SUGU adai yeye ndiye muasisi wa Bongofleva

Wakwetu03

Senior Member
Sep 15, 2010
190
81
BONGO FLEVA NI STORY YA SUGU, MIKE NA TAJI

JOSEPH Mbilinyi ‘2 Proud’, kazi yake “Ni Mimi" ndio wimbo wa kwanza wa Swahili Rap kusikika Radio One Stereo mwaka 1994. Vilevile akawa Rapper wa kwanza wa Swahili Rap kufanya mahojiano Radio One.

Mike Mhagama, alikuwa mtangazaji wa kwanza kugonga ngoma ya Swahili Rap. Mmiliki wa wimbo alikuwa 2 Proud a.k.a Mr II au kwa uzito zaidi mwite Sugu.

Taji Liundi ‘Master T', ndiye mtayarishaji wa kwanza wa shoo za Swahili Rap. Akawa DJ wa kwanza Bongo kucheza nyimbo za Swahili Rap. Akaasisi kipindi cha DJ Show, Radio One, kilichopiga ngoma mfululizo za Kiswahili.

TUMENG'ENYE STORY

Mike alipiga ngoma ya Sugu “Ni Mimi". Mdundo kwenye spika za radio, ukatema “nipo kwenye microphone, hata unipe nini sitamani sioni, Ni Mimi". Uthubutu wa kucheza wimbo huo nusura umletee balaa kazini.

Sera ya Radio One haikuruhusu Swahili Rap kuchezwa redioni kabisa. Big Boss Julius Nyaisanga, alimuibukia Mike studio, kumtamka ajieleze kwa nini amecheza wimbo wa Sugu kinyume na sera ya taasisi?

Nyaisanga alipoingia studio, akamkuta Mike anapata wakati mgumu kujibu simu nyingi za wasikilizaji waliotaka wimbo wa Sugu urudiwe. Watu walifurahia uthubutu wa Mike. Walipenda wimbo wa Sugu kupigwa redioni.

Nyaisanga akaona hakuna budi, akamruhusu Mike arudie kuucheza wimbo Ni Mimi wa Sugu. “Huwezi kuzuia mvua, Sugu ni mvua kama inanyesha inanyesha" – Sugu!

Wimbo ulichezwa, ukarudiwa na kurudiwa, ikabidi Sugu aitwe kwa ajili ya mahojiano redioni. Demand ilikuwa kubwa.

Master T ‘Taji', akairasimisha Swahili Rap kupitia DJ Show ya Radio One. Ni kupitia DJ Show, mwaka 1996, Mike akaanza kuita Swahili Rap kwa jina la Bongo Fleva.

Hivyo, ukisikia jina “Bongo Fleva”, ujue kuna mahali limetoka. Wimbo “Ni Mimi” wa Sugu uliwapa sababu Mike na Taji kuipigania Swahili Rap kwenye vyombo vya mawasiliano ya umma, kisha jina la Bongo Fleva likazaliwa.

Mei 31, ni siku ya “The Dream Concert”, Sugu atafanya shoo “presidential” Serena Hotel, kuadhimisha miaka yake 30 kwenye game. Mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan. Taji ndiye MC. Mike yupo Marekani anacheza na Benjamins.

Kutoka muziki usioruhusiwa kusikika redioni hadi kuwa sanaa ya heshima na Rais anakuwa mgeni rasmi, ni safari ndefu, ilikuwa kama ndoto lakini sasa ni halisi. Twen'zetu Serena. The Dream Concert.

1654248932093.png
 
But Sugu ni overrated sana hakuna shaka kuwa ni rapa wa kawaida sana kiasi ambacho Solo Thang,Afande sele na Prof J wamemuacha mbali sana
 
We jamaa muasisi ni dhana pana sana, chukulia mfano wa muziki wa reggae haimaanishi Bob Marley ndio mkali wa aina hiyo ya muziki kuliko wanamuziki wengineo hapana lakini yeye ndiye kakomaa kiasi cha kuuweka muziki huo kwenye ramani ukatambulika rasmi
 
Sijakataa kwamba yeye ni muasisi ndio maana nikaanza na neno but .Ni ukweli kuwa japokuwa yeye ni mmoja ya waasisi but kiwango chake sio kama cha hao ambao niliowataja kwenyw hiyo list
 
BONGO FLEVA NI STORY YA SUGU, MIKE NA TAJI

JOSEPH Mbilinyi ‘2 Proud’, kazi yake “Ni Mimi" ndio wimbo wa kwanza wa Swahili Rap kusikika Radio One Stereo mwaka 1994. Vilevile akawa Rapper wa kwanza wa Swahili Rap kufanya mahojiano Radio One.

Mike Mhagama, alikuwa mtangazaji wa kwanza kugonga ngoma ya Swahili Rap. Mmiliki wa wimbo alikuwa 2 Proud a.k.a Mr II au kwa uzito zaidi mwite Sugu.

Taji Liundi ‘Master T', ndiye mtayarishaji wa kwanza wa shoo za Swahili Rap. Akawa DJ wa kwanza Bongo kucheza nyimbo za Swahili Rap. Akaasisi kipindi cha DJ Show, Radio One, kilichopiga ngoma mfululizo za Kiswahili.

TUMENG'ENYE STORY

Mike alipiga ngoma ya Sugu “Ni Mimi". Mdundo kwenye spika za radio, ukatema “nipo kwenye microphone, hata unipe nini sitamani sioni, Ni Mimi". Uthubutu wa kucheza wimbo huo nusura umletee balaa kazini.

Sera ya Radio One haikuruhusu Swahili Rap kuchezwa redioni kabisa. Big Boss Julius Nyaisanga, alimuibukia Mike studio, kumtamka ajieleze kwa nini amecheza wimbo wa Sugu kinyume na sera ya taasisi?

Nyaisanga alipoingia studio, akamkuta Mike anapata wakati mgumu kujibu simu nyingi za wasikilizaji waliotaka wimbo wa Sugu urudiwe. Watu walifurahia uthubutu wa Mike. Walipenda wimbo wa Sugu kupigwa redioni.

Nyaisanga akaona hakuna budi, akamruhusu Mike arudie kuucheza wimbo Ni Mimi wa Sugu. “Huwezi kuzuia mvua, Sugu ni mvua kama inanyesha inanyesha" – Sugu!

Wimbo ulichezwa, ukarudiwa na kurudiwa, ikabidi Sugu aitwe kwa ajili ya mahojiano redioni. Demand ilikuwa kubwa.

Master T ‘Taji', akairasimisha Swahili Rap kupitia DJ Show ya Radio One. Ni kupitia DJ Show, mwaka 1996, Mike akaanza kuita Swahili Rap kwa jina la Bongo Fleva.

Hivyo, ukisikia jina “Bongo Fleva”, ujue kuna mahali limetoka. Wimbo “Ni Mimi” wa Sugu uliwapa sababu Mike na Taji kuipigania Swahili Rap kwenye vyombo vya mawasiliano ya umma, kisha jina la Bongo Fleva likazaliwa.

Mei 31, ni siku ya “The Dream Concert”, Sugu atafanya shoo “presidential” Serena Hotel, kuadhimisha miaka yake 30 kwenye game. Mgeni rasmi ni Rais Samia Suluhu Hassan. Taji ndiye MC. Mike yupo Marekani anacheza na Benjamins.

Kutoka muziki usioruhusiwa kusikika redioni hadi kuwa sanaa ya heshima na Rais anakuwa mgeni rasmi, ni safari ndefu, ilikuwa kama ndoto lakini sasa ni halisi. Twen'zetu Serena. The Dream Concert.
Wimbo wa kwanza wa rap wa kiswahili kuwa mainstream ulikuwa wimbo wa Nigga J, Chemsha Bongo.
 
Mimi ni msafiri bado nipo njiani ,sijui lini nitafikaaaaaaa

Ninaulizia kule ninakokwenda ,sijui lini nitafikaaaaaaaa....

Vipi kwanza unit mkuu.
Kuna ule wimbo wa sijui lini nitafika mpaka leo naukubali kinoma.
Namkutana shetani anauliza we nani na unataka nini, njoo unifuate mimi. Dah miss those old days
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom