Suleiman Kova ananikumbusha umuhimu wa kutenda haki

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Huyu mzee aliwika sana enzi akiwa polisi na kila mtu alimfahamu kwa wema au ubaya

Leo nimeonana naye maeneo flani nikashindwa kujua huu unyenyekevu alizaliwa nao au ameupata uraiani? Nikiwaangalia vijana aliowasweka ndani kwa sababu za kisiasa wanavyonawiri najiuliza yeye alilipwa nini?

Ukimwona utagundua kuwa watu hawakuogopi wewe bali wanaogopa mamlaka iliyopo nyuma yako na ukiipoteza hata wakukusalimia unaweza usikutane nao.

Lakini pia kwa wenzetu mliopo kwenye madaraka makubwa jipangeni kuja kuishi uraiani maana yaonekana hata mishahara ya serikali na pensheni siyo kubwa......Ni muda mfupi sana kwa wazee kama hawa kufulia, it's like wametelekezwa.....

Muroto get prepared kuja kuishi kitaa la sivyo utajuta kufahamika kwenye tv....ukipanda pikipiki hata watoto wanakwita mzee kova yuleee, mzee mroto yuleeeeeee.

Jitahidini kuhifadhi adhi zenu na iwe mwiko kwenu kuajiriwa na kutumwatumwa na mabeberu Bora mjiajiri hata kwa kulima ila siyo kuja kukimbizwa na hindiz mjini....

Sijui ntaeleweka....aaaahaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikutana na Kova pale Best Bite Namanga sikuamini yaani kapauka na makengeza yamezidi..Hizi kazi nyengine zina laana ya kudumu yaani hata ujilimbikizie vipi siku ukistaafu tu unapigika gafla

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda kama kova mwingine kova nimoja katika ya makanda tajiri kabisa ana hotel 3 hapa town mmoja iko pale magomeni hospital opposite na na dawasco
 
Hawa watu hufanya kazi ki-uonevu mno wakisahau kuwa, "No one is indispensable nor permanent anywhere". Hata wale watawala wanaong'ang'ania madarakani iko siku wanaondoka tu hata kwa mauti.
 
Nilikutana na Kova pale Best Bite Namanga sikuamini yaani kapauka na makengeza yamezidi..Hizi kazi nyengine zina laana ya kudumu yaani hata ujilimbikizie vipi siku ukistaafu tu unapigika gafla

Sent using Jamii Forums mobile app

Kova alionekana kwenye msiba wa marehem kibonde akiwa vyema kabisa,kuliko hata alivyokuwa mtumishi wa polisi.

Au amekutana na huo mpauko baada ya hapo???
 
Kova kufulia bado sana Mzee, katika watumishi wa Jeshi la Polisi waliozichuma iwe kwa njia halali au haramu ni mmoja katibya waliojiwekeza vizuri kuanzia kwa watoto zake kwenye familia kwa kuwapangia mstari ulionyooka kiasi kwamba kupotea waamue wao ila Mzee alitumia nafasi yake vizuri kuwainua na yeye mwenyewe anavitega uchumi vyake. Sio wale watumishi wa baada ya Mafao tunaanza kuombwa bia Bar kwa hilo namsifu.
 
Kova yupo vizuri kiuchumi, hata utumishi wake ulikua vizuri, tatizo kazi ya Polisi ina changamoto nyingi kiasi kwamba hata kibaka hataki kulazwa ndani na kufikishwa mahakamani.
Mwacheni apumzike maana sasa ameshavua magwanda
 
Hivi yule mkenya wa Kova wa issue ya Ulimboka alimtoa Segerea kabla ya kustaafu au alimsahau kuozea mahabusu??
 
Huyu mzee aliwika sana enzi akiwa polisi na kila mtu alimfahamu kwa wema au ubaya

Leo nimeonana naye maeneo flani nikashindwa kujua huu unyenyekevu alizaliwa nao au ameupata uraiani? Nikiwaangalia vijana aliowasweka ndani kwa sababu za kisiasa wanavyonawiri najiuliza yeye alilipwa nini?

Ukimwona utagundua kuwa watu hawakuogopi wewe bali wanaogopa mamlaka iliyopo nyuma yako na ukiipoteza hata wakukusalimia unaweza usikutane nao.

Lakini pia kwa wenzetu mliopo kwenye madaraka makubwa jipangeni kuja kuishi uraiani maana yaonekana hata mishahara ya serikali na pensheni siyo kubwa......Ni muda mfupi sana kwa wazee kama hawa kufulia, it's like wametelekezwa.....

Muroto get prepared kuja kuishi kitaa la sivyo utajuta kufahamika kwenye tv....ukipanda pikipiki hata watoto wanakwita mzee kova yuleee, mzee mroto yuleeeeeee.

Jitahidini kuhifadhi adhi zenu na iwe mwiko kwenu kuajiriwa na kutumwatumwa na mabeberu Bora mjiajiri hata kwa kulima ila siyo kuja kukimbizwa na hindiz mjini....

Sijui ntaeleweka....aaaahaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwenyewe nimekutana nae leo maeneo Fulani Arusha kila meza anapita anasalimia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom