SUDAN KUSINI: Salva Kiir amfukuza Mkuu wa Majeshi

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_95992795_158a4162-146e-40b5-a0e3-8a86d5b5c58d.jpg

Rais Salva Kiir wa Sudan kusini amemfukuza kazi mkuu wa Jeshi la nchi hiyo Jenerali Paul Malong.

Hakuna sababu yoyote iliyotajwa katika vyombo vya habari vya serikali, lakini katika siku za hivi karibuni maafisa wengi wa ngazi za juu wamekuwa wakijiuzulu na pia wengine kutoka serikali ya Sudan Kusini.

Mwandishi wa BBC anasema Jenerali Malong anaonekana na Wasudan wengi kama mtu mwenye nguvu, na wanasubiri kuona atakavyopokea kuondolewa katika nafasi hiyo.

Wengi wamekuwa na wasiwasi kuhusiana na upendeleo wa kikabila na uhalifu wa kivita katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo yameiingiza Sudan kusini katika mgogoro uliodumu kwa miaka minne sasa.

Chanzo: BBC
 
Salva Kiir anahatarisha usalama nchi kumfukuza mkuu wa majeshi.Bora angemuundia zengwe awe eliminated kama anaona ni threat kuliko kumfukuza!
 
Back
Top Bottom