Sugu: Sitaacha kuchana mistari kamwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sugu: Sitaacha kuchana mistari kamwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 5, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, Mr. II au Sugu (CHADEMA), ambaye kabla ya kuchaguliwa katika wadhifa huo alikuwa akifanya harakati za utetezi kupitia medani ya muziki wa kizazi kipya amebainisha kuwa hataacha kudondosaha mistari licha ya sasa kuongeza majukumu.
  "Kaka siwezi kuacha kuchana mistari hata siku moja, mimi nilianzia huko na kazi uliiona, kwa sasa kitakachokuwa kinafanyika ni kuangalia kama kuna sehemu wananchi wa jimbo hili wanahitaji fedha kwa ajili ya kazi fulani ya maendeleo, mbunge naenda pale nashusha vesi kinachopatikana kinaingizwa kwenye maendeleo" alisema.

  Sugu alitoa kauli hiyo ya matumaini jijini hapa jana, katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, baada ya mashabiki na wadau wengi wa muziki wa kizazi kipya, kuonyesha hofu kuwa msanii huyo hawezi tena kuigeukia fani yake baada ya kuukwaa uheshimiwa.

  Alisema kuwa sasa kitakachokuwa kikifanyika ili kuendeleza harakati zake kupitia muziki ni kutofanya maonyesho ya kibiashara kama ilivyokuwa awali, kwa kuwa sasa majukumu ya kuwatumikia wananchi yameongezeka.

  "Huwezi kwa sasa kusikia Sugu yuko mkoani Arusha, Tanga au Dar es Salaam, kwani muda unakuwa mdogo, lakini kama kuna wasanii wanaochipukia wanahitaji ushauri na mambo mengine yahusuyo fani milango iko wazi" alisema Sugu.

  Mbali na Sugu kufanikiwa kubahatika kupata nafasi ya kuwa mwakilishi wa wananchi katika taasisi nyeti ya kutunga sheria hapa nchini, pia kuna idadi lukuki ya wasanii waliobahatika kupata nafasi hiyo katika bunge hili la 10.

  Kutokana na idadi kubwa ya wasanii kuingia katika chombo hicho muhimu, kumefufua matumaini makubwa kwa vijana wanaiojihusisha na sanaa nchini, kwani muda mrefu kumekuwa na kilio kisicho na mwenyewe cha wasanii kunyonywa na baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kutokana na kukosekana sera imara na sheria kali za kuwadhibiti wahujumu wa kazi za sanaa nchini.
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kat ya wasanii wote walioingia mjengoni ni sugu tu ndiye namuamini atafanya maana alionyesha dhamira hyo ktambo
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  wengine ni akina nani? Tafadhali naomba kufahamishwa mi nipo mbali kidogo na mchakato wa wabunge sikuupata vizuri. Tafadhali wataalam nijuzeni.
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  wanawake na mendeleo tusonge mbele........................vicky kamata
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sugu ni waukweli!Amedhamiria kufanya alichotumwa na wananchi!
   
 6. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  asante mkuu kilimasera, aakh huyo vicky mbona nilisha sikia ni chakula ya mkwere muda mrefu? Duh kwa hiyo mkulu kamvuta mama yake mdogo na ridhwani ndani ya mjengoni. Kazi ipo. Any way si tuiombee nchi yetu.
   
 7. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,127
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Wengine ni Augustino Lyatonga Mrema!:thumb:
   
 8. M

  Msindima JF-Expert Member

  #8
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mmhh hii nayo imenichekesha kweli kweli.
   
 9. BABA JUNJO

  BABA JUNJO JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 241
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mie ndo sina Mbavu. Lakini ni kweli Lyatonga ni msanii maana sijui atafanya nini huko mjengoni? Maana huko kuna kazi tu hakuna historia ya eti nilikuwaga naibu waziri Mkuu na Waziri wa mambo ya ndani !!!! Kinachotakiwa ni kazi tu! Maana usifikiri hii mijitu itatoka kwa kuichekea no way!
   
 10. DJ BABU

  DJ BABU JF-Expert Member

  #10
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 210
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sugu mjita wa ukweli acha apeperushe bendera juu,hivi hayumo humu?
   
 11. P

  Paul S.S Verified User

  #11
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Natamani sana kumsikia mzee wa kiraracha ataongea gani mjengoni
   
Loading...