mr gentleman
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 3,223
- 4,681
Kwanza kabisa natoa pole kwa wafiwa wote kwa msiba wa msanii John Walker.
Pili nasikitika kusema nasikitishwa sana na ambavyo mbunge wa Mbeya mjini Mr Sugu alivyomtelekeza John Walker kiasi aliishi maisha magumu sana mpaka kifo chake.
Mnatakiwa kufahamu John Walker, Mapacha, Mkoloni na G Solo ndio wasanii waliopigana bega kwa bega kuakikisha Sugu anaingia bungeni hiyo ni mwaka 2010. Walijitoa kwa hali na mali kuakikisha Sugu anapata ubunge. Walichangisha michango, walisimama kwenye kampeni bila malipo ili kamanda aingie mjengoni.
Baada ya kuukwaa ubunge John Walker akawa ndio dereva wake wa kwanza wa mbunge Sugu. Walishiriki nae kwenye movement nyingine ya Anti virus ambayo Sugu aliwaaminisha wenzake wanapigania maslahi ya muziki wa bongofleva. Mwisho wa siku Sugu alipppata pesa yake aliyodhulumiwa na Ruge akaenda kimya kimya kupatana na Ruge kisha mzozo ukaanzia hapo. Akawapiga chini rafiki zake wote waliojiita vinega akiwemo dereva wake John Walker akamwondoa kwenye kazi ya udereva na Walker akarudi mtaani kubangaiza kwa kazi ya ufundi wa magari na kuchomelea vyuma.
Tangia anaumwa mpaka anakata roho marehemu akuwai kupata msaada wowote wala salamu ya pole toka kwa rafiki yake kipenzi wa zamani Sugu.
Ama kweli maskini akipata...........