Sugu ang'aka Uwanja wa Ndege wa Songwe kuitwa Jakaya Kikwete

Kuna tatizo gani Uwanja kuitwa Jina la Raisi Jakaya Kiwete? Watanzania mbona tuna matatizo ya akili?! ungeitwa Nelson Mandela, Mugabe, Georgge Bush, Nkurumah mngeshangilia! acheni ushamba, fikirieni jinsi ya kuondoa umasikini wa wananchi tutawaona mnayo akiri na siyo vitu kama hivi!

Unajua kwa watu wa Mbeya mtu mzima kuchekacheka hadharani na kuanguka anguka ilhali ni kiongozi, nia aibu kubwa!!
Sasa uwanja utaitwaje jina la mtu wa jinsi hiyo????

Acheni kujikomba, waiteni watoto wenu Kikwte kama mna mpenda sana!
 
Wewe mla ubwabwa vipi!? Nyerere aliishi,alijenga na kufanya kazi DSM ...tumia akili bwana! Kikwete anaishi,amejenga,na anafanyaia kazi Mbeya???
Alikuja kufanya kazi tu alipomaliza alirudi kwao Butiama!

Zanaki Street, viwanja vya mwalimu nyerere, ukumbi wa mwalimu nyerere n.k wakati Dar ina mashujaa wake ambao hawana hata jina la Shule ya Kata!
 
Jifunze kusoma vitu na kuelewa. Huyo hajakataa jina la Rais kutumika. Alichotaka ni wabunge washirikishwe.

Chadema wanasema Rais hana uhusiano na Mbeya kwa sababu hana nyumba huko!

Two sides of the same coin, kama wamefanya uamuzi ambao yeye anauafiki, ingeleta tofauti gani yeye kuwepo kwenye hicho kikao? Je yeye kama mwana CCM angepinga uwanja kupewa jina la JK?? The point is JK has never and is not liked in Mbeya albeit walishinda "uchaguzi 2010" kwa nini hao wateule wake wameamua ku-impose jina la mtu ambaye hata kwenda huko hapendi??
 
Kwakuwa bagamoyo kutajengwa bandari ya kisasa,bila shaka ipewe jina la J.M.K lakini uwanja wa songwe uitwe Mbeya International Airport.
 
Ataturk - Istanbul, Vaclav Havel - prague, O'Hare - Chicago, Malpensa - Milan, Schipol - Amsterdam, Moi - Mombasa, Charles de Gaulle - Paris, you name it, jina la mji lazima liwepo. Hii ya kusema kiwanja kipewe jina la mji ili mji usikike ni USHAMBA.

Msipoteze muda mwingi wa thamani kujadili mambo mepesi yasiyo na tija. Jadilini jinsi ya kuvutia mashirika ya ndege ya nje yaanzishe safari za kutua hapo.

uwezo wa kuvuta mashirika makubwa kutumia uwanja ule upo, but not under the name proposed.
Mbeya International Airport or Songwe, thats all.
Niomekuuliza kuhusu KIA ukajibu ulivyotaka na si inavyotakiwa.
 
Alikuja kufanya kazi tu alipomaliza alirudi kwao Butiama!

Zanaki Street, viwanja vya mwalimu nyerere, ukumbi wa mwalimu nyerere n.k wakati Dar ina mashujaa wake ambao hawana hata jina la Shule ya Kata!

Kikwete + Wewe = Shehe Ilunga
Mmefundishwa kuamini jambo bila kufikiri....poleni..
 
Two sides of the same coin, kama wamefanya uamuzi ambao yeye anauafiki, ingeleta tofauti gani yeye kuwepo kwenye hicho kikao? Je yeye kama mwana CCM angepinga uwanja kupewa jina la JK?? The point is JK has never and is not liked in Mbeya albeit walishinda "uchaguzi 2010" kwa nini hao wateule wake wameamua ku-impose jina la mtu ambaye hata kwenda huko hapendi??

Unamjua chief Mwailemale wa wanyakyusa?
 
uwezo wa kuvuta mashirika makubwa kutumia uwanja ule upo, but not under the name proposed.
Mbeya International Airport or Songwe, thats all.
Niomekuuliza kuhusu KIA ukajibu ulivyotaka na inavyotakiwa.

Basi uwanja upewe jina la chief wa wanyakyusa. Chief Mwailemale...
 
It would seem as if he owns the Airport. The best you can do is name it after the region where it lays. Why are people always behaving irrationally when it comes to naming National Monuments. What has he done for Tanzania that is remarkable?
 
Two sides of the same coin, kama wamefanya uamuzi ambao yeye anauafiki, ingeleta tofauti gani yeye kuwepo kwenye hicho kikao? Je yeye kama mwana CCM angepinga uwanja kupewa jina la JK?? The point is JK has never and is not liked in Mbeya albeit walishinda "uchaguzi 2010" kwa nini hao wateule wake wameamua ku-impose jina la mtu ambaye hata kwenda huko hapendi??

Sera za chadema zinawapotosha vijana mnasahau kuwa Tanzania ni MOJA...
 
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (CHADEMA) amesema haungi mkono pendekezo la Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya kutaka kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete.

Akizungumza na Tanzania Daima jana jijini Dar es Salaam, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema mapendekezo hayo yametolewa na watu wenye kutaka kujipendekeza kwa mkuu wa nchi badala ya kufikiria kuutangaza Mkoa wa Mbeya katika nyanja ya kimataifa.

Alisema Mbeya ina historia ya kutaka kujitangaza kimataifa na uwanja huo ni fursa pekee ya kufikia malengo hayo aliyoeleza kuwa yanataka kufifishwa na wateule wa rais.

“Siungi mkono uwanja kuitwa kwa jina la JK, tunataka jina litakaloasisi uhalisia wa Mbeya nasi tufahamike kimataifa, kamati ya ushauri ya mkoa chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Norman Sigala ilikurupuka kuleta wazo hilo kabla ya kuwasiliana na wabunge,” alisema.

Alisema hatua hiyo ya Sigala haiwakilishi mawazo ya wananchi bali inawakilisha mawazo ya mtu aliyeteuliwa na kwamba wao wakiwa wawakilishi wa Mkoa wa Mbeya kwa ridhaa ya wananchi hawawezi kukubaliana na suala hilo.

Kauli ya Sugu iliungwa mkono na wabunge wengine wa Mkoa wa Mbeya, ambapo Mchungaji Lukson Mwanjale wa Mbeya Vijijini (CCM) alisema anasikitishwa na hatua hiyo ya kuliwasilisha wazo hilo bila ya kuwashirikisha wabunge.

Alisema wakati wa kikao cha kamati ya ushauri wabunge wengi hawakuwepo na taarifa hizo walizisikia baada ya kusoma kwenye vyombo vya habari.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philip Mulugo ambaye pia ni mbunge wa Songwe, aliomba apewe muda wa kutaka kujua sababu zilizoibua wazo hilo.

Wazo la kuuita Uwanja wa Ndege wa Songwe jina la Rais Jakaya Kikwete linazidi kupata upinzani ambapo awali chama cha NCCR-Mageuzi na kile cha PPT Maendeleo kupitia kwa viongozi wa Mkoa wa Mbeya vilipinga wazo hilo.
dah.!
nnchi hii, kila kitu ni ligi.!!
ila ndo kukomaa kwenyewe kifikra huko..
DC amechemka kutoshirikisha watu muhimu (kuliko hata yeye DC) kama wabunge..
 
It would seem as if he owns the Airport. The best you can do is name it after the region where it lays. Why are people always behaving irrationally when it comes to naming National Monuments.
Exactly!
Hivi ndivyo Tanzania na watu wake inavyoonekana, kama vile inamilikiwa na nyerere!
 
Toba! Lahaula wala kuwata! Ati? Wasema?..ama kweli ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni...

Ukweli ndio huo, kwani hapo Mbeya ana mke? Huku kwetu Hai alikuwa kapela mzunguka mitaani; msione watu wanapata vyeo na kuzunguka na mashangingi huwa wamepitia masahibu makubwa!!
 
Kuna tatizo gani Uwanja kuitwa Jina la Raisi Jakaya Kiwete? Watanzania mbona tuna matatizo ya akili?! ungeitwa Nelson Mandela, Mugabe, Georgge Bush, Nkurumah mngeshangilia! acheni ushamba, fikirieni jinsi ya kuondoa umasikini wa wananchi tutawaona mnayo akiri na siyo vitu kama hivi!

Ni bora uitwe Mwakyembe aliweka nguvu zake mpaka ukawepo.Wa Bagomoyo rukhusa kuitwa JK.Tuachieni uwanja wetu.
 
It would seem as if he owns the Airport. The best you can do is name it after the region where it lays. Why are people always behaving irrationally when it comes to naming National Monuments. What has he done for Tanzania that is remarkable?

Uzi wa kiswahili weye unakoment kimombo wakati imeonekana unaelewa kiswahili ndio maana umeweza kukoment
 
Back
Top Bottom