Sudan: Maandamano dhidi ya utawala wa kijeshi yaendelea, vyombo vya habari vyalengwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Madaktari nchini Sudan wameandama, kulaani kushambuliwa na maafisa wa usalama wakati wa maandamano yanayoendelea mara kwa mara kushinikiza jeshi kurejesha uongozi wa raia, tangu mwaka uliopita.

Siku ya Jumapili Januari 16, madaktari waliandamana kupinga mashambulizi dhidi ya hospitali na vikosi vya usalama wakati wa maandamano.

Na mashirika ya kiraia yanatoa wito kwa watu kujitokeza tena mitaani Jumatatu hii, Januari 17, kuandamana dhidi ya utawala wa kijeshi, huku mamlaka ikifuta kibali cha Al Jazeera Mubasher, mojawapo ya vituo vya habari vya Qatar, siku ya Jumamosi, pamoja na vibali vya waandishi wake wawili nchini humo.

Kituo hiki cha habari ambacho kimebobea katika utangazaji wa matukio ya moja kwa moja, kurusha picha za kila aina kuhusiana na maandamano mbalimbali, bila maoni, Al Jazeera Mubasher ilimekuwa ikirusha hewani maandamano ya kupinga mapinduzi katika miezi ya hivi karibuni. Maandamano ambayo yalikandamizwa vibaya, na ambayo yamewauwa watu 64 hadi sasa.

Wizara ya Habari siku ya Jumamosi ilishutumu katika barua ya wazi kile ilichokiita "utangazaji "usiokuwa wa kitaalamu" wa matukio ya Sudan kwenye idhaa ya Al Jazeera. Ubalozi wa Marekani umeshtumu uamuzi huo wa serikali ya Sudan wa kufuta kibali cha Al Jazeera Mubasher kinachoiruhusu kufanyia kazi nchini Sudan.
 
Back
Top Bottom