jiji la utalii? Wafanya biashara wadogo wadogo na.maduka yote ya kariakoo yahamishwe nje mji.

Na.maeneo yatakayo vumbuliwa lihakikishwe miundo mbinu ya maji machafu na.maji safi na road zinafika kwanza
 
Na maeneo ya biashara pamoja na makazi kuwa nje ya mji, kwa mfano kariakoo ime over load, kwa nini eneo la kariakoo na posta kusiwe jiji la utani? Wafanya biashara wadogo wadogo na.maduka yote ya kariakoo yahamishwe nje mji.

Na.maeneo yatakayo vumbuliwa lihakikishwe miundo mbinu ya maji machafu na.maji safi na road zinafika kwanza

Wazo zuri sana, tuombe wahusika wayaone
 
Nadhani kasome kwanza maana ya makao makuu ya nchi! kiutaratibu wizara zote zinakuwepo pale ambapo ofisi ya Rais ipo ili iwe rahisi kwake kuwa na vikao na watendaji wake mara kwa mara hivyo hivyo kwa mashirika makubwa ya Umma. Suluhisho la foleni ni miundombinu tu
 
Ngumu hiyo

mkuu ugumu wake unakujaje hapo!mfano tuchukulie tunaamua kuihamishia wizara ya mali asili na utalii (kama itakuwepo) arusha...wizara ya kilimo na mifugo (kama itakuwepo pia) mwanza!si itasaidia....maana naamini na wewe utahamia Sumbawanga ambako tutaihamishia wizara ya michezo na kamati za ufundi (hii itakuwepo)!!!
 
pia sioni sababu ya kuacha malori yaingie mjini kwa maoni yangu tuimarishe reli zetu na kujenga mpya ili ziondoe mizigo hasa iendayo mikoani katika ya mji ili malori yaichukue kutokea miji ya pembezoni lakini pia litengenezwe bomba mfano wa lile la tazama ili mafuta yasafirishwe kwa njia hiyo hadi mikoani ili malori yasije dar kusema ukweli huwez pata suluhisho la folen dar bila kupunguza na kudhibiti idadi ya mgari yaingiaya mjiini
 
Nadhani kasome kwanza maana ya makao makuu ya nchi! kiutaratibu wizara zote zinakuwepo pale ambapo ofisi ya Rais ipo ili iwe rahisi kwake kuwa na vikao na watendaji wake mara kwa mara hivyo hivyo kwa mashirika makubwa ya Umma. Suluhisho la foleni ni miundombinu tu

Hata kama uwezo wa kutawanya makao mkuu au sehemu za biashara au sehemu za viwanda vinaweza kufanyika kokote, tatizo sio barabara tatizo ni mfumo wa mji.

Lile soko la kariakoo kwa sasa hivi linahitajika kuondoka na kwenda nje ya mji, kariakoo kuna nuka na ndio chanzo cha traffic
 
Suluhisho pekee ni kuhamia dodoma... Naona uhamiaji wa dodoma ungeenda kwa phases, atlst kila mwaka walau wizara 2 ziwe zimehama Dar. Kwa kiwango kikubwa miundombinu rafiki imeshajengwa Dodoma. Suala ni uamuzi mgumu tu wa kuachana na upepo wa baharı na kuhamia kwa wagogo.
 
Bara bara za mabasi yaendayo kasi, zitumike na daldala, daladala hazina vituo zinafunga barabara.
 
mkuu ugumu wake unakujaje hapo!mfano tuchukulie tunaamua kuihamishia wizara ya mali asili na utalii (kama itakuwepo) arusha...wizara ya kilimo na mifugo (kama itakuwepo pia) mwanza!si itasaidia....maana naamini na wewe utahamia Sumbawanga ambako tutaihamishia wizara ya michezo na kamati za ufundi (hii itakuwepo)!!!

Ktk mipango miji kuna umuhimu wa centralization. Gharama za kuendesha shughuli za serikali zikiwa sehemu moja ni ndogo kuliko zikiwa mbali mbali kwani kuna shughuli nyingi zinategemeana . Sina hakika kama mfumo wako unatumika popote Africa
 
suluhisho lingine ni kuanzisha mfumo wa shifti. Masaa ya kazi yaanze saa kumi na mbili asubuhi hadi saaa tano asubuhi...kumaliza kati ya saa nane mchana na moja usiku. Yaani kuwe na watu wanaanza saa kumi na mbili..wengine saa moja ...saa mbili n.k. Naona hii itasaidia kupunguza foleni.
 
Nadhani kasome kwanza maana ya makao makuu ya nchi! kiutaratibu wizara zote zinakuwepo pale ambapo ofisi ya Rais ipo ili iwe rahisi kwake kuwa na vikao na watendaji wake mara kwa mara hivyo hivyo kwa mashirika makubwa ya Umma. Suluhisho la foleni ni miundombinu tu

Wakati naenda kusoma, nielekeze makao makuu ya nchi yapo Dodoma au Dar es Slaam?
 
Ktk mipango miji kuna umuhimu wa centralization. Gharama za kuendesha shughuli za serikali zikiwa sehemu moja ni ndogo kuliko zikiwa mbali mbali kwani kuna shughuli nyingi zinategemeana . Sina hakika kama mfumo wako unatumika popote Africa

Kwa ajili ya kukuwa kwa teklojia ya Tehama, vingi vimerahishwa.....hata mikutano inaweza kufanyika kwa njia ya mtandao. Kutumiana documents kwa email nk kuliko kutumia mesenja
 
Kutawanya wizara mikoani mmma!!! mmaa!!! fikiria mtu anayehitaji huduma wizara ya fedha na elimu zote zipo magogoni, fikiria kama ikitokea moja iwe Kigoma na nyingine Mtwara
 
kama wana ccm watagundua hilo wazo limetolewa na mtu wa chama pinzani lazima watalibishia japokuwa ni wazo zuri na inawezekana Makufuli akalifanyia kazi
 
mkuu ugumu wake unakujaje hapo!mfano tuchukulie tunaamua kuihamishia wizara ya mali asili na utalii (kama itakuwepo) arusha...wizara ya kilimo na mifugo (kama itakuwepo pia) mwanza!si itasaidia....maana naamini na wewe utahamia Sumbawanga ambako tutaihamishia wizara ya michezo na kamati za ufundi (hii itakuwepo)!!!
Samahani Zamaulid naona tunachokozana hahahaha
 
Last edited by a moderator:
Twahamia Dodoma, hujasikia?

hata tukihamia Dodoma, tutazirundika wizara zote huko? Ishu ni kuondoa foleni Dar na kutawanya wizara mikoani ili fursa na ugumu uwe sawa kwa mikoa yote! Wizara zenye umuhimu wa kubakia DAr basi ziendelee kubakia
 
Back
Top Bottom